Music

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Wednesday, May 1, 2013

KATI YA KATA ZENYE BARABARA ISIYOPITIKA KATIKA JIJI LA ARUSHA NI KATA YA TERRAT LAKINI CHA KUSHANGAZA DIWANI WAKE ANASISITIZA HAKUNA TATIZO LA BARABARA NA WANAODAI BARABARA NI GENGE LA VIJANA WAHUNI

Hii ni sehemu ya barabara kuu ya Terat iendayo kwenye shule pekee ya sekondari iliyopo kwenye kata hii..... Zaidi kata ina zahanati moja ya afya hali inayowafanya wakazi wengi kusafiri zaidi ya KM 20 kufuata huduma hii ya afya....

Endelea kufuatilia habari hii upate mengi usiyoyajua kuhusu kata hii iliyopo ndani ya jiji la kitalii la Arusha na inayotoa moram nzuri ya kutengenezea barabara ambayo ndio inayotumika jijini hapa....

TAFAKURI YANGU
Na mwandishi wetu,
Asalam aleykkum, Tumsifu Yesu kristo ndugu zako wakazi wa Terat na wanaumajimui wa jamvi hili. Nisisahau kusalimia kulingana na umri na rika, airoroki ndai loo akwi, airoroki ndai loo papa, endasupai lepaiyani naidipaki aajo endasupai le muran??? Wooj!!!! Esamiakaki taa noo yeiyo aamu ituarikino ndai, Endakwenye noo koko oo noo yeiyo??? Marikino siake selengen, Endasupai indoiye????
Wanawanchi kama nilivyo ahidi awali kwamba kila siku za Jumanne na Ijumaa nitakuwa nawaletea mfululizo wa elimu yangu juu ya mambo mbalimbali yanayozunguka jamii kisiasa, kijamii na kiuchumi. Leo nafungua ukurasa kwa kuanza na makala hii ambayo naamini itatoa darasa la kutosha kwa wanajamvi wenzangu. Makala hii itakwenda kwa jina la TAFAKURI YANGU, ikiwa na manna ya mawazo yangu (my thought, meditation).
Tafakuri la leo linatanabaisha juu ya MAPATO YA SERIKALI ZA MITAA/VIJIJI. Ungana na mwanatafakuri wetu ili uweze kupata elimu hii ya bure ambayo haitozwi ada wala hela ya dawati.
1.  Mapato yanayotokana na shughuli za kibiashara na viwanda zinazomilikiwa na na au huduma zinazotolewa na mtaa/kijiji.
2.  Fedha zinazotokana na leseni, vibali, ada na ushuru ulioainishwa katika sheria ndogo zinazotungwa na halmashauri ya kijiji/mtaa.
3.  Fedha zinazotokana na upangishaji wa majengo ya halmashauri ya kijiji/mtaa.
4.  Fedha itokanayo na mikopo ambayo halmashauri ya kijiji/mtaa imepata kutoka taasisi zinazokopesha fedha au kutoka mahali pengine.
5.  Mapato ya halmashauri ya kijiji/mtaa kutoka kwa mtu au taasisi ya umma au serikali au halmashauri ya wilaya au ya mji kama mchango, ruzuku, fidia au namna nyingine yoyote.
6.  Fedha inayotokana na sheria ya kodi ya burudani inayokusanywa ndani ya eneo la kijiji/mtaa (sheria Na.21 ya 1970)
7.  Kodi inayolipwa na kukusanywa ndani ya eneo la kijiji/mtaa kutokana na wenye nyuma za wageni.
8.  Ushuru unaotozwa kutokana na sheria ndogo ya kijiji/mtaa kwa biashara za rejareja, usagaji na ukoboaji wa nafaka, uuzaji wa mkaa, mbao na bucha zilizo ndani ya eneo la kijiji/mtaa na katika miji midogo ya biashara:
a)   Biashara ya rejareja                 Tsh 15,000 kwa mwaka
b)  Mashine za kusaga unga          Tsh 20,000 kwa mwaka
c)   Mashine za kukoboa                Tsh 15,000 kwa mwaka
d)  Biashara ya mkaa                     Tsh 15,000 kwa mwaka
e)   Biashara ya kuuza mbao         Tsh 20,000 kwa mwaka
f)    Bucha                                      Tsh 10,000 kwa mwaka
9.  Mapato mengine yoyote halali yanayopatikana kwa njia nyingine.
10.              Fedha atakayotozwa mtu yeyote kama faini ya kuvunja sheria ndogo ya kijiji/mtaa.
11.              Kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya vijiji (Na.5 ya 1999 kifungu cha 18(1)(f) Halmashauri ya kijiji/mtaa kinaweza kutoza wanakijiji ada ya mwaka ya hakimiliki za kimila za ardhi yao.
12.              Chanzo kingine cha mapato ya serikali za vijiji/mitaa kinatokana na kanuni za serikali za mitaa za taratibu za ukusanyaji wa kodi (GN No. 346/87). Kanuni hizi zinateua serikali za vijiji kuwa wakala wa halmashauri ya wilaya/miji na kuagiza halmashauri ya wilaya/miji kulipa halmashauri ya kijiji/mtaa asilimia 17 au zaidi ya fedha zilizo kusanywa na serikali ya kijiji/mtaa na kumlipa mwenyekiti wa kitongoji 3% ya fedha alizokusanya.
Je, Kati ya vyanzo vyote hivi ni vipi vipo kwenye kata yetu ya terat na vinanufaishaje kata yetu???
Asanteni na tukutane tena jumanne ijayo..
Cont: 0712 814 285