Music

Saturday, July 20, 2013

HUYU NDIYE ALIYETUNGA JINA TANZANIA

Kwa muda mrefu sana watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni nini hasa asili ya jina la Tanzania na majibu yao yamekuwa magumu kupatikana hasa kutokana na uwazi wa historia ya jina hilo kutowekwa bayana na serikali na hata katika maadhimisho yake ya sikukuu za muungano jina hili limekuwa halitajwi ni wapi lilipotokea licha ya kuambiwa kuwa TANZANIA ni muunganikoa 
wa nchi mbili ambazo ni Yanganyika na Zanzibar lakini ni nani hasa aliekaa chini na kubuni jina hili au nini maana halisi ya jina Tanzania,hii bado imekuwa ngumu kwa watazania wengi kupatajibu.
Ikumbukwe kwamba jina Tanzania linakuwa halina maana halisi ya moja kwa moja licha ya kwamba ni jina la muungano wa nchi mbili,jina lililotokea baada ya nchi hizi mbili kuungana.
Baada ya nchi nyingi za kiaafrika kupata uhuru,kunako miaka ya sitini baadhi yao zilibadili majina na kuiita majina mapya,kwa mfano:nchi ya Malawi ilibadilishwa jina lake mwaka 1964 na kuitwa malawi badala ya nyasa land,nchi ya Sudan france ilibadilishwa jina mwaka na ikaitwa Mali mwaka 1960, na nchi nyingine kibao ziliweza kubadilishwa majina kutokana na sababu mbalimbali.
Hivyo haikuwa jambo la ajabu pale muungano wa nchi hizi ulipoitwa Tanzania.
Kwa wanahistoria wa Tanzania jina la Muhhamadi Iqbqli Dar siyo jina geni kwao.
Kwani huyu ni mtoto Daktari maarufualikuwa akiishi mjini Morogoro kunako miaka ya 1963.
Muhhamadi Iqbali Dar ndie aliebuni jina la Tanzania baada ya kuona tangazo katika gazeti la THE STANDARD ambako aliona tangazo la kubuniwa kwa jina muungano na wakati huo bwana huyu alikuwa ni mwanafunzi katika sekondari ya mzumbe ya morogoro.
Baada ya kuona tangzo hilo kijana huyo aliiamua na yeye kukaa chini ili kujaribu kuunda jina ambalo ataon yeye kuwa linafaa kutumika kama jina la muungano.
Kwanza kabisa alikaa chini na kwa mujibu wa mafundi ya dini ya kiislamu kuwa mtu unapotaka kufanya kitu ni sharti uanze na jina BISMILAHI,basi ndivyo bwana huyo alivyofanya,kwa aliandika neno BISMILAH na baadae alichukua herufi tatu za mwanzo katika jina Tanganyika na kupata neno TAN kisha akachukua herufi tatu katika jina la Zanzibar yaani ZAN na kuziungani kwa pamoja na herufi tatu katika jina la Tanganyika na hapo alipata neno TANZAN,Baada ya kupata jina hili aliamua kulitaja mara nyingi nyingi na kuona kuwa jina hili linakuwa halivutii sana mdomoni na ndipo alipoamua kuoneza herufi I kutoka katika jina lake na kuoongeza harufi A kutoka katika dhehebu lake la ahmadiya na alipoziunganisha pamoja alipata neno TANZANIA. Alituma jina hilo kwa serikali ya jamuhuri ya Tanganyika na muda siyo mrefu baba yake alipokea barua nzito kutoka serikalini ikimtaja Muhamadi Iqbal Dar kuwa ndie mshindii wa kubuni jina la muungano(Tanzania).
Katika barua hiyo ilimtaja Muhamadi Iqbali Dar kuwa ndie mshinde na atapatiwa zawadi ya shilingi mia mbili ambayo atagawana wenzake wengine ambao nao pia waliweza kubuni jina kama hilo,kalini katika barua hiyo licha ya Muhamadi Dar kutajwa kama mshindi na kupewa fungu lake,washindi wengine hawakutajwa.
Barua hiyo ilisainiwa na Idrisa Abdul Wakil ambae kwa wakati huo alikuwa waziri wa habari na utalii.
Mpaka muda huu histori ya jina hili imekuwa ikiweka kapuni bila ya kutajwa hali ya kuwa ni muhimu sana kwa watanzania.
Unaweza pia kusoma kitabu kimoja kilichoandikwa na M.H:Mubiru juu ya kubuniwa kwa jina hili,kitabu hicho kinajulikana kwa jina la NANI ALOBUNI JINA TANZANIA,ni kitabu kinachopatikana kwa gharama nafuu kabisa na pia nimekuwa nikikiona mara nyingi katika maonyesho ya nane mkoani Arusha

0 comments:

Post a Comment