Music

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Showing posts with label ELIMU. Show all posts

Saturday, February 3, 2018

WARAKA KWA MAMA NDALICHAKO (WAZIRI WA ELIMU)

Asalaam Aleikumu watanzania wote wenye imani ya Kiislamu. Tumsifu Yesu Kristo kwa wale wenye imani ya Kikristo. Fuatana name kwenye makala yangu hii kwa Mama Joyce Ndalichako (Waziri wa Elimu)

WARAKA WANGU KWA WAZIRI WA ELIMU (JOYCE NDALICHAKO)

Asalaam Aleikumu watanzania wote wenye imani ya Kiislamu. Tumsifu Yesu Kristo kwa wale wenye imani ya Kikristo. Fuatana name kwenye makala yangu hii kwa Mama Joyce Ndalichako (Waziri wa Elimu)

Thursday, January 22, 2015

Impressive quote


Kama tukisimamia maneno haya ni ukweli usiofichika tutafika mbali kiuchumi na kamwe hawa wnguruwe weupe wataacha kutunyonya..........

Tuesday, December 23, 2014

UDSM YAFUKUZA TENA, SAFARI HII NI VIONGOZI WA DARUSO



Image result for udsm
UDSM INAELEKEA WAPI???
Nawasalimu wote kwa salamu ya kikamaradi ambayo huamkiwa kwa fanani kusema; “Mbiu ya mnyonge” na hadhira kuitikia: “Ni kalamu”…!!!!!!!!!!!
Natumai wote hamjambo na mnaendelea vyema na maandalizi ya sikukuu za krisimasi na mwisho wa mwaka.

Friday, November 28, 2014

My Graduation-UDSM



Thursday, November 20, 2014

UNAIFAHAMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM?



UNAIFAHAMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM?
Uuuuuwiiiiiiii!!!!!!!!!!!! Yarabiiiiii!!!! Mwaka 2009 nilipatwa na furaha isiyokuwa na kifani baada ya kuchaguliwa kujiunga na masomo ya juu katika ngazi ya uhasibu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nilimshukuru maulana kwani ndoto yangu imetimia kwani sio tu kwamba nimefanikiwa kujiunga na masomo ya juu bali ni kwa kufanikisha ndoto zangu za kusoma Chuo Kikuu barani Afrika na duniani kwa ujumla. Toka utotoni nalikua na fikara za kuitwa mwanazuoni wa “Mlimani”…..

NCHI YA KUZIMU

NCHI YA KUZIMU......
Kumi na mbili Aprili, karne ya ishirini....
Wa kwanza si wa pili, Kwa familia mwarobaini......
Nalizaliwa kwenye ukili, Hosipitali hawakuibaini.....
Tanzania Ole nakupenda, ila megeuka nchi jinamizi.

Tuesday, July 29, 2014

Kwa wanafunzi..............

Habari za muda na wakati huu, nimepata meseji na simu nyingi kutoka kwa wanafunzi wakitaka kupata ufafanuzi zaidi juu ya makala zangu mbili nilizoandika siku kazaa zilizopita zikijinasibu kwa jina la "namna mwanafunzi anaweza kusoma kwa mafanikio". Kutokana na ufinyu wa muda, sitoweza kujibu meseji ya kila mtu na vile vile kumpigia simu atakayenibipu ila ukisoma vizuri kama kuna sehemu utahitaji msaada zaidi nipigie simu na usitume meseji ama kunipibu.

Wednesday, March 26, 2014

Mwanafunzi fanya hivi upate kufaulu....P.II

MWANAFUNZI FANYA HIVI UPATE KUFAULU MITIHANI YAKO YA TAIFA
Awali ya yote niwasalimu na kama ilivyo ada kwa tamaduni zetu za kiafrika baada ya salamu kifuatacho ni kujualiana hali ya familia na utokako. Vivyo hivyo na mimi niwe na tumaini moyoni kwamba wewe msomaji wa makala hii u mzima na bukheri wa afya pamoja na familia yako.

Monday, March 24, 2014

Muhimu sana kwa wanafunzi......

MBINU ZA KUSOMA KWA MAFANIKIO
Asallam Allaeikum wenzangu waislamu na tumsifu Yesu kristo kwa wenzangu wenye imani ya kikristo. Vile vile msidhani nimewatenga wale msioamini upande wowote kati ya hizo mbili nilizotaja, la hasha, ila kwa kuwa hakuna salamu moja inayowaunganisha wote basi kila mmoja achukue nafasi yake ajisikie ndani ya moyo wake kwamba nimemsalimu kwa aina ya salamu wanayoitumia kwa imani yao.
Naam! Baada ya salamu hizo nikiwa na imani kwamba kila mmoja amefarijika kwa kutaja imani yake na ameitikia kutoka ndani ya nafsi na moyo wake, nami ni mzima bukheri wa afya tele. Nisileta hoja nyingi sana kwenye utangulizi wa mada ili nisichoshe medulla yako msomaji kabla ya kupata kupakua kile nilichokiandaa.

Tuesday, March 11, 2014

TUJIKUMBUSHE TULIPOTOKA

KARUDI BABA MMOJA
Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali
Wakataka na kauli iwafe maishani. 

Tuesday, February 25, 2014

MCHANGANUO MATOKEO KIDATO CHA NNE

 

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA


 


                                                           







UFAFANUZI WA MASWALI MBALIMBALI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2013


 

 

 

 




Imetolewa Na:

KAIMU KATIBU MTENDAJI

25 Februari, 2014

Tuesday, February 11, 2014

UNAYAJUA HAYA???????

KAMA HAUKUJUA BASI JUA KUWA
1. Kwa mujibu wascientificamerican.com, Mende anaweza kuishi kwa siku TISA bila kuwa na kichwa.


Monday, November 18, 2013

Bunge lakataa kubariki "Division 5"

Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, imevikataa viwango vipya vya alama za ufaulu kwa elimu ya sekondari vilivyotarajiwa kuanza kutumika mwaka huu na kutaka utaratibu na alama zilizotumika mwaka jana, zitumike kupanga matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne wa mwaka huu. Serikali ilitangaza utaratibu mpya wa alama za Mitihani ya Kidato cha Nne na Sita kwa kufuta Daraja la Sifuri na kuleta Daraja la Tano.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stephen Ngonyani alisema jana kuwa kamati hiyo ilichukua uamuzi huo kwa kuwa pamoja na udhaifu ulio kwenye alama hizo, kamati yao haikuhusishwa katika mchakato wa kuandaa alama hizo.

“Mwenyekiti wangu (Margaret Sitta) alisema kile hakiwezekani, kuna viwango ambavyo wameleta havipo kwenye nchi nyingine duniani, tumewaambia wakavifanyie kazi walete tena,” alisema mbunge huyo wa Korogwe Vijijini, ambaye ni maarufu zaidi kwa jina la Profesa Maji Marefu.

Ngonyani alisema waliagiza watendaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhakikisha wanaishirikisha kamati yao kwani imejaa walimu wanaoweza kushauri vizuri.


“Hatutaki watuletee mambo ambayo yamewashinda baada ya kuyapeleka kwa wananchi,” alisema Ngonyani.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome akitangaza uamuzi huo mapema mwezi huu, alisema uamuzi wa kubadilisha mfumo huo umechukuliwa kutokana na changamoto zilizojitokeza mwaka 2012.

Alama zilizokuwa zikitumiwa awali na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), katika kupanga matokeo hayo, kwa Kidato cha Nne ni A=80-100, B=65-79, C=50-64, D=35-49, F 0-34 kwa upande wa Kidato cha Sita, A=80-100, B=75-79, C=65-74, D=55-64, E=45-54, S=40-44 na F= 0-39.

Alama mpya zilizotangazwa ni A=75-100, B+=60-74, B=50-59, C=40-49, D=30-39, E=20-29 na F=0-19. Alama hizo ni kwa kidato cha nne na sita.

Kwa utaratibu huo, A ilitafsiriwa kuwa ni ufaulu uliojipambanua, B+ ni ufaulu bora sana, B ufaulu mzuri sana, C ufaulu mzuri, D ufaulu hafifu, E ufaulu hafifu sana na F ufaulu usioridhisha.

Katika utaratibu huo, mtihani wa mwisho ulitarajiwa kuwa na alama 60 na alama 40 zitokane na alama za Maendeleo ya Mwanafunzi Shuleni (Continuous Assessment-CA).

Mwaka jana baada ya Serikali kufuta matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne, Necta ilitumia CA ya 30 huku mtihani wa mwisho ukiwa na alama 70.

Wadau wa elimu na wabunge walipinga vikali utaratibu mpya wa alama za mitihani hali iliyofanya Spika wa Bunge, Anne Makinda kuamuru wizara husika kupeleka bungeni taarifa yenye maelezo juu ya uamuzi huo.

Kabla ya Serikali kutoa kauli yake, watendaji na viongozi wa Wizara ya Elimu walikutana na Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii Mjini Dodoma mwezi huu ambapo wajumbe wa kamati hiyo walikataa viwango hivyo vipya na kuitaka wizara kuendelea kuvifanyia kazi viwango hivyo kwa kuishirikisha Bodi ya Necta.

Mjumbe mmoja aliyekuwa ndani ya kikao hicho alisema hoja kuu zilizosababisha kukataliwa kwa alama hizo ni ile iliyosemwa kuwa ni kushusha sana viwango vya ufaulu, pia kutaka shughuli hiyo ifanywe kwa kushirikisha Bodi ya Necta ambayo kisheria ndiyo yenye jukumu la kutunga sera za mitihani.

“Tulichosema ni kuwa viwango vya ufaulu pamoja na utaratibu uliotumika mwaka jana, viendelee kutumika kwa mitihani ya kidato cha nne inayoendelea kwa sababu viwango vipya vimekosa uhalisia,” alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.

Wajumbe hao walisema haiwezekani ufaulu wa A ukaanzia 75 wakati hakuna nchi duniani yenye A ya namna hiyo, pia haiwezekani 20 ikahesabika pia kama ufaulu.

“Pia ukiangalia, Kifungu cha Nne cha Sura ya 10 ya Sheria ya Necta kinasema kuwa taasisi hiyo ndiyo yenye jukumu la kutengeneza sera ya mitihani,” alisema mjumbe huyo.

Hata hivyo, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema bungeni kuwa daraja sifuri litaendelea kuwapo lakini hakuzungumzia chochote kuhusu alama ambazo kamati ilishauri wizara hiyo izifanyie kazi.

Mulugo ambaye ndiye aliyehudhuria kikao hicho hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo. Hata alipopigiwa simu yake ya mkononi, iliita bila kupokewa.

Ofisa Habari wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyanzu alisema kwamba hana taarifa za maagizo hayo ya kamati hiyo.

Ufaulu wa chini

Kwa mujibu wa kitabu kinachoonyesha viwango vya ufaulu duniani kila mwaka cha International Qualification, baada ya Tanzania kutangaza alama hizo mpya, sasa inaongoza duniani kwa kuwa na alama za chini za ufaulu.

Nchi zinazofuatia kwa viwango vya chini baada ya Tanzania ni Kenya, Rwanda, Uganda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) ambazo hata hivyo, viwango vyake vipo juu kwa kiwango kikubwa vikilinganishwa na vile vya Tanzania.

Tuesday, October 15, 2013

UDSM IN PICTURE