Fikiri kwa makini juu ya tafakuri hii...............
Neno
likishanenwa mnenaji hutegemea kupata mawazo zaidi kutoka kwa hadhira na
hadhira hutegemea kutumia ama kurudufisha kwenye shuguli za kila siku.
Leo nawatunuku maneno haya ili kila mmoja ayafanyie utafakuri kama yana mchango kwa maendeleo ya nchi yetu na jamii yetu kwa ujumla.
1. Ili kushusha gharama za usafirishaji, usafiri wa treni upewe kipao mbele. Kwa kuwa serikali imeshindwa kufufua usafiri wa treni, tufunguwe milango kwa makampuni binafsi kuwekeza kwenye hili. Masharti ya uwekezaji:
i. Mwekezaji atarekebisha njia zote za treni
ii. Mwekezaji anatakiwa kuwa na wafanyakazi watanzania zaidi ya 75%
iii. Mwekezaji atatakiwa kuleta vichwa vya treni kwa garama zake/ kuruhusu ubia na wawekezaji wengine
iv. Bei ya usafiri na usafirishaji kwa njia hii utasimamiwa na serikal
v. Mwekezaji atapewa tax holiday ya miaka 5, kama kampuni inafanya vizuri kama ilivyopangwa na serikali
vi. Mwekezaji atafungiwa na kufilisiwa mara moja kama atashindwa kutimiza masharti ama atashindwa kufanikisha malengo atakayopewa na serikali ndani ya siku 365
vii. Ni marufuku wa watumishi wa umma kuwa na ubia na makampuni haya
2. Ili kupunguza gharama za uzalishaji, serikali iruhusu uwekezaji binafsi kwenye nishati ya umeme na TANESCO ibaki kama chombo cha kusimamia na kuratibu kama ilivyo TCRA. Masharti yawe:
i. Ni marufuku kwa mwekezaji kutoa/kuuza nishati nje ya nchi
ii. Mwekezaji atatakiwa kuwekeza na kuuza bidhaa yake (nishati ya umeme) kwa watanzania wote wa mijini na vijijini kwa bei nafuu
iii. Hakutakuwa na ruhusu kwa mwekezaji mmoja kuwekeza kwenye chanzo zaidi ya kimoja, mf maji, gesi, nyukilia, mawimbi etc
iv. Ni marufuku kwa mwekezaji kuhamisha rasilimali ya uzalishaji kutoka sehemu moja na kuipeleka kwingine kwa uzalishaji wa nishati, mf ni marukufu kutoa gesi Mtwara na kuipeleka Dar ama Bagamoyo bali utajenga kinu cha uzalishaji wa nishati mtwara na kitakachotoka mtwara ni nishati ya umeme
v. Bei ya kuuzia nishati itasimamiwa na serikali
vi. Wafanyakazi watatakiwa kuwa zaidi ya 75% ni watanzania
vii. Mwekezaji atakayesambaza huduma yake vijijini hatatozwa kodi
viii. Kila mwekezaji atapewa tax holiday ya miaka 5
3. Ili rasimali za asili zimnufaishe mtanzania, wawekezaji wote wa madini na rasilimali asili:
i. Ni marufuku kusafirisha rasilimali asili nje ya nchi bali atatakiwa kujenga viwanda mama ndani ya nchi na kitakachosafirishwa ni final goods/consumer goods
ii. Wafanyakazi wote kwenye kila idara wanatakiwa kuwa zaidi ya 75% wawe ni watanzani asili
iii. Rasilimali asili zilenge kunufaisha eneo ambapo rasilimali hiyo inapatikana, mf huduma za afya, elimu, umeme, maji nk ziboreshwe kwa ushirika wa mwekezaji na serikali
iv. Hakutakuwa na uwekezaji binafsi kwenye vivutio asili kama wanyamapori, milima, mabonde nk
v. Ni marufuku kwa mfanyakazi wa umma kuwa na ubia na mwekezaji
Nategemea mawazo yenu zaidi kwa hili la leo kabla sijaleta sehemu ya pili ya "NENO" langu.

Fanya tafakuri tunduizi...........
0 comments:
Post a Comment