Music

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Friday, March 14, 2014

KAULI YA SIZITAKI MBICHI HIZI.....

Kitila Mkumbo
Nikisema tunaendeleza utamaduni wa chama kimoja ndani ya mfumo wa vyama vingi watu wengine inawakera na wanaanza kulalamika na kunilalamikia. Lakini sitoacha kusema kwa sababu mimi ni muumini wa falsafa mojawapo ya Steve Biko kwamba “I write what I like’.

Monday, December 2, 2013

TAARIFA YA CHADEMA


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA NDUGU ALI O. CHITANDA

Kutokana na kuwepo kwa taarifa ya Ndugu Ali O. Chitanda, huku pia waandishi wa habari wakitaka kujua na kupata ukweli kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, tunapenda kutoa ufafanuzi mfupi;


Kwanza suala la maamuzi ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi ndani ya chama, Ndugu Zitto Kabwe na Dkt. Kitila Mkumbo, chama kimeshafunga mjadala kwenye vyombo vya habari kwa kuheshimu na kuzingatia taratibu za kikatiba za ndani ya chama kuendelea.



Pili kuhusu suala la restructuring ya Makao Makuu ya Chama. Chitanda ametoa taarifa akiwataja wakurugenzi wafuatao, kuwa ni wapya;



1.Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.

2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika 
3. Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.

Wakurugenzi wote aliowataja si wapya. Mkurugenzi pekee ambaye uteuzi wake ni mpya na umefanyika hivi karibuni na kuthibitishwa ni Mwanasheria Peter Kibatala, atakayesimamia Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu.


Kama ni suala la kuangalia mtu anatokea wapi (ambalo halijawahi wala haliwezi kuwa moja ya vigezo), ili kuonesha ukweli na kubainisha uongo wa watu wanaojaribu kufanya kazi ya CCM wakisema wao ni wanaCHADEMA, kwa kutumia propaganda zile zile na kuzifanya kuwa ni kete zao za kisiasa ndani ya chama, tunaweza kutaja maeneo ya wanakotoka au asili yao kama ifuatavyo;



Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji, Antony Komu- Kilimanjaro.

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama, Wilfred Lwakatare- Kagera.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni, Benson Kigaila- Dodoma.
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John John Mnyika- Mwanza
Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, John Mrema- Kilimanjar.o
Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala- Morogoro.


Hadi sasa uteuzi wa kurugenzi za Makao Makuu ya CHADEMA haujakamilika. Bado kuna nafasi zinazotakiwa kujazwa kwa kufuata taratibu za chama. 



Hii ni kwa sababu maboresho yanayofanyika ndani ya chama, hadi sasa yanaendelea katika ngazi ya Makao Makuu na kanda, kisha itaendelea kwa ngazi za mikoa, wilaya, majimbo, kata, kijiji na hatimaye kitongoji.



Katika maboresho hayo, kwa nafasi za uteuzi, yanayoendelea sasa ambayo yanakwenda hatua kwa hatua, hadi kuwa na makatibu wa kuajiriwa ngazi ya chini ya chama, chama kinazingatia uwezo, uadilifu na utayari wa mtu katika kutoa utumishi bora kwa wanaCHADEMA na Watanzania wote katika nafasi husika.

Suala la maslahi ya watumishi wa CHADEMA ni utaratibu wa chama ambao unajadiliwa, kufikiwa uamuzi na kisha kuridhiwa kwenye vikao vya chama, kama ilivyofanyika kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichoketi karibuni. 



Katika suala hili la maslahi ya watumishi wanaojitolea Makao Makuu ya CHADEMA ambayo si siri, Ndugu Chitanda amesema uongo mkubwa. Kusema kwamba Ofisa Mwandamizi anaweza kulipwa posho kubwa kuliko Mkurugenzi wa kurugenzi husika, ni uongo unaovuka mipaka. 



Ndugu huyo anadhihirisha uongo huo yeye mwenyewe kwa kuandika hivi; 
800,000/= za awali na sasa itakuwa ni kuanzia Tshs. 1,500,000-2,500,000/= kwa Mkurugenzi na kutoka Tshs.6,800,000/=kwa Afisa Mwandamizi na sasa ni Tshs.1,000,000-1,500,000/=”.


Pia si kweli kuwa kila mtumishi anayejitolea Makao Makuu analipwa. Mathalani, wakurugenzi wenye nafasi za ubunge, hawalipwi hata shilingi moja kwa kazi zote wanazokitumikia chama na Watanzania kwa ujumla.



Kwa maelezo hayo ya kutengeneza, ni kwamba hadi sasa Ofisa Mwandamizi anapokea posho kubwa kuliko Mkurugenzi na hata baada ya maboresho atapata posho kulingana na Mkurugenzi. Anapaswa kuwa mkweli. Mtu anayetaka kuonekana muungwana, anapaswa kujiweka mbali na uongo pamoja, maneno ya kutunga pamoja na upotoshaji wa makusudi.



Kama ilivyoelezwa hapo juu, restructuring inaendelea. Ni hatua kwa hatua. Itafika ngazi za chini kama Baraza Kuu lilivyoagiza. Kwa sababu hiyo hadi sasa uteuzi wa Makatibu wa Mikoa na Wilaya haujafanyika. 



Hata hivyo ruzuku imekuwa ikipelekwa kila kanda, mkoa, wilaya na jimbo kama ilivyoridhiwa na Kamati Kuu. Na hii ni zaidi ya pikipiki, kompyuta na magari yaliyopelekwa kila kanda. Angelikuwa mkweli, nagelisema na hili pia.



Ndugu Chitanda anajichanganya sana katika taarifa yake yote. Hii ni moja ya sifa ya kukosa hoja hivyo mtu anaamua kuibua viroja au kutunga maneno kwa sababu ya kujaribu kuukana ukweli anaoujua moyoni. Tutatoa mfano mmoja; 



Kupitia taarifa yake, anasema alikuwa mtu aliyeaminiwa hadi kuwa katika vikao muhimu, lakini wakati huo huo anasema kuna ubaguzi! Tunapaswa kumhurumia kwa kushindwa kuunganisha hata mawazo yake na kupata mtiririko wa hoja zenye mantiki! Angelikuwa mkweli angesema katika vikao vya sekretarieti na CC, aliingiaje kama kuna ubaguzi wa dini!



Kwa sababu anazozijua yeye, Ndugu Chitanda ameamua kujipachika cheo ambacho hajawahi kuwa nacho. Amejiita kuwa ni Katibu wa Sekretarieti ya Makao Makuu. 



Ndani ya CHADEMA pamoja na kwamba nafasi hiyo imetajwa ndani ya Katiba ya Chama, hakuna mtu ambaye ameteuliwa kutumikia nafasi hiyo. Kama anaweza athibitishe kwa kutoa barua ya uteuzi kutoka kwa Katibu Mkuu.



Mahali pengine amejitambulisha kuwa ni Katibu Ofisi ya Katibu Mkuu. Ofisi hiyo ina Katibu Mtendaji mmoja ambaye ni Mzee Victor Kimesera, mmoja wa waasisi wa CHADEMA.



Operesheni ya Chama inayoendelea nchi nzima kwenye majimbo 103, si suala la siri wala lengo bovu kama anavyotaka umma uamini. 



Ni mwendelezo wa mpango mkakati wa chama kupitia progamu za Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), unaotekelezwa kwa hatua mbalimbali na kwa mbinu tofauti tofauti pamoja na dhana ya CHADEMA ni msingi. 


Operesheni hiyo ambayo ni mwendelezo wa nyingi za namna hiyo zinazokwenda ngazi za chini kabisa za chama, zikilenga kuimarisha taasisi na mifumo, imeanza wiki hii na ilitangazwa mbele ya waandishi wa habari.



Tungependa kumalizia ufafanuzi huu mfupi kwa kutoa tahadhari kwa umma kuwa makini na matamko ya watu wa namna hii. Maana tunajua kwa uhakika yako mengi ya namna hii yataandaliwa na kutolewa kadri ambavyo Watanzania wanakaribia kuona na kuishi matumaini ya mabadiliko ya kiutawala na mfumo ndani ya nchi yao.



Mathalani katika taarifa yake, Ndugu Ali Chitanda amedhihirisha na kuonesha kuwa ni aina ya watu ambao wanaCHADEMA na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kuwaangalia kwa macho ya kuhoji na tahadhari ya hali ya juu, anasema hivi; 



“Kwa kuwa siamini kwamba kuvuliwa nyadhifa kwa Zitto Kabwe na Dkt Kitila Mkumbo ni kwa sababu ya waraka wa ushindi, bali ninaamini kuvuliwa kwao ni kutokana na hofu ya uchaguzi, ubaguzi wa kikabila na kikanda.” 



Aya hiyo pekee inayotumia lugha wanayotumia mahasimu wa CHADEMA, wakiongozwa na viongozi waaandamizi wa CCM, wanaohangaika kutokana na Watanzania kuwakataa, wakijiandaa kuwaondoa madarakani kwa sababu sera zao zimeshindwa, inatosha kuonesha uhalisia wa yeye mwenyewe (mtoa taarifa) alivyo. 



Ni kauli za namna hii (kuwatisha na kutaka kuwatenganisha Watanzania) ambazo zimekuwa zikitumiwa na watawala kama njia pekee ya kutaka kuzuia upepo wa mabadiliko unaovuma nchi nzima, zimekuwa zikiwaunganisha zaidi Watanzania kuiunga mkono CHADEMA bega kwa bega, ili kupata haki na matumaini ya wanyonge, katika mapambano ya awamu ya pili, kuelekea uhuru wa kweli. 




Imetolewa leo Novemba 30, 2013, Dar es Salaam na;


Tumaini Makene

Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA

Monday, November 18, 2013

Kauli ya Lema-mbunge wa Arusha mjini

Lengo la Uongozi lisiwe Madaraka bali Mabadiliko yaliyojaa Utu – LEMA

Nimekuwa nikifuatilia mijadala mbali mbali inayohusu CDM katika vyombo vya habari na hususani mitandao ya jamii , nimeona fikra nyingi halali na haramu na nikajiridhisha kwa uhalisia kabisa kuwa Taifa linahitaji ukombozi mkubwa wa fikra . Watu wengi wanaopita katika mitandao ya jamii na kutoa maoni juu ya hali ya Nchi na Vyama vya siasa na matukio mengine mbali mbali unaweza kabisa kusema ni kundi kubwa ambalo lina mwanga kiasi katika matumizi ya vifaa vya electroniki au komputya na kundi hili linaweza kutajwa kama kundi lenye uelewa wa mambo japo kidogo .

Hata hivyo kuna tofauti kubwa sana kama utajaribu kufanya utafiti kupitia maandiko yao mbali mbali na michango yao katika kuelimisha Jamii , pengine tofauti hii kubwa inatokana na hisia za kishabiki ambazo zinapewa kipaumbele kuliko mambo ya msingi yanayoweza kuleta fikra chanya katika Jamii . Nimeona maandiko mbali mbali kuhusu Chama changu ninachokitumikia na Nchi yangu , nimekuwa nikishangazwa na ushauri wa maadui zetu kuhusu mustakabali wa Chama Chetu , Maadui zetu ambao wanatupiga kila siku , kutubambikia kesi , kuuwa watu katika mikutano yetu na mateso mbali mbali mabaya kuna saa unawaona wakijaribu kuhimiza umoja wetu kama nguzo muhimu ya kuwatoa madarakani wao . Hili ni fumbo kubwa kwetu ? 

CHADEMA itachukua Dola 2015 . Changamoto na matatizo yeyote yatakayoonekana sasa na hapo baadae hayatakuwa kikwazo katika ndoto hii muhimu bali ni ufunguo katika kufikia haya mafanikio kwa ufasaha zaidi . Natambua kuwa Viongozi tunawajibu muhimu katika kujenga Demokrasia isiyo na chembe ya hofu wala uoga kwani katika ujenzi wa demokrasia ya ukweli ni vyema tukaendelea kufundisha watu namna muhimu ya kushinda hofu na uoga kama nguzo kuu ya ulinzi wa rasilimali na Nchi yao , Chama hiki kitakuwepo na kitaendela kuwepo na hakuna Mtu wala kelele za kuangusha Chama hiki natambua juhudi kubwa zinafanyika ndani yetu na nje yetu kuangusha Chama hiki na faraja ya maadui imekosa hekima kwani kuua chama Kikuu cha upinzani Nchini ni kuua demokrasia na kuua demokrasia sio faida kwa watawala kwani wananchi wanapotaka mabadiliko kama wakiyakosa kwa haki na njia sahii watayatafuta kwa silaha , kwa hiyo ukuaji wa demokrasia ni muhimu katika ulinzi wa Amani ya Nchi , ingekuwa kuuwa Upinzani na Chadema ni kumzorotesha Mtu binafsi na sio maono muhimu katika utawala wa Nchi yetu basi Chama hiki kingeweza kufa , lakini kwa sababu sio hivyo basi ni vyema maadui wakajua wanafanya kazi ambayo hawatafaulu kwani Demokrasi , Haki , Ukweli , Usawa na Utu ni tabia ya Mungu na hivyo Chadema ni mpango wa Mungu kelele za shetani na Watu wake haziwezi kuangusha Mbingu .

Wanachama wetu ni muhimu wakajua CCM ni adui wetu si kwa sababu ya rangi ya bendera yao ila ni kwa sababu ya matendo yao , hatuwachukii CCM kwa sababu rangi yao ni kijani isipokuwa tunachukia matendo yao na tabia zao ambazo zimezorotesha Taifa katika kila Nyanja mbali mbali na huu ndio ugomvi wetu mkubwa na Chama hiki katili .
Tulipowafukuza Madiwani Arusha nilisema hivi “ Kama Madiwani wanaweza kukaidi agizo la Kamati kuu juu ya mahusiano yenye usaliti katika baraza la Halmashauri ya Jiji la Arusha na sisi tukaona ni vyema wao kuendelea kwa sababu ya kuhofia uchaguzi , Je tutawezaje kama Chama cha Upinzani kikubwa kuwanyooshea Chama tawala vidole kwa kushindwa kuwawajibisha viongozi wake wenye tuhuma mbali mbali tena waliokuwa na nyadhifa kubwa Serikalini ? . Kuliko tuchukue Dola 2015 na Watu wasio na rangi inayojulikana ni bora tuendelee kuwa Chama cha Upinzani , kwani lengo la msingi la Chadema lisiwe kutafuta heshima na utukufu katika uongozi bali mabadiliko na utu wa kweli katika Taifa letu .

Huu ni wakati muhimu kuelekea uchaguzi mkuu 2015 ambao ni lazima tutafakari sana , je tunataka kura kwa ajili ya utawala au kura kwa ajili ya mabadiliko ? Maadui zetu wa nje ni wepesi sana wamekwishalegea kinachosubiriwa ni juhudi zetu ili kufika kileleni , hatuwezi kufika kileleni huku wasaliti wakiwa ndani yetu ni lazima kama Chama sasa tuchukue hatua . Hatua hizi ngumu haziwezi kuwa na test ya raha bali uchungu ambao ni lazima uvumiliwe ili kufikia malengo muhimu , Mwanamke mjamzito ana njia mbili ya kujifungua Mtoto , moja ni kwa njia ya kawaida na pili ni njia ya upasuaji na zote zina maumivu na mateso lakini baada ya hapo Mtoto huwa anakuja na furaha na faraja na zawadi mbali mbali na Mama kusahau changamoto zote alizopitia . CHADEMA ni tumaini kubwa Tanzania ni muhimu sasa kuchagua njia muhimu ya kusafisha Chama kabla mambo hayajifika mbali na kama tukikosa madaraka na sababu ikawa ilikuwa kujisafisha wenyewe basi sababu hii itakuwa ina maana kubwa kwa sisi kutokuchukua madaraka na utawala wa Nchi hii , kwani lengo lisiwe madaraka bila mabadiliko bali Mabadiliko na mamlaka ili kuweza kurudisha utawala unaojali haki , utu na heshima katika Taifa hili .


Katika msingi wowote wa maamuzi magumu lazima tutambue kwamba , kelele , dhihaka , matusi , kashfa vitainuka kwa kiwango cha juu na kwa msaada mkubwa wa maadui zetu lakini ni vyema tukatambua kuwa Uongozi ni kukumbana na Changamoto mbali mbali kama vile hofu , mashaka na vishawishi na kuamua kuzishinda kama ambavyo Wright Brothers walifanya katika ugunduzi na utafiti wa kurusha ndege Duniani hata hivyo faida kubwa tuliyo nayo ni kuwa Wanachama wetu wamekuwa wengi sana kwa hiyo hatuna Mtu maarufu tena ila tuna CHAMA maarufu na mashuhuri , tulipofukuza Madiwani Arusha kuna Watu walisema Chadema imekwisha Arusha na wengine walijitapa kuwa wao walikuwa wanakubalika kuliko Chama lakini uchaguzi wa hivi karibuni wa Madiwani unaonyesha kuwa CDM Arusha imeshinda kwa aslimia kubwa kuliko ilivyokuwa mwaka 2015 tena kwa Watu wapya na wenye sura ngeni katika Siasa , pamoja na kuwa maamuzi ya kufukuza madiwani yalipigiwa kelele sana lakini msingi wa kufukuza madiwani ulikuwa muhimu kwa afya ya Chama na Nchi kwani utawala usiokuwa na nidhamu ni sawa na kupanda mahindi katika tiles , japo kuwa tiles ni nzuri kuliko udongo lakini mahindi hayawezi kuota na kwa hiyo kwa kadri utovu wa nidhamu unavyokuwa sugu ndivyo ambavyo roho ya usaliti inakuwa muhimu kwani “ you can not feel bad to discourage the move that you do not respect “ Ukitafakari kwa makini sana utagundua kuwa historia haijawi kuwapa kipaumbele wasaliti hata siku moja, kwa hiyo ni muhimu wanaosaliti hii kazi muhimu wakajua hivyo kwamba heshima yetu ni Chama Chetu na sio Majina yetu kwani tukijenga Chama imara hata kama hatutakuwepo Chama kitaendelea kuwepo na hapa kanuni ni moja tu “ Nguvu kubwa ya mshikamano na Upendo wetu itakapokuwa muhimu kwetu kuliko Ubinafsi wetu na Sifa binafsi basi safari itakuwa imefika mwisho “ Sio tu kwa kushinda dola bali kwa kubadilisha mitazamo ya fikra katika Siasa jambo ambalo ni muhimu sana kwa wakati huu kuliko hata kushika madaraka .

Kuna uoga mkubwa sana katika Taifa hili ni vyema tukajenga kizazi kinachoweza kushinda hofu na kusimamia Nchi yao katika haki na kweli kwani ni hatari sana kwamba leo ndani ya Bunge hata kutaja majina ya wezi wa mali ya Umma eti inahitaji ITIFAKI , lakini katika hatua hii muhimu ya kuondoa hofu na kufundisha ujasiri Jamii lazima Viongozi wakubali kuwa wataitwa majina yote mabaya kama ambavyo Mandela aliitwa wakati alipokuwa anataka utu wa Watu wake .

" Dhambi mbaya na kubwa kuliko zote duniani ni uoga " 


Godbless J Lema

Tuesday, October 15, 2013

TAARIFA KWA UMMA/WADAUTAREHE 15 OKTOBA 2013 MKUTANO WA BARAZA LA UONGOZI LA KANDA YA KASKAZINI NA WADAU WA CHADEMA WAPENDA MABADILIKO NA UHURU WA KWELI.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Kanda ya Kaskazini kinapenda kuwatangazia na kuujulisha umma na wadau wote kutoka mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Arusha kuwa tarehe 25 hadi 27 Oktoba 2013 katika JIJI la Arusha yalipo makao makuu ya chama kwa kanda, kuwa kutafanyika mkutano wa Baraza la Uongozi la Kanda tarehe 25 Oktoba, ambalo
litajumuisha viongozi wa mikoa na mabaraza ya chama ngazi ya mikoa kutoka kanda ya kaskazini, Wabunge wote kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri zilizopo chini ya CHADEMA kutoka kanda ya Kaskazini na wajumbe wa kamati kuu wanaoishi ndani ya kanda ya kaskazini.

Sambamba na mkutano huu wa baraza la uongozi, tarehe 26 na 27 Oktoba, utafanyika mkutano wa wadau wote wa chama na wapenda mabadiliko ya kweli kutoka kanda ya kaskazini. Wadau hawa ni pamoja na wanasheria wote, wachumi, wahasibu, wahandisi, wahadhiri wa vyuo na waalimu, wanahabari, wafanyabiashara, viongozi wa dini na makundi yote maalumu na ya kitaaluma, wote wanaalikwa kushiriki katika mkutano huu ambao una lengo la kutoa fursa kwao kama watanzania wakiwa kama wadau wa kweli waweze kuitumikia nchi yao kupitia CHADEMA.

Katika mkutano huu wadau watapata fursa ya kushirikishwa katika nafasi za kimaamuzi na kiutendaji za kanda kwa lengo la kuijenga na kuiimarisha CHADEMA ambayo imekuwa na imeendelea kuwa tumaini kwa Watanzania kwa wakati huu wa uhitaji mkubwa wa mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi katika nchi yetu.

Mkutano huu utafunguliwa na pia kuhudhuriwa Mwenyekiti wa CHAMA Taifa Mhe Freeman Mbowe (MB) ambaye pia ni mbunge kutoka Kanda ya Kaskazini.

MAWASILIANO yote yafanyike kupitia kwa MRATIBU - KANDA
Ofisi ya KANDA – ARUSHA – Ngarenaro: NHC Nyumba Na. 8
S.L.P. 12525, Arusha, Tanzania. Simu: +255 784 343 275,
Email: chademakaskazini@gmail.com Tovuti: www.chadema.or.tz
Wadau wote mnakaribishwa sana kuhudhuria mkutano huu.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na ushiriki kwenye mkutano huu tafadhali tumia mawasiliano kwa
njia zifuatazo:
Simu: +255 758 976 260
+255 656 557 586
+255 755 282 878
Barua pepe: chademakaskazini@gmail.com
golugwa@gmail.com
Imetolewa leo tarehe 15 Oktoba 2013
Amani S. Golugwa
KATIBU – KANDA YA KASKAZINI

Thursday, October 10, 2013

KIONGOZI MAKINI NI HUYU....

Mr. President, the faculty, staff, students, invited guests and the public at large. Allow me to express my gratitude, for the cordial welcome at your lovely campus. It is one of a kind, and If I could, I would have stayed much longer to learn more on your success that I could take back to our young people. The environment and the surroundings are as beautiful as the people themselves. Along the way, I have met great people with great hearts, and I thank you for that.

Likewise, receive greetings from the people of Tanzania. I was quite impressed with your level of research, and the homework you have done trying to know Tanzania, I was also particularly touched by some of you in the audience that knew the geography of my country; and even trying to challenge me . Mrs. Macquire, “People of Mto wa Mbu” are definitely proud of you for being such a good Ambassador. We thank you, and Tanzania needs more of you that will help in exposing it to the people of America
.

The Samford community, my journey has been long and tedious; I have travelled through hills and valleys of trials and tribulations. However, due to the need and challenges we face as a nation, physical fatigue of travel would not stop me from marching forward. I am determined to work with my countrymen to see our nation of Tanzania reach the Promised Land.

Tanzania is a great and rich country, with rich culture and rich people at heart. Her people have sent me on a study tour. They have sent me to learn the secrets of your success as a society

Tanzania is one of the most blessed countries on the face of the earth. It has abundance of natural wealth, and for those who understand the world history, know that the best game parks are in Tanzania. It is the place believed to be the cradle of mankind.

Tanzania is the home of Mt. Kilimanjaro, Serengeti national park, Ngorongoro crater, and Olduvai Gorge where the first man is believed to have lived. We have some of the world best beaches; our people are very hospitable and extremely welcoming. I welcome all of you to Tanzania

For a long time, Africa has been known as a dark continent infested with disease, poverty, starvation, illiteracy and never endings wars. This might have been created in your minds with the images in your televisions. I can’t blame you, because this is the truth you know

However, this is far from the reality. Africa and Tanzania in particular is the new frontier. Tanzania is a country rich in natural resources and only lacks human capital. It is a country with rich land and plenty of water bodies
Many African leaders are believed to come to Washington and other western capitals begging for handouts known as foreign aid. This has created a notion in the minds of many that Africans are poor and lazy.

This is not the case.

Africa is transitioning from mismanagement, dictatorship and corruption that have plagued the continent. Corruption is the main vice depriving Tanzanians and other Africans a chance to a better education, better healthcare and economic prosperity.

Well, I am not here to beg, because my country is rich. I know clearly well that, foreign aid does not come cheaply. It comes with a condition of signing up our sovereignty

I am not here for foreign aid, and CHADEMA party which I represent does not believe on foreign AID. This is my party’s philosophy, and any sane human being would not want to live off handouts, or going around begging because foreign aid is only needed as short term relief for countries coming out of calamities. Rwanda needed help to so it could emerge out of the ruins of genocide. Once it did, it became less interested on the foreign aid now a success economic story in Africa

Foreign aid is a form of slavery which creates a false sense of entitlement. It confines a beggar into a psychological and mental prison of his own creation, becoming incapable to make any meaningful decision of his own. He does not think on how to get out of his difficulties as long as he knows that, someone somewhere will help him.

CHADEMA party believes that all too often, foreign aid creates dependency by the receiving country onto the giving country and winds up in the pockets of corrupt rulers.

Foreign aid money are your taxes, your sweat which should work for your benefit not for people sitting on their wealth. More important than your dollars, are your brain trust, investments and technological advantage. This is what we need to utilize our resources and also in planning for years beyond our non-renewable resources

Our country rich in resources is being exploited by foreign entities, while our President is busy trotting the world begging for mosquito nets. With our resources, we can make our own mosquito nets without them being donated to us. Chadema party which I represent is poised to changed that, and the most important tool we need is the development of human capital

We need our resources to benefit our people. We need to create jobs for our people, we need to improve our health care, we need to improve our education, our infrastructures, communication and economy as a whole. And this is only possible if can with the wealth that we have all we need is better education for our people

We are currently having inequitable trade, where far eastern countries are exporting their poor populations to compete for jobs with our citizens. They are even exporting to us their prisoners to work on our roads yet millions of our young men have no jobs. This is not possible in any civilize society, unfortunately, because our rulers have signed contacts shrouded in secrecy whose contents are only known to them

Some of these individuals have turn to insult us as a nation. They are now interfering on our sovereignty, publicly aligning themselves with political parties. A whole ambassador standing on a political platform to address a political rally, and has ignored the public call for him to leave the country!

This is not the kind of trade we are looking for. We are looking for partners that will work with us to develop our resources in order to benefit our people; Partners that will bring to our country new skills, and also create jobs for our graduates. We need your expertise so we can turn our country into a bread basket of Africa. America is the world’s land of milk and honey where everyone wants to be, that’s the model we want to learn from

Well, we have come to realize, that if you feed us today with your milk and honey, our meals for tomorrow may not be guaranteed. We instead want to know how you made your country into a land of milk and honey so we can be able to feed ourselves for unforeseeable future and also feed the rest of the world. We have the potential but lack the expertise, and the know how is what we need

Tanzania is not an island; it is part of the global community where all humans have the liberty to visit whenever they want. Our boarders are open for all, as long as our laws and culture are respected. All we need is trade partnership that will guarantee fifty-fifty trade, in which the country benefits equally with the investor.

The younger American generation, I am inviting you to visit Tanzania; I am talking to you as the investors of tomorrow. Come and explore the endless possibilities my country has for you. We need investors that will bring into our country, a set of skills and creativity to turn our hardwood into high quality, made in Tanzania products, as opposed to bringing cheap furniture made of plywood while hauling away our valuable timber

Chadema party believes on the free market economic philosophy in which individual creativity is rewarded. We need your partnership in fostering individual innovation within our people. We don’t need your tax money; neither do we need your mosquito net donations, we need your skills.

We don’t need shoe boxes, we need to know how to make our own shoes. We need your technological know how
CHADEMA party’s priority number one is education! Priority number two is education and so is the priority number three.

We believe on education to be the only way for Tanzania to rise from the abject poverty it is in today. We have no alternative but train our young people who will in turn, employ their intellectual creativity into full practice to enable Tanzania become an economic giant in a continent long forgotten

Samford is one of the American’s finest educational institutions. It is producing some of the world finest, from school teachers to the finest lawyers. It is my hope that we see your institution open its doors to our support and in preparing Tanzania’s aspiring scientists, teachers, and accountants to become innovators.

In our effort to make our country a unique success story, I am challenging you the young people to go out to the world, and open new trails for others to follow. Tanzania has its doors open for you.

Thank you all for listening.

Dr Wilbrod Peter Slaa is the General Secretary of the Main Opposition Party in Tanzania (CHADEMA).He came second during the 2010 Presidential elections which President Kikwete won. Dr Slaa is expected to contest in the year 2015 General elections.He is the number one critique of President Kikwete's government.

Friday, August 2, 2013

SERIKALI ILIKOSEA HAPA KWENYE MADAI YA MADAKTARI


Nianze kusema kuwa mimi ni daktari, na ningependa kwa pamoja tusio madaktari na madaktari tujadiliane katika uzi huu, si kwa kuonyesha hisia (hasira,matusi,kejeli n.k), kupoteza muda, kupotosha madai na taarifa na bali kwa kuona mapungufu ya chanzo cha mgomo kabla ya kujadili madhara yake, ili wote kama watanzania(na wasio watanzania pia) kuliweka sawa hili na kulisaidia Taifa.


MADAI NA UFAFANUZI:
-Uwajibishwaji wa watendaji wakuu wa W/Afya
Ufafanuzi: Kutokana na ubadhirifu uliothibitika, hatua za kinidhamu zilipaswa kufuatwa.

-Uboreshwaji wa Huduma za Afya katika hospitali.
Ufafanuzi: Upatikanaji wa vifaa kazi, madawa na mazingira ya Hospitali ili kutoa huduma stahiki wa wagonjwa. Yaani 
Upatikananji wa vitendea kazimachine za upimaji moyo, kifua, sukari, uzito, urefu n.k), Mashine za Oxygen, vifaa vya kuongezea maji na damu mwilini n.k .
Upatikanaji wa nyenzo(Machine kama vile CT Scan, MRI, Mashine za mionzi yaani X-ray, mashine za matibabu yaani mionzi ya kutibu saratani)
Mazingira-Kuongeza vitanda, mashuka, huduma za chakula kwa wagonjwa wasio na ndugu n.k

-Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (Risk allowance) 30% au Chanjo
Ufafanuzi: Katika mazingira ya sasa ambapo unaweza kuambukizwa Kifua kikuu(TB), Homa ya Ini (Hepatitis), UKIMWI (HIV/AIDS) tunapaswa kujikinga dhidi ya magonjwa haya tunapokuwa tukitibu wagonjwa na hivyo ni vyema serikali kutoa chanjo au isipowezekana kutoa chanjo na itoe posho tajwa kujikinga, mfano chanjo ya Homa ya ini pekee kwa mwaka ni mara 3 na inagharimu 45,000 (30USD) kwa kila chanjo.

-Posho ya kuitwa kazini(On call allowance)-5%
Ufafanuzi: Kisheria(Sina uhakika na kifungu), Muda wa kuitwa kazini au katika kada/sekta nyingine huitwa “Overtime” ni asilimia tano(5%) ya mshahara na hivyo, sheria ifuatwe katika hili.

-Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu(Hardship allowance)-40%
Ufafanuzi: Si madaktari wote(yaani madaktari 1500) wafanyao kazi katika hospitali za serikali wanafanya kazi katika mazingira magumu bali, wachache hasa walio vijijini na hivyo, ili kuwapa motisha na kuonyesha njia ya motisha ili madaktari wasibaki mijini tu na hivyo kuwafanya waende vijijini ili kuepuka usumbufu wa wagonjwa kusafiri toka mkoahadi mkoa kwa matibabu, posho ya mazingira magumu itolewe kwa madaktari hawa walio vijijini na si wote.

-Posho ya Usafiri(10%) au mkopo wa magari.
Ufafanuzi: Kwa madaktari wale kukaa mbali na hospitali, wapatiwe posho hii au mkopo wa gari(NA PESA HII IKATWE KATIKA MSHAHARA). Hii ikiwa na maana daktari aliye zamu na anayeishi(mfano) bunju na kufanya kazi Muhimbili, au anayeishi Vikindu na kufanya kazi Amana, anayeishi kimara mwisho na kufanya kazi Temeke nk katika mikoa mingine anayetakiwa kufika usiku saa nane na hakuna usafiri anaweza kufika kwa wakati.

-Posho ya makazi (30%) au kupatiwa nyumba.
Ufafanuzi: Kisheria (“Doctor is equal to high government officer and is entitled to a house”).Nitapokuwa na vifungu vya sheria nitathibitisha hili. Na kwa kuwa jambo hili lipo kisheria basi na sheria ifuatwe(na ndio Seriakali ilisema inajenga nyumba 700 za madaktari), lakini isipowezekana kwa daktari kupatiwa nyumba(kwa ambao hawana) basi posho ya asilimia 30% itumike kama mbadala.

-Wafanyakazi wote wa Sekta ya Afya wapewe kadi za kijani za bima ya Afya.
Ufafanuzi: Kwa wafanyakazi wa sekta ya Afya yaani madaktari, wauguzi, wafamasia, watu wa maabara, nk. Wapewe bima za Afya wakipata huduma sawa na ile wanayotoa.

-Pendekezo la mshahara kuwa mil. 3.5/=kwa mwezi.
Ufafanuzi: Kama vile mishahara katika Serikali inavyotegemea 
*Muda wa masomo wa fani. 
*Kiwango cha elimu.
*Ugumu wa masomo wa fani husika.
*Ugumu wa kazi.
*Muda unaotumika kazini.
Hivyo kwa kuzingatia haya, pendekezo la mshahara tajwa utolewe kwa madaktari lakini kama ikishindikana basi Mwajiri(Seerikali) na itoe pendekezo lake. 

MAKOSA:
Jumla ya madaktari wote katika hospitali zaSerikali ni 1500, hii ikiwa ni takwimu ya Wizara ya Afya yam waka 2011 na ikijumuisha zaidi ya madaktari 300 waliofukuzwa na 150 waliokwenda nje tayari hadi leo trh 17.07.2012. Hivyo tafsiri iliyotumika ni ;
-Daktari hayuko entitled kupata nyumba kama high government official kama ilivyoainishwa kisheria
-Daktari hatakiwi kulipwa overtime (call allowance)mara baada ya muda wa kazi kwa aslimia tano ya mshahara 
-Tafsiri ya kuwa madaktari wote huwa wanakuwa zamu za usiku (overtime) na hivyo kuwekakiasi cha posho tajwa juu kuwa ya madaktari wote na kila siku! 
-Tafsiri ya pesa ya mazingira magumu kwa madaktari wote(KWANI SI MADAKTARI WOTE WAKO MAZINGIRA MAGUMU YA VIJIJINI)
-Tafsiri ya kutaka posho ya mazingira hatarishi pekee badala nyenzo za kujikinga na chanjo
-Tafsiri kuwa wafanyakazi wengine wa sekta ya afya hawakujumuishwa katika madai.
-Tafsiri ya pendekezo la mshahara tajwa kuwa ni SHURUTI ya kurudi kazini.
-Tafsiri ya kuwa PENDEKEZO la mshahara haliwezi kupungua!