Music

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Monday, November 24, 2014

IFAHAMU UDSM PART 2


Ndugu mfuatiliaji wa kisa hiki, karibu ungana nami kwenye sehemu ya pili ya “unaifahamu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam?” Kabla sijakudokeza wapi tuliishia wiki iliyopita, nisiwe mchoyo wa fadhila kukupeperushia zangu salamu zikukumbe popote ulipo. Bila hiyana nikupongeze pia kwa kunipa muda wako tena bure kabisa kwa kusoma mtiririko wa makala zangu kupitia kitovu cha fikra endelevu cha “Fukununu.blogspot.com”. Hii inanipa moyo wa kuzidi kuandika, kuanika na kuchimbua na kuibua mengi ambayo yapo nyuma ya pazia ama yanasikika kwa nadra sana kutokana na mfumo beberu na kandamizi ulioota mzizi ndani ya jamii yetu hii ya “adabu na utii kwa bwana mkuu” (Amani)

Friday, November 21, 2014

ILANI YA COMRADE.....



ILANI YA COMRADE
Asubuhi na mapema, Usingizini nakurupuka….
Lahaja tamu natema, moyoni nafunguka………
Tena bila kuhema, wala machoni kuyumba……
Comrade nanena, huyu mwana anankuna.

Thursday, November 20, 2014

UNAIFAHAMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM?



UNAIFAHAMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM?
Uuuuuwiiiiiiii!!!!!!!!!!!! Yarabiiiiii!!!! Mwaka 2009 nilipatwa na furaha isiyokuwa na kifani baada ya kuchaguliwa kujiunga na masomo ya juu katika ngazi ya uhasibu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nilimshukuru maulana kwani ndoto yangu imetimia kwani sio tu kwamba nimefanikiwa kujiunga na masomo ya juu bali ni kwa kufanikisha ndoto zangu za kusoma Chuo Kikuu barani Afrika na duniani kwa ujumla. Toka utotoni nalikua na fikara za kuitwa mwanazuoni wa “Mlimani”…..

NCHI YA KUZIMU

NCHI YA KUZIMU......
Kumi na mbili Aprili, karne ya ishirini....
Wa kwanza si wa pili, Kwa familia mwarobaini......
Nalizaliwa kwenye ukili, Hosipitali hawakuibaini.....
Tanzania Ole nakupenda, ila megeuka nchi jinamizi.

Wednesday, November 19, 2014

TAFAKURI PART 3

TAFAKURI YANGU.......

Ni jukumu la mtanzania mmoja mmoja kuanzia ngazi ya familia kuanza kujenga jamii mpya yenye uadilifu, kwa hatua taifa lilipofikia hakuna muujiza utakaoweza badili maadili mabovu ambayo kwa sasa yanamulikwa kwa urahisi kupitia kwa viongozi wa serikali ambao ni rahisi kujua maovu yao kutokana na uchungu tulionao kutokana na kodi zetu.Lakini tukiamua kujichunguza kila mmoja wetu utagundua udhaifu uliona au matendo kadhaa ambayo ungekuwa kiongozi ungeyafanya na na kuligharmu taifa kama wafanyavyo wengine.

Sunday, November 16, 2014

Nasaha zangu kwa wakazi wa kata yangu ya Terat.....

Asalam aleikum/Bwana Yesu asifiwe/Endasupai engaji e maa/ Airoroki ndai laisho pookin/habari za muda na wakati huu wadau wote wa maendeleo Terat.

Ni takribani muda kidogo sasa nimekuwa kimya kutoa mawazo yangu juu ya shughuli mbalimbali za kujenga na kukuza uchumi wa jamii na jamaa zetu wa Terat. Hii inatokana na kutingwa kwa majukumu ya kulitumikia taifa langu kwa faida ya vizazi vijavyo....

Tuesday, July 29, 2014

Kwa wanafunzi..............

Habari za muda na wakati huu, nimepata meseji na simu nyingi kutoka kwa wanafunzi wakitaka kupata ufafanuzi zaidi juu ya makala zangu mbili nilizoandika siku kazaa zilizopita zikijinasibu kwa jina la "namna mwanafunzi anaweza kusoma kwa mafanikio". Kutokana na ufinyu wa muda, sitoweza kujibu meseji ya kila mtu na vile vile kumpigia simu atakayenibipu ila ukisoma vizuri kama kuna sehemu utahitaji msaada zaidi nipigie simu na usitume meseji ama kunipibu.

Tuesday, May 27, 2014

SAUTI YA VIJANA TANZANIA- MAAZIMISHO YA SIKU YA UKOMBOZI WA AFRIKA 25/05/2014

UCHUUZI- AFRIKA KATIKA AWAMU YA MAKUCHA YA UTANDAWAZI






UTANGULIZI
Awali ya yote nitangulize salamu zangu kwako wewe unayenisikiliza kwa namna ambavyo utaoona itakupendeza wewe. Iwe ni kwa mrengo wa imani yako, itikadi yako ama kulingana na umri wako, hapo ulipo salamu zangu zikufikie.
Pia nimshukuru mwenyezi Mungu aliyenijalia afya njema na kuendelea kunibariki kwa kila jambo ninalolitenda.

Friday, April 11, 2014

NINAPOKUMBUKA MIAKA KADHAA YA KUZALIWA.....

Maalumu kwa mama yangu.
Ilikuwa tarehe 12th April 198…, saa mbili usiku jijini Arusha, ilikuwa siku ambayo familia ya Mesaya Simanga Masakoi na Tiinoi Mashon Kivuyo (Mr & Mrs Mesaya) walipotunukiwa na Mungu zawadi ya mtoto wa kiume. Najaribu kuvuta hisia zangu juu ya furaha waliokuwa nao vijana hawa wa enzi zile kwa kufanikiwa kumpata mtoto mwenye afya njema na ambaye alipofinywa kwenye kisigino cha mguu wake alilia mara tatu kuonyesha kwamba ni mwanaume rijali.

Sunday, April 6, 2014

Fukununu, makala muhimu sana kwenu wana-UDSM

CHUO KIKUU KIMEGEUKA CHOO KIKUU
Yapata miaka zaidi ya miaka miwili (2) toka makala hii iliyoshika kasi na kupendeza machoni mwa wasomi wa CHUO KIKUU ilipopotea kwenye mbao za matangazo za Cafteria na Getini Mabibo Hostel. Kwa wale waliokuwa sehemu ya umajimui huu wa UDSM, makala ya mwisho ilitoka tarehe 17th December 2011 ikiwa na kichwa cha habari kilichonakshiwa kwa maneno ya MCHAWI HUYU HAPA.