Habari za muda na wakati huu, nimepata meseji na simu nyingi kutoka kwa wanafunzi wakitaka kupata ufafanuzi zaidi juu ya makala zangu mbili nilizoandika siku kazaa zilizopita zikijinasibu kwa jina la "namna mwanafunzi anaweza kusoma kwa mafanikio". Kutokana na ufinyu wa muda, sitoweza kujibu meseji ya kila mtu na vile vile kumpigia simu atakayenibipu ila ukisoma vizuri kama kuna sehemu utahitaji msaada zaidi nipigie simu na usitume meseji ama kunipibu.