Maisha tegemezi humnyang'anya mtu utu na hadhi yake. Misaada humuingiza mtu utumwani kifikra, kiuchumi na kiutawala. Humfanya mtu kupoteza mila na desturi zake, na kubaki daima mtumwa wa huyo mhisani. Humfanya mhisaniwa kuwa jalala la mhisani......
Nasema hivyo kutokana na masharti yanayotolewa na wahisani kwa wahisaniwa. Kwa mfano kama atakusaidia kujenga kiwanda ndani ya nchi yako:
1) Wataalamu wote wenye kushika nafasi muhimu na nyeti ni lazima wawe watu wake.
2) Malighafi itoke kwake
3) Mali itakayozalishwa ya kwanza ni lazima iuzwe kwao (First grade)
4) Awe na uhuru wa kutoa fedh nje ya nchi yako (Free money transfer)
5) Watumishi wa kutoka kwao wasitozwe kodi
6) Malighafi kutoka kwao isitozwe kodi
Sasa swali la kujiuliza ni Je, Huyu mhisaniwa atanufaika nini?? Au ndio kubaki kuwa kibarua wa kujitapa anamiliki kiwanda!!!!!!!!!!!!!
0 comments:
Post a Comment