Music

Saturday, January 18, 2014

Historia ya mfumo mpya wa dunia - the new world order

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza nini maana ya mfumo mpya wa dunia ? (New world order). Kwa kutamka tu unaonekana ni mkakati wenye tija na una lengo la kutafuta ubinadamu wa kweli kati ya binadamu. Lakini kiuhalisia na hasa ukizingatia mkakati wake wa hawa watu wa ulaya kututawala ,basi mfumo huo unakuwa na kiasi kikubwa kabisa cha upinzani kwa mungu . Mfumo huu mpya unamtukuza zaidi Lucifer ambae ni Shetani Mkuu,



Katika kusoma vyanzo mbalimbali vya habari ninakuja na historia kamili ya vyanzo vya jamii hizi za siri lenye lengo la kusimamia mfumo huu mpya wa dunia.

Mwaka 1773 Meyer RorthChild aliwaalika marafiki zake kumi na wawili katika mjadala wa kutaka kutawala dunia kiuchumi. Hivyo mkakati huo ulilenga kuunganisha assets (Mali) za watu hawa kama mtaji wa kuunda mkondo wa kinyonyaji kwenye uchumi wa Dunia. Katika kikao hicho Meyer alitamka kwamba amempata mshirika madhubuti katika mpango huo.Alimtaja kama kijana jasiri,mwenye upeo na akili vilivyo ambae angeweza kuongoza umoja huo . Huyu hakuwa mwingine bali ni Adam Weishaupt (baadae ndie alienzisha jamii ya siri ya Illuminati)

Tarehe 1, mwezi wa tano mwaka 1776, Weishaupt Alianzisha jamii ya siri ya Order of illuminati .Weishaupt kitaaluma ni Mwanasheria aliebobea katika sheria za kanisa ‘Cannon Law’ na ni mhitimu katika Chuo cha Ingolstad kilichopo Bavaria ambayo ni sehemu ya Ujerumani. Jamii hii ya The Order of Illuminati ilikuwa na malengo yafuatayo :

ü Kuachana na mfumo uliozoeleka wa kiserikali
ü Kuachana na taratibu za kurithi
ü Kuachana na utaratibu wa Dini katika dunia
ü Kuunda serikali moja ya Dunia
ü Kupinga jinsi yeyote ya harakati katika dunia ( Abolition of Patriotism )

Mwaka 1782 Weishaupt aliamua kuunganisha nguvu na Freemasons na katika mkutano uliofanyika Wilhelmsbad ,mheshimiwa mmoja aliekuwa anaitwa Comte de Virieu alitoka kwenye mkutano huo akiwa anatetemeka na hofu kubwa . Alipoulizwa madhumuni na siri zilizozungumzwa alisema kama ifuatavyo ‘Siwezi kudhizihiri siri hizo mbele yenu lakini kubwa nalotaka kuwaambia ni kuwa mambo haya ni makubwa na dhahiri kuliko mnavyodhania’ Hivyo inaonekana katika kikao hicho mambo mengi yalijadiliwa jinsi ya kunyonga uchumi wa dunia hii na kuuweka mfukoni mwao. Tayari maneno na lengo lao likawa ni kwamba ‘Tuhakikishe tunaushikilia uchumi wote wa dunia na pindi tukifanikiwa hilo hatutajali kamwe nani anatengeneza Sheria’ Kwa tafsiri nyepesi ni kwamba watakuwa na uwezo wa kumnunua yeyote yule ataekuwa anakinzana na malengo yao katika dunia yetu .Mpigapicha wa Comte anasema kwamba Comte aliweza kuongelea Freemason kwa shaka kubwa sana.

Kabla sijaendelea na mtirirko huo wa Historia ya New World Order naomba niende ndani kidogo ili tuweze kumfahamu huyu Weishaupt na ana ushawishi gani katika jamii hizi za siri .

Alizaliwa February 6, 1748 na ni motto kutoka kwenye familia ya kiyahudi na baba yake alikufa mwaka 1753. Kijana huyu aliingia katika mfumo wa Kikatoliki akiongozwa na Baron Johann Adam Lckstatt ambae alimuingiza katika jamii ya Wajesuits.Mwaka 1742 Lckstatt alipelekwa na Jesuits akasimamie chuo chao na majukumu ya msingi aliopewa ilikuwa ni kuweka mifumo muhimu katika uendeshaji wachuo hicho .Alistaafu mwaka 1765 lakini hata baada ya kustaafu bado Lckstatt aliendelea kuwa na ushawishi mkubwa kwenye sera na mwelekeo wa Chuo hicho .Weishaupt kwa upande wake aliendelea na kitaaluma na baadae akawa Padri wa Shirika la Jesuits .Akapata kuingia kwenye library ya Lckstatt na huko akasoma vitabu mbalimbali . Mbali na maktaba hii ya Lckstatt Weishaupt akapata pia kusoma na hasa akashawishika sana na kazi za French Philosophers na hii ikampelekea kusoma Sheria,siasa ,uchumi na historia.Moja ya mwanafalsafa aliyemvutia ni Voltire (1694-1778) na ni huyu Voltire ambae alikuwa anapinga kanisa na aliwai kuandika barua kwa King Fredrick 11 ( Great Mason ) na katika moja ya maandishi yake ambayo yanapinga na/au kupanga kudhoofisha kanisa ni kama alivyoandika Lastly, when the whole body of the Church should be sufficiently weakened and infidelity strong enough, the final blow (is) to be dealt by the sword of open, relentless persecution. A reign of terror (is) to be spread over the whole earth, and...continue while a Christian should be found obstinate enough to adhere to Christianity.’ Inaaminika na/au kuhakikishwa kwamba maandiko haya ndiyo yaliyomplelekea Weishaupt kuwa na azma ya kuliharibu kanisa .Akaenda kusoma Ufaransa na kukutana na Robisphere ( baadae robisphrere ndie alieongoza French Revolution ),akajenga urafiki na watu wa nafasi za juu katika’ French Royal Court ‘ na katika muingiliano huu ndipo inaaminika kwamba Weishaupt alikuwa anaingizwa taratibu kwenye ushetani .

Akafanya yafuatayo katika muingiliano huu wa kishetani 

ü Alisoma maandiko mbalimbali ya kupinga kristo yajulikanayo kama Maniech ambayo yanahusika sanasana kama kutabiri nyota na mazingaumbwe.
ü Akatambulishwa kwa Mganga mashuhuri wa kipindi hicho huko Misri ambae alijulikana kama Colmer . Akasoma kazi za Essenes na akapata nakala za ‘Kalaba’ ambao ni ufunguo muhimu wa jinsi ya kuwatumia majini katika kufanya mazingaumbwe .
ü Alisoma pia maandiko mbalimbali ya Ki–freemason na akapanga kuanzisha jamii inayofanana na hiyo .
ü Akatambulishwa kwa RothChilds ( Ambao wanadhaniwa pia kwamba ni waabudu mashetani ) , wakamwamuru aachane na kanisa katoliki na kuungana na jamii za siri nyingine katika kutekeleza mkakati wa ‘ The New World Order’
Kwa historia hii kwa sasa tunapata mwanya wa kumjua Weishaupt ni nani na anasimamia nini . Ametumia muda wake mwingi kupata mafunzo ya kishetani . Hivyo wakati tutakapofanya majumuisho ya jumla ya Illuminati na Freemason tutajua kwa dhati kwamba waanzilishi wake walisimamia nini na hivyo Jumuiya hiyo itakuwa inasimamia nini 

0 comments:

Post a Comment