Tunapenda kuchukua fulsa hii kwanzakuomba msamaha na kuwataka radhi wazazi wetu mliotutuma kwenda kutafuta Elimuvyuo vikuu hapa nchini kutokana na vurugu, migomo na maandamano ya mara kwamara ambayo mmekuwa mkiyasikia au mkiyaona kupitia vyombo vya habari katikavyuo mbalimbali hapa nchini, pia tunaomba radhi toka moyoni mwetu kwa walimuwetu (lecturers) kwa adha inayowakuta pale inapotokea migomo na maandamano. Piatunawaomba msamaha viongozi wetu wa dini ambao kwa namna moja ama nyinginewamekua wakitulea kiroho na kimaadili. Lakini tutakuwa hatujawatendea hakiwatanzania ambao kodi zao ndizo zinazogharamia Elimu yetu hapa chini, bilashaka walitegemea kutuona tukisoma kwa bidii na kufaulu vuzuri ili tutakaporudikatika jamii zetu tutumie elimutuliyoipata kuwakomboa watanzania wenzetu ambao mpaka sasa wanalia na kuangamiana vita kubwa ya UJINGA, UMASKINI, MARADHI NAUFISADI. Lakini wameendelea kushuhudia migomo na Maandamano ya Mara kwa Marayasiyo na kikomo. Baada ya kutafakari kwa kina kama wasomitukaona kama hatutakaa chini na kufanya utafiti wa kina (research) ya vyanzo nasababu zinazotufanya tuwe na migomo, tuandamane na kufanya vurugu za mara kwamara vyuoni. hatutaeleweka na tutaonekana kweli sisi ni wahuni, au tunatumiwana watu ama wanasiasa wakati hizi nituhuma ambazo hazina ukweli hata chembe ndani yake, Lakini tunapenda kuwataarifu viongozi wetu,wazazi na watanzania kwa ujumla kwamba matatizo haya yanatokana na vitendovichafu vya baadhi ya watumishi pamoja na sera mbovu za kiukandamizaji, kibaguzi, manyanyaso na uonevuuliovuka mipaka kwa wanafunzi wa Elimu ya juu (vyuo vikuu). Na hatutaelewekakwa walimu wetu waliojitolea kwa uzalendo wao wa hali ya juu kutufundisha japomaslahi yao ni madogo ukilinganisha na kazi kubwa wanayoifanya, Pia kama tungekaa kimyaviongozi wetu wa dini ambao ni walezi wetu wa roho na maadiliwasingeuelewa. vilevile hatutaelewekazaidi kwa watanzani ambao wanatozwakodi kwa ajira ya kugharamia elimu yetu ya juu ili tusome kwa bidii iliturudi kulitumikia taifa. Tumefanya utafiti huu wa migomo, vurugu namaandamano ya mara kwa mara ili tutoe taarifa ya upande wa pili wa wanafunzi kwanikumekuwa na desturi au utamaduni wa vyuo kutoa taarifa zisizokuwa na ukweli kwa wananchi(umma) kwa kuwasingizia wanafunzi kwamba wanatumiwa na viongozi wasiasa kufanya fujo, vurugu na migomo pindimatatizo haya yanapojitokeza,
Taarifa hizi zisizokuwa na ukwelizimekuwa zikitolewa na baadhi ya watawala wa vyuo ili kukwepa kutekereza madaiyetu ya msingi kwa kisingizio hiki kisicho na ukweli ndani yake hata chembekama ilivyonekana katika gazeti la mtanzania ISSN 0856 - 5678 toleo namba na5842 Jumapili Januari 15 2012 makala ya13 yenye kichwa cha habari kilichoandikwa kwa herufi kubwa na kusomeka hivi VURUGU UDSM. Uongozi wa chuo wadaiwaliofukuzwa ni wanasiasa pia habari kama hiyo ilichapishwa katika gazeti lauhuru ilisomeka hivi katika ya kwanza ya gazeti hilo VURUGU ZA UDSM: CHAMA CHA(……..) CHA SHUKIWA KUWA NYUMA YA MGOMO. ukweli wabainika nalo gazeti la mzalendojumapili 15 January 2012 makala ya 7 ilikua na habari kama hizo. Kwa bahati Mbaya kwa upande wawanafunzi hatukupata nafasi ya kukanusha madai hayo kwa ushaidi wa wazi kwa wazazi wetu, walimu wetu, viongozi wetuwa dini, na watanzania waliolipa kodi zinazotusomesha wakaamini madaiyaliotolewa na serikali na utawala chuo kuwa ni sahihi. Wakatuhukumu na kuwafukuzwa chuo wenzetu kwa kutuhusisha kutumiwa na vyama vya siasakitendo ambacho si kweli. Ili kukwepa na kupinga hoja na madai yetu ya msingikwa majibu mepesi eti tumetumwa ni ajabu kweli! Namna hii siasa zinaingizwa katikachuo matokeo yake chuo kinakuwa sehemu ya kisiasa jambo ambalo si sahihi chuoni taasisi inayojitegemea inapaswa kuendesha mambo yake bila kuingiliwa nataasisi nyingine. Hali hii ikiachwa iendelee kamaserikali haitatekeleza mapendekezo yetu ambayo ni njia sahihi ya kupunguzavurugu migomo na maandamano vyuo vikuu nchini kama sio kumaliza kabisa tutaombawazazi wetu, walimu wetu, na watanzania walipa kodi mtuelewe kwa maamuzi magumututakayo yachukua kama itakavyoonekana inafaa. Lakini vyuo vikuu vitapoteza sifa yakeya ndani na nje ya nchi. Vitabaki ni vyuo vya migogoro ya migomo, vurugu namaandamano miaka nenda rudi. Na kufukuza wanafunzi sio mwarobaini watatizo kwani maandamano, vulugu, migomo itaendelea kuwepo. Iwapo madai namahitaji ya wanafunzi hayatatekezwa pia. Yapomadhara makubwa ambayo anatokana na migomo vyuoni ikiwemo kuharibika rasilimaliza chuo, kuharibu ratiba za masomo, Serikali inaingia hasara na gharama zaziada chuo kinapofungwa kwa mgomo. Kwani bajeti ya chuo inakua Ishapitishwapia na gharama za kupeleka polisi na magari ya maji ya kuwasha na mabomu yamachozi n.k. Mbayazaidi ni kwa wanafunzi kufukuzwa na kusimamishwa masomo ambao wamegharimiwa na kodi za watanzania wakitarajiwa kuhitimu na kurejesha mkopo na kulitumikia taifa letu. Tunaomba wazazi wetu, walimu wetu,viongozi wetu wa dini na watanzaniawalipa kodi. Kwa pamoja mtumie fursa hii kuishauli serikali kutekelezamapendekezo yetu ili kuinusuru sekta mama ya elimu nchini isiyumbe nakuporomoka kwa kasi ya ajabu. Ni matumaini yetu kila kundi litatumianafasi yake kuishauli serikali kupeleka mapendekezo yetu Inshallah. Ili binaadamu aweze kuzikabili changamoto zamaisha na kujikomboa katika lindi la umaskini, lazima awe na elimu. Elimu ndio msingi wa kujitambua,kuyatawala na kuyatumia mazingira anayoishi binadamu ili kuboresha maisha yakena kujiletea maendeleo ya haraka, ni wazi kuwa elimu ndiyo ukombozi wa binadamukuiona kesho iliyo bora zaidi na kuogelea katika bahari ya utandawazi ambayoinamtaka kila mmoja, aogelee kwa namna awezavyo. Kwa kutambua ukweli huoSerikali ya Tanzania imetoa fursa kwa wadau wa elimu kuwekeza katika sekta hiyoili kujenga taifa la watu wenye Maarifa, ujuzi na uwezo wa kuzalisha. Diraya Taifa ya Maendeleo ya 2025, Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA) pamoja na sera ya Elimu namafunzo, zote zinaeleza umuhimu wa elimu ili kuiwezesha nchi kusonga mbele. watanzaniana wazazi kwa ujumla wanatarajia kuona watoto wao wanapata Maarifa uwezo iliwachangie juhudi za watanzania na wazazi wao kutatua changamoto zilizopo katikajamii. Wanafunzi wenye Maarifa naujuzi huwa na uwezo wa kufanya mambo mengi mapya kwa usahihi na kuwaongozawenzao. Katika maendeleo ya ukwelikatika jamiitunayoishi, Matendo ya wasomi, kazi zao, majukumu yao na shughuli mbalimbali wanazofanyazinapaswa kuthihirisha matunda ya elimu waliyonayo. Zao muhimu la elimu kwa mtoto ni kuwa nauwezo mkubwa wa kufikiri kwa makini . Uwezo huu ndio unahitajika sana katika jamii ya leo. Mtu mwenye uwezo wa kufikiri ndiye Mwenyenguvu ya kuibua dhana mpya na kutafuta njia mbadala za kutatua matatizo. watu walioibua teknolojia tulizonazo,waliongozwa na upeo wa kufikiri ndipo wakaibuka na dhana mpya. Tendo la kufikiri lipo ndani ya akili nautashi wa mtu bila kufikiri matokeo ya juhudi za mtu mara nyingi huwa anguka auhasara. Serikali pamoja na wadau waelimu nchini. Wanamchango mkubwa wakuibua taifa la wasomi na kutekeleza Dira ya Taifa ya maendeleo ya 2025,mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA) pamoja na sera ya Elimu na mafunzo ambazo zote zinaelezaumuhimu wa elimu ili kuiwezesha nchi kusonga mbele. “Kukua kwa uchumi pamoja na mambo menginehutegemea uwekezaji hasa wenye manufaa kama elimu ili kupata wataalamu ambaondiyo watainua uchumi wetu, kimsingi uchumi hauwezi kukua bila wasomi’, Nchilazima iandae rasilimali watu ambao wanaitajika ili kuinua uchumi wa nchiyetu. Na kusaidia familia zao. Maskini. Rais wa kwanza wa Tanganyika kwa sasaTanzania aliwahi kusema maneno yafuatayo katika hotuba zake kwa wananchi kwamba. Hakunaserikali yoyote duniani inayowawekea wananchi wake hela mfukoni bali “the onlybest way to enrich a poor people is to educate their children”. Yaani njia pekee ya kuwasaidia wananchimaskini ni serikali kuwasomeshea watoto wao. Hii alikusudia kwamba ukimsomesha mtoto wa maskini atakapopata hiyoelimu ataitumia kuinua familia yake kiuchumi na Taifa kwa ujumla. Na ndiyo maana baada ya kupata uhuruTanganyika, hayati Mwalimu Julius Nyerere alitambua maadui watatu MARADHI,UMASKINI na UJINGA. Lakini ili ukabiliane na maadui hawa lazimauanze na Adui ujinga kwa kutoa elimu bora kwa wananchi ili waondoe umaskini namaradhi. Lakini tume Shuhudia Serikalikwa sasa inavyo suasua katika sekta hii muhimu ya Elimu nchini. Nakatika katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 9 kifungu kidogo cha(i) inasema hivi 9 (i) “Kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazomaendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondoshaumaskini, ujinga na maradhi; Baada ya Uhuru wa Tanganyikamwaka 1961, na baadae Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – Tanzania Mwaka 1964,Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, alitangaza vita kwa maadui watatu,Ujinga, Maradhi na Umasikini. Mwalimu alihakikisha anafanikiwa katikaMapambano hayo. Alianza kuweka mikakatimbalimbali ikiwa ni pamoja na kukazia elimu ili kufuta ujinga, kupatikana madaktariwa kupambana na adui maradhi na wataalamu wa uchumi wa kupambana na aduiumasikini. Fikra hii ya Mwalimu ilidumuhadi kufikia maziko ya AZIMIO LA ARUSHAna kuanzishwa AZIMIO La Zanzibar –Februari 1991. ambalo liliamua kufuataMfumo wa kibepari ambayo ilikusudia kumilikisha rasilimali ya Tanzania kwawachache “Matajiri”. Baada ya hapo, Maadui hawa kukaa mbali waliwavamia Watanzania. Ujinga ulianza kuongezeka (idadi ya watuwasiojua kusoma na kuandika iliongezeka), maradhi yakaongezeka vifo kwa mama namtoto, Uchumi ukadorora, umaskini ukaongezeka, shillingi ya Tanzania ikashukathamani siku hadi siku huku mfumuko wa bei ya bidhaa ikiwaumiza wananchi wakipato cha chini. Hilo ndilo Azimio laZanzibar. Elimu ya Tanzaniahaijulikani iko wapi, mpasuko mkubwa baina ya watoto wa maskini na matajirikatika nyanja ya elimu imeongezeka. Shule za kimataifa (International Schools) zinafundisha masomo yote kwakingereza wakati shule za akina kayumba zinafundisha masomo yote kwa lugha yaKiswahili. Matajiri wanafanya kufuru kwa kuwalipia watoto wao ada katika shule zamsingi inayolipwa na mtoto wa maskini katika vyuo vikuu, la ajabu kama si kushangaza akimalizaanaungana naye kutafuta mkopo, na cha ajabu anapewa kwa sababu ni mtoto wakiongozi Fulani au tajiri Fulani, mtoto wa Maskini anarejeshwa nyumbani etihajatimiza masharti na vigezo. Kama wameamua kujitengakwa sababu ya fedha walizonazo, kwa nini wasiundiwe vyuo vyao na balaza lao lamitihani? Kwa nini wanafanya mtihani wa taifa ule ule kwa siku moja katikalugha mbili fofauti? Hii si mikakati ya mafisadi kuhakikisha kuwa madaraka yanchi hii yanabaki kuwa ya kuridhishana kwa sababu ya watoto wao kuwa na elimunzuri? Kwa nini elimu ya msingi katika nchi moja huru ifundishwe kwa lughambili tofauti tena chini ya wizara moja? Wakulima wanadanganywa kwakuwekewa Shule za Sekondari za kata ambazo hata mtoto wa Diwani au Mratibu elimu wa kata, hasomikule shule haina walimu wa kutosha, Vitabu, nyumba vya madarasa havitoshi,uwiano mbaya wa vitabu kwa kila mwanafunzi, mrundikano wa wanafunzi darasamoja, uhaba wa nyumba za walimu.wakati wengine wanabebwa kwa magari na kusoma katika vyumba vyenye viyoyozi,walimu wenye uwezo mzuri wa kufundisha na vitabu hali hii si kujenga chuki kwajamii? Kama kweli dhamira ya kujenga utitiri wa Shuleza Sekondari za kata ni kuinua elimu ya Tanzania ni kwa nini hakuna hata watotowa viongozi yeyote wanaosoma katika shule hizi? Hii si sababu tosha ya shulehizi kukosa usimamizi mzuri, Enzi ya Baba wa Taifa, watoto wa watanzania ambaoni viongozi sasa. Walikuwa wanasomapamoja, wanafanya mtihani mmoja, wanafundishwa kwa lugha moja, wanachaguliwa nakuwa katika sekondari moja, wanaishi kwa pamoja wakishirikiana katika kilajambo, sasa ni ubaguzi mtindo mmoja. Ukipita karibu na shulehizi za serikali utakutana na vibao vya wakina Pwagu na Pwaguzi, vibao vyenyekauli mbiu tata, za uongo mtupu, “Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi” Ingiandani ya shule hizo au madarasani uonemadudu yaliyomo kule. Ni kweli katikashule zile zinafundisha Ufundi au kunafundishwa Ufundi ?Kunahaja gani ya kutangaza biashara usioifanya ? Ni ufundi gani unafundishwa katikashule hizi za msingi? Wanamfurahisha nani katika Matangazo hayo? Watanzaniawanapumbazwa kwa sababu ya maradhi,ujinga na umaskini uliopaliliwa na Azimio la Zanzibar. La kujiuliza na kushangazakatika shule hizi zote za msingi za serikali ambazo vibao hivi vimekuwa nisehemu ya urembo, barabarani, hakuna hata Mwalimu aliyepewa hata kozi ya elimuya ufundi ili aweze kuwafundisha wanafunzi japo kwa kubabaisha ni ajabu sana! Sera ya elimu ya kimataifainaeleza kuwa ni wanafunzi 45 katika kila chumba cha darasa, watanzania kwakuchakachua ni jadi yao mpaka wanapiganana wataalamu wa kimataifa. Ilimradi turuzuku imeongewa katika wilaya ufisadi ufanyike.Inafahamikakuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi hutoa ruzuku kufuatana na wingi wawanafunzi katika wilaya husika.Hivyokinachosababisha wanafunzi kujazwa darasani katika chumba ambacho kinapaswakuchukua Watoto 45 ni uongozi wa elimu wa wilaya zao maafisa elimu wa wilayawanashinikiza wanafunzi waandikishwe wengi ili kupata ruzuku iliyo kubwa wapatecha kugawana.Seraya Tanzania ya elimu ni watoto wote wapate elimu, lakini Je? Ni katika matesokama haya ya kurundikwa katika chumba kimoja watoto zaidi ya 100? Walimu na hasa wanaofundishashule za vijijini wanalalamika kuwa wanapewa mzigo mkubwa katika kufundisha,kwa sababu ya wanafunzi kuwa wengi na miundombinu finyu, uhaba wa walimu hadiwanashindwa hata kupumua, lakini pamoja na walimu hawa kulalamika kwa niniwanashindwa kutii sheria hii ya kimataifa ya wanafunzi 45 kwa chumba kimoja? Ukalimu wa walimu na uwoga wawalimu unatufikisha pabaya sasa wanazalisha taifa la wasiojua kusoma nakuandika kwa sababu ya uzembe wa Serikali.TuangalieElimu ya juu. Vyuo vikuu serikali inamkakati gani wa kumaliza migogoro na vurugu zilizopo katika Elimu ya juu yamara kwa mara yakiwepo maandamano. Yasiyo isha. Japo hata kipindi cha nyuma migomo hasa chuo kikuu cha Dares Salaam ilikuwa inatokea lakini sio kama ilivyo kwa sasa. Na migomoya wakati wa kipindi cha awamu ya kwanza na pili ilikuwa ya kupinga seratofauti na migomo na maandamano yasasaya kupinga matokeo ya sera mbovu. Nikweli wanafunzi wa vyuo vikuu leo hii wamekuwa na madai ya msingi kwa serikalihivyo kutokana na viongozi kutokuwa na utamaduni wa kukutana nao mapema kujuamatatizo yao wanafunzi hulazimika kutumia njia ya kuandamana na kugomakufikisha ujumbe wao kwa njia ya mgomo au maandamano kwa viongoziserikalini. ebu tuone baadhi ya migomo, vyuo vikuu nchini
HALI YA ELIMU KATIKA MIAKA 50 UHURU WATANZANIA (1961 - 2012) I. VUGUVUGU LAUJENZI WA SHULE NA VYUO VIKUU NA MATATIZO YAKE.
1. Nikiangalia matatizo yanayoikabili sekta ya elimunchini, machozi humilengalenga hasa kutokana na kutambua ukweli kuwa ubora waTaifa lolote lile hutegemea na ubora wa elimu itolewayo kwa watu wake. Maanayake ni kwamba, Watanzania tukitaka kuharibu ubora wa Taifa, letu njia nyepesini kuua au kuharibu misingi ya kupatia na kutolea elimu bora. Kwa hiyoWatanzania tukikiuka misingi ya kutolea na kupatia elimu bora misingi hiyoitatukiuka. Leo hiiElimu Tanzania imekuwa ya kufanyiwa majaribio kila mara na viongozi wetu awamuya Rais wa kwanza ilijitahidi kwa kadri ya uwezo wake katika sekta ya Elimukwani aliamini ndiyo sekta pekee ambayo ingeweza kutatua adui wengine wawiliujinga, maradhi na umaskini kama alivyobainisha. Baada ya nchi yetu kupatauhuru 1961 watanzania asilimia kubwawalikuwa hawajasoma. Serikali yake ikaleta Mfano wa Elimu ya watu wazima. Mwalimu Julius Nyerere Alisema: “ Elimusiyo miujiza fulani unaotokeadarasani tu. ni kujifunza kutoka kwa wengine na kujifunzakutokana na mafanikio na makosa yetu wenyewe ya siku zilizopita”Mwalimu alisema Mwaka huu wa 1970 ni muhimu nguvuzikaelekezwakuwaelimishaw ananchi na hasa watu wazima ili kutimiza ahadi za TANU. Alisema hiyo inasema “Nitajielimisha kadri ya uwezowangu wote na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote. Katika salamu zamwaka mpya zilizo tangazwa kwa njia ya redio, Mwalimu alisema kuwa ingawawaanzania wengi wanazungumza sana habariya Elimu ya watu wazima. “kamati kuu yaTANU sasa imeamua kwamba lazima tufanye kazi hiyo katika mwaka 1970 Miezi 12ijayo lazima iwe na lengo la kuwaelimisha watu wazima” alisema. Mwalimu aliendelea“sisi ni maskini na tuko nyuma na watu wengi mno miongoni mwetu wanaikanilihali tuliyonayo kama kwambwa ni amri ya Mungu na wanadamu kuwa hatuna lakufanya kuondoa hali hiyo. Shahada yakwanza ya Elimu ya watu wazima alisisitiza Mwalimu., lazima iwe Elimu yakujiondoa katika kuikubali hali ya maisha ambayo watu wa Tanzania wameishikarne nyingi zilizopita. Alisemawatanzania hawana budi kufahamu kwamba si lazima waishi katika vibanda vibovu,au walime kwa vijembe vibovu na katika hali ya udhaifu wa Afya, bali hawanabudi kutambua wanaweza kuyakabili mambo hayo. Kazi ya kwanzaya Elimu ya watu wazima itakuwa kuwafanya wakatae vitu hivyo na kwamba wanauwezo wa kupata nyumba nzuri zaidi, vyombo vizuri ya zaidi vya kufanyia kazi naafya nzuri zaidi. Shahada ya piliya Elimu ya watu wazima ni jinsi ya kujifunza jinsi ya kuyabadili maisha nahivyo hawana budi kujifunza jinsi ya kuongeza mazao katika mashamba katikaviwanda na kwenye ofisi zao. Mwalimualiongeza, watanzania hawana budi kujifunza habari za mipango ya maendeleo yauchumi ili waweze kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa muda mrefu serikali nawadau wa masuala ya elimu wamekuwa wanatafuta sababu ya wanafunzi kufanya vibaya katikamitihani ya kidato cha nne kutokana na ukubwa wa tatizo hilo serikali iliamuakufanya uchunguzi na kubaini mojawapo ya sababu za ufaulu duni kwa wanafunzi hasa kidato cha nne nikushushwa hadhi kwa mitihani ya kidato cha pili. Mtihani huo wataifa wa kidato cha pili ulianzishwa mwaka 1984 kwa lengo la kutathiminimaendeleo ya wanafunzi, baada ya miaka miwili ya masomo shuleni ambapoaliyeshindwa kufikisha alama zilizowekwa alirudia darasa. Hata hivyo 2008, serikali ilitamkawanafunzi ambao hawatapata asilimia 30 ya alama katika mtihani huo. Hawatarudiadarasa ila wataendelea na masomo ya kidato cha tatu na kupatiwa mafunzorekebisho. Ni kweli uamuzi wa kurudisha makali ya mtihani wa kidato cha pili niwa msingi kwa kuwa unawapa wanafunzi sababu ya kusoma. Hata hivyo tatizo lililopo katika mfumo wa elimuTanzania ni mchanganyiko wa uamuzi. Wakati ule ambapo mungai Joseph Mungai,akiwa waziri wa Elimu, alifuta masomo ya biashara shuleni, athari zakezinaonekana sasa hivi kwa wanafunzi wanaokuja vyuo vikuu. Yale masomo yalikuwa yanamwandaa mwanafunzikwa masomo ya chuo kikuu sasa mtu anakuja akiwa hana maandaizi ya awali, hilini tatizo. Mgongano wa uamuzi kama huo. Ndiyo pia uliofanya kufutwa kwa mtihanikwa kidato cha pili na matokeo yake wanafunzi wakawa wanaona hakuna sababu yakusoma. Lakini kuhusu suala la kuwatoa kwenye mfumorasmi wa elimu wale watakao kariri darasa mara moja na kushinwa kufaulu. Hilisio haki na tunaiomba serikali ibadili sera hii ya kuwaondoa wale wanafunziwatakao kariri darasa na kushindwa kufikisha asilimia 30 waruhusiwe kuendeleakukariri darasa mala mbili. Kwa sababu zifuatozo: i. Wale watoto ni wadogo sio vizuri kuwafukuza shulelakini wakiwa wanarudia darasa itawasaidia kujitahidi na kuhakikisha wanafanyavizuri. ii. Athari hii itawaathiri sana wanafunzi wa shule za kataambao hawana walimu wa kutosha, vitabu maabara na ukosefu wa maktaba. Wapimwesawa katika mtihani moja na wanafunzi wenye walimu bora,vitabu,maktaba, maabara na madarasaya kutosha watakuwa hawajatendewa hakikwa sera ya serikali ya kutaka waondolewe kwenye mfumo rasmi na kubaki tumtaani, itakuwa hawajawasaidia kw alolote lile, badala yake itakuwa ni mzigokwa serikali na jamii kwa ujumla. Na ikizingatiwa uhaba wa shule za ufundinchini.
1. SERIKALI HAIWATHAMINI WALIMU KAMA WAFANYA KAZI WENYETAALUMA. Leo hii serikali imewatekeleza walimuna haiwadhamini kama wafanya kazi wengine. Mwalimu ambaye ndiye Mwaaandaji wawataalamu wa fani zote. Kitu ambacho kimepelekea wanafunzi na jamii kwa ujumlakuiona siyo kazi ya maana. Huku serikali ikiwapumbaza walimu kwa maneno ya ualimu ni wito ili iwanyimehaki zao za msingi na wawe wepesi” kuvumilia shida kama ualimu ni wito na siyoTaaluma mbona kuna vyeti vinatolewa vya ualimu mbona kuna madaraja na ngazi zaualimu, hizi zote ni njia za Serikali za kuwapumbaza walimu ili isiwalipemishahara mizuri, nyumba nzuri za kuishi mafao yao mengine ya msingi. Leo hii ualimu umeonekana ni kazianayoichagua Mwanafunzi baada ya kukosa kazi zote au kufeli, kabisa na kukosasifa ya kusomea fani nyingine. Walimuwanaonekana kama wafanyakazi waliokata tama na kazi yao, wanaonekana wanyongehawako huru katika kazi yao (peace in mind) kutokana na sababu zifuatazo. i. Kucheleweshwa na kutopandishwa madaraja nawanapopandhishwa madaraja mishahara yao haipandishwi. ii. Mazingira magumu ya kazi kama nyumba hazina umeme, majina nyumba kuwa na hadhi ya chini/mbaya. iii. Umbali/mwendo wa muda mrefu kwend akazini/shulenihawana vyombo vya usafiri. iv. Kunyimwa na kuzungushwa kupewa ruhusa ya kwendakusoma/kujiendeleza kielimu. v. Idadi kubwa ya wanafunzi inayowaelemea kuhimilikuwafundisha. vi. Kutoshirikishwa katika ubadilishwaji wa mitaala marakwa mara. vii. Kupewa mishahara midogo na serikali ambao hauendani nahali halisi ya maisha ya sasa. viii. Kupangiwa vipindi vingi vya kufundisha shule nikutokana na uchache wa walimu shuleni. ix. Kudhalilishwa. Kwa kuadhibiwa na viongozi serikalinikama tulivyoshuhudia baadhi ya maeneo. x. Serikali kukataa kuwalipa malimbikizo yao ya mishaharakwa kisingizio cha kuhakiki majina uongo mtupu. Ni uhakiki gani huo usioishamuda wote.Leo hii walimu wameamua kujishughurisha na ujasiliamali wabiashara ndogo ndogo na kuamua kutangaza mgomo baridi ambao bado serikalihaijaushtukia yaani wanafika kazini kama kawaida lakini wanafanya kazi nchiniya viwango wanaingia darasani lakini hawafundishi kama inavyopaswa kujitolea. Mfano mwalimu Juma anayefundisha shule yaMtoto wa mkulima somo la Hisabati darasa la Tano lenye wanafunzi 120 atapatawapi muda wa kuelekeza kila Mwanafunzi aelewe (Individual) atapata wapi muda wakupitia madaftari ilihali anakipindi kingine darasa la NNe, pia anakipindi kingine darasa la sita chakiingeleza kwa siku na yote madarasa yana zaidi ya wanafunzi 100 kila darasa. Matokeo yake leo hii tunashuhudia Maelfu yawanafunzi shule za msingi wakimaliza darasa la saba hawajui kusoma na kuandikahuku kidato cha NNe na sita wakiambulia daraja la mwisho (division iv na zero) Na serikali ikishindilia kabisakudidimiza Elimu nchini kwa kuchukua wale wanafunzi waliofeli au waliofanyavibaya katika mitihani yao ya Taifa eti ndiyo wasomee ualimu ili wawe waalimu.Labda ndiyo Maana haiwadhamini na kuwatekeleza kiasi hiki ukilinganisha na wafanyakaziwengine. Ni kichekesho Mwanafunzi aliyepata daraja la NNe (Divisioniv) awe mwalimu amwandae mwanafunzi ambaye hana vitabu, maabara na uchache wawalimu apate daraja la kwanza (Division i) kati yawanafunzi 100 utapata wanafunzi 5 na wanafunzi 95 watafeli wengi wao watapata (Divisioniv) kama yeye wengine zero. 2. Kuna wakati Tanzania ikisherehekea uhuru wake, hayatiMwalimu Julius k. Nyerere Rais wa kwanzawa habaari kutoka nje ya nchi. Jamhuri ya Tanzania aliauzwa swali lifuatalo nawaandishi wa habari kutoka nje ya nchi. Kitu gani. hasakinawafanya Watanzania msherehekee siku hii ya Uhuru weni? Hayati J.K Nyererealiwajibu kuwa Watanzania walikuwa wakisherekea siku ile kwa sababu ya kuwa haihadi siku ile. Huenda jibu lile lilikuwa sahihi. Hata sisi tungeulizwa swalikama lile leo bila shaka tungejibu kama alivyojibu hayati J.K Nyerere. 3. Je hali ya elimu nchini ikoje? Kuna wakati nchi yetu ilisifikasana kwa kufanikisha Elimu ya Msingi kwa kutumia njia za kimapinduzi chini yaushauri wa mzee Nicholas Kuhanga. Wakati huo Tanzania ilitoa Elimu ya Msingi naElimu ya kisomo bura kwa watoto na watu wazima wote. Vilivile serikali ilitoaelimu ya sekondari nayo vyuo vikuu kwamalipo kidogo. Kumbuka elimu hiyo itlithaminiwa kote duniani. Dosari kubwakatika utoaji wa elimu ya sekondari nayo vyuo vikii ni kwamba kwa muda mrefuhata baada ya Tanzania kupata uhuru iliendelea kutolewa kwa watu wachache sana.Leo elimu ilele inatolewa kwa watu wengine zaidi na kwa gharama nafuu zaidi.
I. VUGUVUGU LAUJENZI WA SHULE NA VYUO VIKUU NA MATATIZO YAKE. 5. Ni katika miaka ya hivi karibuni tu ndipo vuguvugu laujenzi wa shule za sekondari za serikali, za binafsi na vyuo vikuu lilianzakujitokeza na kusababisha leo Tanzania kuwa na vyuo vikuu na vyuo vishirikikufikia 40. leo shule za sekondari na vyuo vikuu vinaota kama uyoga. Pongeziziwaendee wananchi na wote waliohusika na ujenzi wa shule hizo. Kwa upande wasekondari watu binafsi wanajenga shule hizi kwa kutegemea fedha zitokanazo kwawazazi wa watoto wakati kwa upande wa Vyuo vikuu watu binafsi wanajenga kwakutegemea mikopo toka BODI YA MIKOPO. Kwa hiyo bila mikopo hiyo (Loan Board).Baadhi ya vyuo vikuu haviwezi kudumu. 6. Hata hivyo mwamko wa wazazi kupenda elimu umesababishaelimu kupatikana kwa njia za ulanguzi. Shule za binafsi ni za watu wenye uwezo,kama zilivyo hospitali binafsi. Leo shule za serikali ndizo shule za watu wakawaida. Tatizo jingine linatokana na wamiliki wa shule za binafsi nikuwarubuni walimu wa shule za serikali ili wajiunge na shule zao na ilikuwapata huongeza mishahara na malupulupu mengine mengi. Matokeo ya kufanyahivyo ni shule za binafsi kufaulisha watoto vizuri kuliko shule za serikali.Leo baadhi ya wazazi wako tayari kupelekea watoto wao katika shule za binafsihata kama wamechaguliwa kwenda katika shule za serikali. Wazazi hawaelewi kwanamna gani shule yenye 7. wanafunzi zaidi ya 400 inaweza kuendelea kielimu wakatiikiwa na walimu watatu au wane tu. Shule tunazo lakini zinakabiliwa na uhaba wakila kitu (walimu, vitabu, maabara, vyumba vya madarasa, mabweni, matundu yavyuo, nyumba za walimu, maktaba nk.) maneno ya kuzingatia hapa ni UHABA naUKOSEFU walimu wa masomo, huduma ya maji, umeme, zahanati, mabweni, viwanja vyamichezo, vifaa vya michezo na kadhalika. Msamiati huu pia unatawala vyuo vikuu,vya ualimu, shule za Elimu ya Msingi, vyuo vya ufundi na kadhalika. NI UHABA NAUKOSEFU wa mahitaji katika kila ngazi ya elimu. Shule za sekondari za kata aushule za madiwani zote zinakabiliwa na uhaba na ukosefu waq mahitaji ya shule. 8. Kutokana na UHABA NA UKOSEFU huo elimu inaporomokaKATIKA NGAZI ZOTE. Hii ndiyo hali ya elimu nchini Watanzania wanaopenda ukweliwanajua ukweli huu. Kazi kubwa ya wanafunzi wa vyuo vitapoteza umuhimu wakuwepo kwake. Tume ya elimu ya 1982 inasisitiza sual hili. Naomba wale ambaohawajasoma ripoti ya TUME YA ELIMU ya mwaka 1982 na mapendekezo ya tume yakewaisome. Sehemu kubwa ya mapendekezo yale ni muhimu zaidi leo kulilo mwaka1982. inasikitisha kuona kuwa Watanzania wengi hatuna muda wa kusoma vitabu aumaandishi! Tuna muda wa kufanya mambomengine! Binafsi naamini kuwa TUME ya 1982 ilifanya kazi nzuri. Wajumbe wa tumeile wengi wao wangalia hai. Kwa namna gani wanashirikishwa katika kuboreshaelimu nchini ni swala zuri la kujiuliza. Kwa tabia ya watanzania si rahisikuwashirikisha watu wengine katika mambo yetu. Kwa mfano, Mwalimu NicholasKuhanga aliyefanikisha UPE katika nchi yetu kwa nini tusimshirikishe katikauboreshaji wa elimu nchini? 9. Leo shule za sekondari na vyuo vikuu vinaongezekawakati ubora wa elimu unazidi kupungua. Kwa mfano, katika matokeo ya mwaka 2010nusu ya vijana wa kadato cha nne waliofanya mtihani wa Taifa hawakufaulu. Hatakatika miaka mingine, vijana wengi wanafaulu kwa viwango vya chini yaani, divisheni3 na 4 idadi ya wale wanaoshindwamitihani ya mwisho minazidi kuongezeka. (Tanzania kiambatanisho) kuonyesha kuwaubora wa elimu nchini unaporomoka. 10. Labda wengine hawapendi kusikia maneno, kushuka kwaubora au kuporomoka kwa elimu. Naombawatushauri tutumie maneno gani? 11. Sisemi kuwa elimu imekufa bali nasema ubora wa elimuumepungua (vijana wengi kushindwa mtihani wa kidato cha nne). Mfano Baraza laTaifa (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyikamwaka jana 2011 yanaoneasha kuwa asilimia 53.59% ya wanafunzi 426,314waliofanya mtihani huo wamefaulu huku ikitangaza viwango vya ufaulu kamaifuatavyo.
Wanafunzi waliopata daraja la kwanza hadi latatu ni 33,577 sawa na 9.98% wamefaulu huku wasichana waliofaulu kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu ni10,313 sawana 7.13% na wavulana ni 23,267 sawa na 12.13% Na waliopata Daraja laNNe ni 146,639 sawa na 43.60% ambao wavulana ni 87,039 sawa na 45.40% nawasichana 59,600 sawa na 41.22% Na waliofeli (zero) ni 156,089 sawa na 46.41% kati yao wavulana ni 81,418 sawa na 42.47% nawasichana wakiwa na 74,667 sawa na 51.64%. kwa maana hawa hawatapata vyeti vyakuhitimu kidato cha NNE. Na huku wanafunzi 3,303 wakifutiwa matokeo kutokana naudanganyifu Mwaka juzi 2010 wanafunzi450,324 walisajiliwa kufanya mtihani ambao wasichana walikuwa 201,799 sawa na44.81% na wavulana 248,525 sawa na 55.19% ufaulu wao ulikuwa kama ifuatavyo 2010. wasichanawaliofaulu ni 69,913 na wavulana 110,303 kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemeawaliofaulu ni 44,910 wasichana wakiwa 20,972 na wavulana 23,938; Hivyo kwamahesabu ya kawaida wanafunzi 180,216 ndiyo waliofaulu kati ya 450,324 mwaka2010 na wanafunzi 270,108 wako barabarani wanaungua na jua sababu walifelikabla wazazi hawajaishiwa na uchungu wa wanao kufeli kidato cha NNe 2010konteina la NECTA limeshusha mzigo mwingine wa wanafunzi 156,089 mwaka 2011 naowamefeli poleni sana wazazi wetu, poleni sana wadogo zetu kwa matokeo hayomabaya ambayo hata cheti cha kidato cha NNE hamtapata. Hivyo ndani ya miaka miwili 2010 na 2011 Ndugu zetu wanafunzi wa kidato cha NNE 426,192 wamefeli kati ya876,638 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2010 na 2011. Hilitunaomba Serikali ilitangaze kama (JANGA LA KITAIFA) kama vijana 426,192 wakomtaani wanateseka na ugumu wa maisha na ni upi mustakbali wa maisha yaowatapataje ajira hawa hata vyeti vya kidato cha nne hawatapata Na hii ni miakamiwili je itakuwaje miaka 50 ijayo. Pia tathiminiiliyofanywa hivi karibuni kuhusu hali ya elimu katika nchi za Uganda, Kenya naTanzania imeonyesha kuwa Tanzania inatoa elimu hafifu kuliko katika zoezi hiiunaweza kuendelea ila naomba tutenganishe utaalamu na siasa. Kwa mfano, kunabaadhi ya wana siasa wanapendekeza kuwa mitihani ifutwe katika ngazi zoteFulani za elimu. Lakini hawapendekezi njia gani zitumike katika kupima elimuitolewayo nchini. Hata hivyo sielewi lengo lao nini hasa. Watanzania tukikiukamsingi ya kutolea na kupatia elimu bora, misingi hiyo itakiuka. 12. Lazima tujiulize maswali yafuatayo kuhusu Elimuitolewayo katika nchi yetu: Tunataka nini katika elimu yetu. Tuataka elimu yetuitatue matatizo gani? Je elimu hii inatatua au inaongeza matatizo? Je tunataka elimu ya bure nay a lazima kwawatanzania wote na ifikie ngazi tunataka elimu ya bure nay a lazima kwawatanzania wote na ifikie ngazi gani? (MSINGI AU YA SEKONDARI AU VYUO VIKUU) jekuna uhusiano gani kati ya maendeleo katika katika elimu na maendeleo yetukiuchumi? Je, kwa namna gani BODI YA MIKOPO itaweza kukidhi mahitaji ya vyuobila kufanya mabadiliko ya kimsingi katika sera ya Elimu? Kwa nini watoto wamatajiri ambao tangu elimu ya awali, msingi na sekondari wamekuwa wakisomakatika shule za binafsi kwa gharama kubwa leo wanaomba mikopo na serikaliinawapa mikopo hiyo. Tatizo hili halijatatuliwa.
- TANZANIA IMEPIGA HATUA KUBWA KATIKA ELIMU LAKINI
Elimu ni ufunguo wa maisha, ndivyo ambavyo watanzania wengi tunaamini hivyo, kwani elimu husaidia kutupa maarifa ya kuweza kuishi vyema kutokana na mazingira tuliyopo na kupanua upeo wetu wa mawazo.
Pia elimu hutusaidia kupata ajira au kuwa na uwezo wa kujiajiri wenyewe katika shughuli mbalimbali, kujitambua kuwa na upeo wa kunga’mua mambo mbalimbali ili kuweza kuishi sambamba na mazingira. Katika nchi yetu miaka ya hivi karibuni kiwango cha elimu kimeonekana kushuka ukilinganisha na miaka ya nyuma. Tumejaribu kumtafuta mchawi, lakini mpaka sasa hajapatikana, ukweli ni kwamba tatizo kubwa lililopo ni mfumo mbovu wa elimu uliopo, walimu wengi wamepoteza ari ya kutimiza
majukumu yao ya ufundishaji. Kubadilika badilika kwa mitaala, uchache wa zana za kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi, uongozi mbovu, walimu kutolipwa stahiki (madeni) kwa wakati na matatizo mengine lukuki yaliopo katika wizara ya Elimu ni tatizo kubwa linalorudisha maendeleo ya elimu nyuma hapa nchini.
Mfumo mzima wa elimu katika nchi yetu umekuwa haueleweki hivyo kusababisha kuwachanganya walimu na wanafunzi katika masomo. Kila kiongozi anayeingia katika wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi anakuwa na msimamo wake, wakati wa uongozi wa Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu Bw. Benjamin Mkapa, kuna waziri alipewa dhamana kuiongoza wizara hiyo na matokeo yake akakulupuka na kuamua kuyavunja masomo ya Jiografia, Uraia na Historia katika shule za msingi na kubakiza somo moja ambalo aliliita Maarifa ya jamii.
Tanadiliki kusema kuwa alikurupuka kwani hakuweza kufanya uchunguzi na kujua uwezo wa walimu wake wa kufundisha masomo hayo matatu kwa mara moja tena kwa mwalimu mmoja. Na baadae ilikuja kugundulika kuwa kuna baadhi ya walimu hawawezi kumudu masomo yote hayo na badala yake anauwezo wa kufundisha Uraia, lakini hana uwezo wa kufundisha Historia hivyo Mwanafunzi ndiye anayeumia kwa kutopata taaluma iliyokamilika.
Kwenye shule za sekondari Waziri huyo aliamua kuunganisha masomo ya chemistry na physics na kunganishwa kama somo moja na kuitwa (chemistry with physics) la kujiuliza hivi huyo waziri alijiuliza kama kama Mwalimu aliyesoma fani (combination) CBG hawezi kuimudu au kufundisha PHYSICS akipangiwa kufundisha somo la chem./phy. Ninashukuru kwa kuwa serikari iliyopo madarakani imeliona hilo na kuamua kurudisha mfumo wa zamani wa kila somo kujitegemea ingawa kodi za wananchi ziliteketea kwa kutunga tena vitabu badala ya hizo pesa kufanya kazi nyingine kwa jamii.
Kuna tatizo la walimu kupoteza ari ya kufundisha, hali hiyo imesababisha wanafunzi kutopata taaluma iliyokamilikan matokeo yake kufeli na kufutiwa mitihani mfano kidato cha nne mwaka huu wanafunzi 3303 na darasa la saba wanafunzi 9700 wamefutiwa mitihani kwa madai ya kuibia mtihani ni muhimu Serikali ikajiuliza kwa nini Wanafunzi hawa wanaibia mitihani?. Hii inasababishwa sana na walimu kutolipwa madeni yao ambayo wanaidai serikali na kutoboleshewa mishahala, mazingira ya kazi na wakati mwingine
kupoteza kabisa matumaini ya kutolipwa stahiki zao na wao kuamua kulipiza kisasi kwa kutofanya kazi kwa bidii na maarifa.
. Walimu wapo kwenye mgomo baridi serikali ifanye utafiti itagundua bado haijashutuka. Lakini Wanaoumia zaidi ni wanafunzi na walimu wengine wameamua kuacha kazi na kuamua kurudi mitaani na kuendelea na maisha mengine. Katika hatua yoyote ya ufundishaji na ujifunzaji zana ni muhimu, lakini cha ajabu na kushangaza shule nyingi hazina zana za kufundishia wala kujifunzia na pale ambapo zipo ni chache, haziko imara au zimepitwa na wakati. Hapo ndugu zangu Watanzania mnategemea Elimu ipande labda kwa nguvu za miujiza ya Mungu au nguvu za giza.
Katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu na kidato cha NNE mwaka huu tumeshuhudia wanafunzi wengi wakifutiwa matokeo yao kwa kile kilichoitwa Eti ni udanganyifu. Tunazitupia lawama zote kwa serikali, mfano huyu mwalimu ambaye halipwi vizuri, hana nyumba nzuri ya kuishi (haina umeme,maji,choo), mshahara hautoshi (ugumu wa maisha) hana zana za kufundishia na hata motisha pia hapati mwaka mzima, ATAWEZAJE KUFUNDISHA?.
Na je? Wanafunzi watapataje maarifa ya kutosha na kuweza kujibu maswali kwa usahihi katika mitihani yao kama si kuwatafutia majibu ili wafaulu hata wasiojua kusoma wala kuandika kama sio kuwatupia mzigo? Pamoja na hayo yote, lakini pia tunaipongeza Serikali kwa kujenga shule za kata, ambazo hazina zana za kufundishia.
Mwalimu mmoja shule nzima yeye ndiye mwalimu mkuu na pia ndiye mwalimu wa somo, yeye ndiye mwalimu wa zamu, nidhamu, taaruma na uchache wa madawati HIVI HAPA TUNATEGEMEA KUPATA TAIFA LENYE WASOMI KWELI WATANZANIA? Na kurudishwa kwa mitihani ya kidato cha pili hatudhani kama ni hatua ya kuokoa Elimu ya Tanzania. Ni sababu gani zilipelekea mitihani hiyo ya kidato cha pili kufutwa na sasa kurudishwa? Jamani ELIMU SIYO SIASA YA MAJARIBIO.
Suala la msingi kwanza ni kubadili mfumo mzima wa ELIMU TANZANIA na kuboresha shule za kata zinazochukua maelfu ya watoto maskini kwa kuwaajiri walimu wa kutosha wenye uwezo mzuri wa kufundisha, kuwalipa walimu stahiki zao, kubolesha mishahala yao (kima cha chini) na pia Serikali iwasikilize wadau mbalimbali wanapotoa maoni yao juu ya uboreshaji wa Elimu yetu ili tulikomboe Taifa letu. Zaidi rejea mapendekezo yetu.
katika makala haya tunazungumzia mafanikio na matatizo ya elimu katika miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. Takwimu kuhusu idadi ya shule, vyuo, walimu na wanafunzi zinapatikana kwa urahisi kutoka wizara husika. Takwimu hizo zinaonyesha kuongezeka kwa kila kigezo cha kutolea na kupatia elimu nchini.
Tunashauri tuzitumie vizuri taarifa hizo. Kwa mfano, idadi ya dhule za sekondari za serikali imeongezeka sana. Kwa mfano, idadi ya walimu wa shule hizo, lakini vipi uwiano kati ya walimu na wanafunzi katika shule hizi? Ukweli ni kwamba walimu ni wachache kwa uwezo wa kufundisha na kwa idadi yao. Kutokana na uchache na uwezo wao mdogo wanafunzi katika ngazi zote za elimu nchini hawapati “dozi” kamili ya elimu wanayotakiwa kupata hali inayosababisha wanafunzi kumaliza elimu wakiwa hawajapata “dozi” kamili ya elimu wanayotarajia kuipata. Kwa hiyo watanzania tusishangae kwa nini nchi yetu ni ya mwisho katika utoaji wa elimu bora katika Afrika ya Mashariki.
Kamwe vijana wetu hawataweza kupata elimu bora ya Msingi au ya sekondari,na Vyuo vikuu kwa kukaa tu katika majengo yaliuoandikw “shule” au Chuo kikuu. Kamwe vijana hawatawez kupata elimu ya ngazi yoyote ile kwa njia ya OSMOSIS. Upatikanaji wa elimu bor un kanuni na misingi yake. Tukikiuka misingi ya utoaji elimu bora misingi itatukiuka. Kama elimu bora ni ufunguo wa maisha bora basi elimu bora basi elimu mbaya ni ufunguo wa maisha mabaya.
- TUNAPATA WAKATI MGUMU KATIKA MASUALA YA ELIMU
Watanzania tunapita wakati mgumu kiasi kwamba hata kubaki hapa tulipo ni kazi ngumu, kurudi nyuma ni kazi rahisi, kwenda mbele ni kazi ngumu zaidi. Breki za gari tulilopanda hazishikiki. Kuna hata ya gari kuruki nyuma. Gari hili ni nchi yetu ya Tanzania. Nchi ikirudi nyuma tutapoteza hata mafanikio kidogo tuliyoyapata katika miaka 50 ya uhuru. Hali inazidi kuwa mbaya. Vyanzo vya maji vinakauka, nchi inakosa umeme gharama za huduma muhimu zinazidi kupanda mfumuko wa bidhaa unapanda kwa kasi vijana wanakosa ajira na nguvu kazi yao haitumiki. Maana yake ni kwamba mapendekezo yoyote ya kuboresha elimu lazima pia yaonyeshe nchi itapata wapi fedha kufanyia kazi hiyo? Kwa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa ushuru kuondoa na kufuta aina zote za posho za semina, (sitting allawance) katika ofisi za umma Taasisi za umma kwani ni pesa nyingi zinapotelea huko bila sababu za msingi, fedha za kutosha za kuboreshea sekta ya elimu.
Fedha ya misululu ya magari makubwa yaendayo Zambia, Malawi na Congo kila siku inatumikaje? Watu wamepata wapi fedha ya kununua utitiri wa malori, magari madogo na mapikipiki yanayosababisha barabara zisipitike katika miji yetu? Pamoja na umaskini wetu lazima watanzania tujue kuwa maendeleo yetu yataletwa na sisi wenywewe kwa bidii, maarifa, nidhamu, na kwa kuitegemea. Serikali inauwezo mkubwa wa kutunga sheria na kuweka taratibu za kusimamia uchumi lakini haina uwezo wa kusimamia taratibu zake. Ni nchi zenye serikali imara kama Marekani ndizo zinaweza kusimamiea uchumi wake. Kwa mfano serikali bila kupanga imekabidhi uchumi wa Tanzania kwa watu wachache ambo inashinswa kuwatoza kodi. Kwa nini tusichukue hatua zifuatazo:-
- Tusimamie vizuri shughuli zote za maendeleo ili kuzuia ufujaji wa fedha.
- Serikali isimamie elimu italewayo nchini ili kuondoa Ulanguzi Utapeli nauchakachuaji na iboreshe zana za kusomea hasa shule za kata (vitabu maabara walimu maktaba)
- TCU iongezewe madaraka zaidi kuhusiana na vyuo vikuu
- Tuongoze ufanisi katika kazi zetu na kupenda kufanya kazi
- Tubane matumizi na kutumia vizuri kila senti tunayopewa.
- Tuache rushwa, ufujaji mali ya umma na uvivu.
- Tupunguze sherehe, tafrija, mikutano, semina na kpngamano yanagharimu pesa nyingi.
- Tutumie vizuri wakati
- Tupunguze michango ya starehe (Inner partu, Send-off, Bag Party, Kitchen Party na Wedding part) na tuwekeze elimu .
- Tusipinge migomo badala yake tujue kwa undani sababu ili kama ni uzembe hatua kali ziwe zinachukuliwa kwa wahusika mapema.
- Kama idadi ya wanafunzi wa kwenda vyuo vikuu huwa haijulikani hadi mwezi mmoja kabla ya vyuo kufunguliwa tunategemea nini. Tujisahihishe. Nani alaumiwe? Kama migomo huzaa matunda kwa nini ifutwe.
- Tuanzishe michango ya maendeleo ya elimu badala ya michango Harusi.
- Tubadili mwelekeo wetu au mtazamo wetu kuhusu umuhimu wa mambo (mindset). Kwa mfano kuongeza ubora wa elimu bila kuwashirikisha wananchi katika gharama.
- Kama kuna wakati mzuri wa kubadili mambo au kufanya mapinduzi katika elimu basi wakati huo ni sasa. Mwamko wa watu wa kuelewa na umuhimu wa kutoa elimu kwa watoto wao umeongezaeka. Matatizo ni mengi, na hakuna nchi isiyo na matatizo ni muhimu suala la Elimu liwekwe wazi katika katiba mpya ijayo.
- Elimu kwanza. Kwanza Inaelekea treni la elimu liko nje ya reli.
Watanzania tunawezaje kulirudisha treni katika njia yake. Tanzama baadhi ya shule za Elimu ya Msingi bado baadhi ya wanafunzi wanamaliza karasa la saba wakiwa hawajui kusoma na kuandika ½ ya wanafunzi wanaomaliza kadato cha nne wanafeli mtihani wa mwisho. Kama watoto wanamaliza elimu ya msingi bila elimu ya msingi wataendeleaje mbele? Ni Elimu gani hii ambayo haimwezeshi mwanafunzi kuwaelezea watu kile anachokijua au kubuni na kuibua mabo, kufikiri kisayansi, au kupeleleza na kuchambua mambo, kuumba vitu, kutafuta njia sahihi za kutumia katika kutatua matatizo yake. Tukubali kuwa elimu yetu ni butu. Tofauti na wenzaao walioachwa nyuma baada ya kumaliza elimu ya Msingi hawawezi kulima, kuzurura mitaani na kucheza disco. Lakini ajabu ni kwamba vijana hawa wanataka makuu, wanataka wakipanda mahindi asubuhi wavume jioni. Mara wakianza kazi wanataka kuwa na simu pana, gari la kuendea kazini na nyumba nzuri ya kuishi. Pale wanapokosa vitu hivi hupauka akili na huwafanya wafanye yasiyotegemewa. Vijana hawa ni wengi na wanaongezeka kila mwaka. Serikali isipowatumia vijana hawa watu waovu watawatumia.
- HOJA YA KUTUMIA UZOEFU ULIOKO NCHINI.
- Duniani hakuna kidumcho isiopkuwa mabadiliko.
Watanzania wana haki ya kupata kilicho bora katika nchi yao ikiwa ni pamoja na kuwatumia watumishi bora waliostafu na vijana wenye akili kwa faida ya nchi yao.
Tabia ya kuwatenga au kutowatumia watu hawa ni tabia mbaya inayodidimiza nchi yetu. Kuwatenga watu kwa sababu za kisiasa au kwa sababu ya kuwaogopa au kwa sababu ya roho mbaya ni ufisadi wa aina yake. Wenzetu huko Ulaya ambako tunainga mambo mengi wanafanya hivyo. Si vema kwa baadhi ya watanzania kuonekana hawatakiwi au wanaishi kwa hisani ya watu Fulani. Wale wenye uwezo au madaraka wanaweza kumuua raia yoyote au kumtesa au kumtenga kwa sababu zozote zile ila sssshawawezi kunyang’anya utaifa na uraia wake, hawawezi kumfukuza katika nchi yake.
- Tume ya elimu ya chini ya uenyekiti wa MAKWETTA (1982) ilichambua hali ya elimu iliyokuwa ikitolewa wakati ule hapa nchini. Pia ilitembelea nchi nyingi zilizoendelea na zisizoendelea ili kujifunza taratibu zao za utoaji elimu. Tume ilijifunza mengi na kutoa mapendekezo kwa serikali. Ni muda mrefu umepita tangu (1982). Kama serikali inatekeleza au haitekelezi mapendekezo ya Tume mimi sina la kufanya. Ajabu tangu tume ripoti ili hawajawahi kuitwa au kuulizwa lolote na wizara husika kuhusu elimu nchini. Kwa maoni yangu hii ni kasoro kubwa katika nchi yetu.nchi haifaidiki na utajiri wa uzoefu wa watu walio nje ya mkondo wa serikali kwa sababu ya sababu zilizoeleweka (wataalamu majaji, wanajeshi,walimu, mawaziri hawatumiki). Watu hawa ni hazina ya nchi na si tishio kwa yeyote. Nchi hii ni yetu sote. Tusiwaenzi watu wliostaafu baada ya kufa kwa kuhudhuria mazishi yao. Tusisubiri watu wafe ndiyo tuseme mazuri yao.
- BAADHI YA VIKWAZO VILIVYO MBELE YETU.
Huenda mapendekezo ya Tume ya MAKWETTA yamepitwa na wakati. Hofu yangu ni kwamba tangu Tume ili itoe mapendekezo yake kwa serikali hawajawahi kuitwa kutoa ushauri au ufafanuzi wowote kuhusu mapendekezo ya Tume. Napendakeza iundwe Tume nyingine kwa madhumuni yaleuale ili kukidhi mazingira ya karne ya 21. tusichezee elimu madhara ya uharibifu yatakuja jitokeza miaka michache ijayo.
- Hapa chini tunatoa mapendekezo lakini mapendekezo haya yatafanikiwa tu kama baadhi ya mambo yaliyoko yatabaki kama yalivyo. Mabadiliko katika baadhi ya mambo yalioko leo yataathiri nguzo muhimu za kutolea na kupatia elimu.
Kwa hiyo mapendekezo yoyote kuhusu mabadiliko katika mfumo wa elimu nchi nzima yazingatie mambo yafuatayo:-
- Kuongeza kwa idadi ya watu ambao hawana elimu ambako kuasababisha kukua kwa umaskini.
- Kuweko kwa watu wenye uzoefu na kutotumia uzoefu wao kujenga Taifa letu kwa sasabu ya tofauti za kisiasa.
- Kushuka kwa uchumi kutokana na kupungua kwa mafuta, gesi, maji, umeme, madini nakadhalika.
- Uhaba au kukosekana kwa chakula (njaa).
- Kukua kwa umaskini na kukosekana kwa amani.
- Kukosekana kwa ajira na kutotumika kwa nguvu kazi.
- Ubaguzi wa kipatao (maskini na matajiri) kuongezeka kwa mpasuko kati wenye nacho na maskini.
- Kurudi kwa ukoloni mambo leo na utumwa
- Wenyenavyo watashika mali na utawala wa nchi
- Kustawi kwa ukoloni mamboleo. Nchi itageuka nchi ya ombaomba. Kesho ni leo na leo ni kesho. Kwa hivyo kila jambo tufanyalo au tusilofanya leo linajenga au kubomoa missingi ya maendeleo yatu ya kesho. [The future is now.]
- HATUA ZA KUCHUKUA ILI KUZUIA KASI YA KUPOROMOKA KWA ELIMU NCHINI.
- Kobe kufanya maendeleo pale tu anapothubutu kutoa shingo yake nje ya gamba lake. Kwa hiyo pamoja na yote yanayosemwa kuhusu elimu, ni vigumu sana kutabiri kuhusu mambo yatakavyokuwa kesho. Labda tutumie ujenzi na uzoefu wetu katika kuelezea baadhi ya viini vya matatizo katika shule na vyuo vyetu:-
- Wizara ya Elimu iunde haraka Tume ya Elimu ili kutizama matatizo ya elimu na mwelekeo wake kwa lengo la kuzuia Tanzania kuachwa nyuma kielimu au kuzuia kuporomoka kwa elimu.
- Serikali isimamie na kuratibu elimu katika ngazi zote ili kuzuia biashara na ulanguzi katika elimu chini.
- kutokana na uwezo mdogo wa walimu hasa walimu wa shule za sekondari, yaanzishwe mafunzo ya kuboresha elimu yao wawapo kazini
- Serikali itizame upya sera ya kugharamia elimu nchini ili kuhakikisha kuwa fedha ya umma inatumika vizuri na inatolewa mapema kwa wahusika.
- Hatua za kuboresha elimu zianzie katika vyuo vya ualimu, vyuo vikuu na shule za msingi na mafunzo kazini.
- sekta ya ukaguzi imarishwe kwa kuongeza wakaguzi na vyombo vya usafiri.
- migomo shuleni na vyuoni inaathiri sana maendeleo ya elimu nchini licha ya kuharibu mali ya umma. (Sera ya Mikopo bado hafifu)
- wanafunzi washirikishwe katika masuala ya maamuzi yanoyo wahusu na sio watawala wanawaamulia kila kitu bila wao kushilikishwa
- wanafunzi wajihusishe na ubora na usalama wa mazingira ya shule na vyoo badala ya kubaki na 3ks tu yaani KUSOMA,KULA NA KULALA.
- ubadilishwaji wa mitaala ushilikishe pande zote kama walimu, wadau wa elimu, wanafunzi wenyewe na wizara ya elimu na sio kiiongozi mwenye dhamana anaamua atakavyo sio sahihi athari yake tunaiona inavyotuathiri kwa sasa.
- Walimu wawezeshwe kwa kupewa vyombo vya usafiri (kupitia mikopo)
- Baadhi ya wazazi watatakiwa kulipa ada yote katika vyuo vikuu ili kupunguza kuelemewa kwa serikali katika suala hili.
- Udhaifu wa serikali usielezwe kwenye vyombo au taasisi zisizohusika (BODI YA MIKOPO) na utoaji wa huduma Fulani muhimu.
- taarifa kuhusu uwezo wa wazazi wa watoto kiuchumi zijulikane mapema.
- Ziundwe BODI ZA ELIMU katika ngazi za wilaya ili kusaidia Wizara ya Elimu kusimamia kwa kuwahusisha wadau wote wa Elimu Wilayani.
- Serikali itizame upya sera kuhusu lugha ya kufundishia shuleni na vyuoni. Lugha ya “Kiswakinge” inayotumika leo shuleni inaaathiri elimu. Leo Kiingereza ni Kiswashili cha dunia!
- Serikali iwe na utaratibu wa kuendelea kuwatumia walimu waliostaafu (Sera au Mwongozo)
- Liingizwe somo la Maadili katika ngazi zote za kutolea elimu nchini.
- Itolewe tafsiri sahihi kuhusu maana ya shule na kuhusu maana ya shule na mahitaji ya shule, chuo. Shule au chuo ni majengo, walimu bora na wakutosha, vifaa bora vya kutosha nk.
- walimu walipwe madeni yao yote kama malimbikizo ya likizo na posho ya kufundishia ili waweze kuendelea kufundisha kwa bidii.
- walimu wenye sifa ya kupandishwa madaraja wapandishwe madaraja na mishahara yao iendane na madaraja waliuopandishwa mara moja.
- Yaboreshwe mazinga ya kazi kwa walimu shuleni kama nyumbani za kuishi, umeme, maji.
- serikali iboreshe mishahara ya walimu. Kutokana na ugumu wa maisha kuongezeka (mfumuko wa bei za bidhaa) ili waweze kuyamudu maisha.
- Sera ya elimu iwe wazi katika ngazi zote. Je ni elimu ya bure kwa watoto wote kuanzia Elimu ya Awali, Msingi (UPG) elimu ya Sekondari (UDE) na ya vyuo vikuu (UUE) na kadhalika.
Hakuna kidumucho isipokuwa mabadiliko
Kama elimu bora ni ufunguo wa maisha bora basi elimu mbaya ni ufunguo wa maisha mabaya. Elimu itolewayo katika Tanzania ni ufunguo wa maisha bora au ni ufunguo wa matatizo? Je vijana wetu wanasoma kwa malengo? Je Elimu itolewayo nchini inakidhi malengo yao? Kama haikidhi kwa nini umma wa nchi hii uendelee kugharamia elimu isiyo na manufaa? Kama shule na vyuo vyetu havifundishi kufikiri, kudadisi haviumbi kazi bali vinaibua tamaa ya kupenda starehe na kazi nyepesi. Tatizo kubwa la nchi hii ni serikali kutofuatilia, wala si tatizo la kukosekana kwa sera. Hili ni taifa la wasemaji maneno na siyo taifa la watekelezaji. Mapendekezo ya tume ya MAKWETTA ya mwaka 1982 licha ya kukubalika na serikali yamewekwa kabatini. Hayatekelizwi kwa sababu wahusika hawataki kupata “taabu”. Baada ya kuichambua tena ripoti ya TUME mimi naona bado yana manufaa hadi leo.
Sasa naelewa kwa nini V.I Lenin alisema matumizi ya nguvu ni lazima kwa mama aliyefikia siku za kujifungua. Kwa maneno yake Lenin alisema “force is a midwifery of any society pregnant of a new one”. Kwa maoni yangu Tanzania ni kama mama mjamzito ambaye siku zake za kujifungua zimefika lakini hajifungui.bila kumpasua mama, wote wawili mama na mtoto watakufa. Kwa hiyo.
- Mama akipasuliwa wote wawili wanaweza kuokolewa (au mmoja wao). Tanzania inahitaji kupasuliwa ama la sivyo itaendelea kudidimia kiuchumi milele.
- Nchi ya Tanzania inahitaji kiongozi shupavu mwenye msukumo mwenye akili na siyo mkusanyaji au malafi, mwaminifu, awe mchapakazi mpenda haki na anayeona mbali.
- Rushwa na utawala usiothubutu ni kama mjamzito: Inahitaji kupasuliwa ili kuwaendeleza watanzania kiuchumi.
- Tufafuteni kwanza maendeleo katika elimu na mengine yote yatafuata.
- Twende pamoja
- Tushirikiane
- Tuboreshe elimu
- Tujinge nchi yetu, Tanzania.
NI LIPI SULUHISHO LA VURUGU, MIGOMO NA MAANDAMANO VYUO VIKUU NCHINI.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa aliahidi bungeni kwenye mkutano wa nne kwamba serikali imepata mkakati wa kumaliza migogoro na matatizo katika vyuo vikuu nchini na kwamba hatua za haraka zingechukuliwa kama sehemu ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2011/2012 .
Hata hivyo badala ya migomo na migogoro kumalizika Tunashuhudia tena kurejea kwa wimbi la uvuguvugu,migomo, maandamano na sitofahamu katika vyuo vyetu vikuu. Katika siku za karibuni pamekuwepo na Maandamano na migomo ya mara kwa mara katika chuo kikuu cha Dar es salaam (UDOM) chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi (Muhas) chuo kikuu cha mtakatifu John Tanzania (SJUT) Aidha hali ya mambo chuo kikuu cha Dodoma haijatulia mpaka sasa huku vurugu, migomo na maandamano hayo yakipelekea wanafunzi wenzetu 934 kufukuzwa vyuo vikuu na wengine kusimamishwa masomo kutokana na vurugu hizo ambazo zimetajwa na uongozi wa taasisi na utawala wa vyuo hivyo kwamba vurugu hizo zimehatarisha maisha na kusababisha uharibifu wa mali .
Tunaomba Serikali itambue kwamba chanzo cha migomo ya hivi karibuni (UDSM)iliyopelekea wanafunzi 56 kufukuzwa chuo na 99 kusimamishwa masomo kwa muda usiojulikana, na kupelekea kuvunjwa serikali ya wanafunzi (DARUSO) ni matokeo ya kugeuzwa kwa utaratibu za utoaji mikopo kutoka bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwenda vyuoni na hatimaye kuchelewa kwa malipo ya wanafunzi na
wengine kupata pungufu au kukosa kabisa. Huku chanzo cha mgomo tarehe 11-`1-2011 kikiwa ni kucheleweshwa kwa pesa zao za kujikimu (boom)na wanafunzi kuamua kusitisha masomo kwenda Ofisi za utawala kuzuia shughuri zozote kufanyika hadi pesa
zao za za kujikimu zitakapotolewa (boom) zitakapoingizwa na chuo. Huu ndiyo utaratibu mpya unaonyesha kutofanikiwa kumaliza vurugu migomo na maandamano vyuo vikuu nchini.
Kwa upande wa Muhaso ambapo wanafunzi 85 walisimamishwa masomo chanzo cha vurugu hizo pamoja na mambo mengine ni madai ya wanafunzi hao kutaka kurejeshewa serikali yao ya (Muhaso) iliyovunjwa na Baraza la chuo Juni 2011. baada ya kukaidi waraka wa serikali wa Mwaka 2009 uliozitaka serikali za Wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kubadili katiba zao.
WITO wetu tunaomba uongozi wa chuo uwafejeshe chuoni wanafunzi wote 85 waliosimamishwa masomo badala ya kuwahukumu kwa kutumia matokeo ya tatizo (Sera) kama chazo cha mgogo wa (muhaso) ambao ni tofauti katika utekelezaji wa agizo la serikali la tarehe 12 Juni,2009 (GN.178) ambayo imefanya mabadiliko makubwa kwenye uendeshaji wa serikali za wanafunzi katika vyuo vikuu na hivyo kuanzisha mivutano baina ya wanafunzi na utawala katika chuo hicho na vyuo vingine nchini
[IMG]file:///C:\DOCUME~1\ADMINI~1\LOCALS~1\ Temp\msohtmlclip1\01\clip_imag e001.jpg[/IMG]
Wanafunzi wa chuo kikuu Muhimbili wakiwa katika sehemu ya mgomo wao wa kishinikiza utawala wa chuo hicho, kurudishwa serikali yao.(Muhaso)
Serikali irejee kwamba chanzo cha migomo (UDOM) ni Madai ya msingi ya wanafunzi kuhusu mafunzo kwa vitendo na malalamiko mengine kutoka kwa wahadhiri. Toka wanafunzi 670 wasimamishwe masomo mwezi Juni 2011 mpaka sasa Ikiwa imepita karibu miezi sita (6) wanafunzi 670 bado hawajalejeshwa chuoni hivyo bado wamesimamishwa masomo huku zoezi la kumhoji mmoja mmoja likisuasua na kutarajiwa kwamba limepangwa kumalizika Mwishoni Mwa Mwezi Marchi 2011.
WITO wetu kwa serikali kuhusu wanafunzi wenzetu waliosimamishwa masomo 670 tunaomba uongozi wa chuo kikuu cha Dodoma kuwasamehe na kuwarudisha chuoni kwani chanzo cha vurugu na mgomo ni kudai mafunzo kwa vitendo ambayo ni madai ya msingi.
Pia Serikali inaweza kabisa kwa kushirikiana na chuo kuharakisha taratibu za kinidhamu. Wakati huo huo kushughulikia Madai ya Msingi ya wanafunzi ili kuepusha Mazingira ya mivutano ya kudumu kwa muda Mrefu.
Tunaomba Serikali itambue kwamba chanzo cha mgomo wa hivi kariburi tarehe 19-12-2011. hadi 21 Disemba mwaka 2011 ni kugeuzwa kwa taratibu za utoaji mikopo kutoka bodi ya mikopo ya wanafunzi kwenda vyuoni na hatimaye kuchelewa kwa malipo ya wanafunzi na wengine kupata pungufu au kukosa kabisa. Ambapo mgomo huo chuoni umesababisha wanafunzi 15 wa chuo hicho kikuu cha mtakatifu John Tanzania (SJUT), kusimamishwa kuendelea na Masomo chuoni hapo kwa kipindi kisichofahamika kwa kile kilichoelezwa kuwa ni vinara wa mgomo na fujo chuoni hapo. Uamuzi huo umefikiwa ikiwa ni siku kadhaa tangu chuo hicho kilipofungwa ghafla tarehe 21-12-2011 ambapo wanafunzi wake wa shahada ya mwaka wa kwanza waliondoshwa chini ya ulinzi mkali wa polisi sababu kwamba, ikiwa ni kuepusha madhara ya vurugu ambazo zingesababishwa na mgomo uliokuwa umepangwa.
Taarifa ya chuo hicho kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa chuo hicho kitafunguliwa 02-01-2012. lakini wanafunzi 15 waliosimamishwa hawatatakiwa kurejea chuoni hapo hadi chuo kitakapofikia Uamuzi wa kuwarejesha au la kuwaonya kutoonekana kabisa katika mazingira ya chuo hicho.
Chuo hicho kilikumbwa na jinamizi la mgomo na vurugu kuanzia tarehe 19-12-2011 ambapo utawala wa chuo hicho uliamua kukifunga ghafla na kuwataka wanafunzi wote wa shahada ya kwanza kutoweka katika maeneo ya chuo ndani ya kipindi cha masaa matatu (3). Hata hivyo kauli ya utawala wa chuo pamoja na ya mwakilishi wa bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ambaye alifika chuoni hapo na kutoa uthibitisho kuwa fedha bado hazijaingizwa chuoni hapo lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda kwa jazba za wanafunzi hao.
Hali katika vyuo vikuu hivi na vingine haiendani na ahadi ambayo waziri Kawambwa alizitoa bugeni na kwa umma miezi kadhaa iliyopita katika kukabiliana na migomo na migogoro katika Elimu ya juu.
Serikali na uongozi wa vyuo vikuu umekuwa ukichukua hatua dhidi ya matokeo badala ya kushughulikia vyanzo vya matatizo kitu ambacho kimepelekea wanafunzi wenzetu kufukuzwa na kufunguliwa kesi mahakamani ni suala la ajabu kweli.
Nitakumbusha kisa ambacho wazee watakuwa wanakumbuka. Ili tulinganishe Maandamano ya wakati wa Serikali ya kwanza ya hayati Mwalimu Julius Nyerere na serikali zilizofuata katika kutoa uhuru kwa wanafunzi haki yao ya msingi kuandamana kufikisha ujumbe wa hisia zao kwa viongozi serikali baada ya njia ya mazungumzo hushindikana.
Na kwa hili naomba vyombo vya dora na jeshi la polisi lijifunze namna linavyotumia nguvu nyingi kukabaili maandamano ya amani ya wanafunzi kwa maagizo ya viongozi wao kwa kutumia Risasi za moto, mabomu ya machozi, maji ya kuwasha, virungu dhidi ya Maandamano ya amani ya wanafunzi ambao huandamana wakiwa na mabango yenye ujumbe wa madai yao bila kuwa na aina yoyote ya silaha au dalili za kufanya fujo au kuathiri shughuri zozote za kitaifa. haya yalikuwa maandamano ya amani ya wanafunzi kuelekea Ikulu wakati wa serikali ya kwanza.
Itakumbukwa Baada kuingizwa kwa jeshi la kujenga Taifa kikundi cha Wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam kiliandamana hadi Ikulu kupinga kupelekwa kwenye “kulitumikia taifa” kama sehemu ya mchango wao baada ya Taifa kuwalipia gharama yao ya elimu ya juu. Serikal ilikuwa imesema kwamba, wasomi wetu
wote watalipwa kiasi cha fedha ambacho kilikuwa chini ya kipato cha mshahara wa mtumishi wa umma na sehemu ya Mshahara wao ambao wangelipwa ilikuwa ni zile gharama ambazo taifa limeingia juu yao.(walikuwa wanasoma bure). Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam waliamua kuandamana kupinga mtindo (sera) wakidai kuwa ulikuwa unanyonya nguvu kazi zao hivyo walitaka walipwe kama watumishi wengine.
Walipofika Ikulu (hapo hapo anapoishi kikwete leo) walipokewa na Rais Mwenyewe Julius Nyerere pamoja na Mzee kawawa. Hawa wanafunzi Hawakuitiwa mbwa wala polisi au Mabomu ya Machozi na vilungu kama ilivyo kwa wanafunzi wa sasa wanapoitisha maandamano ya amani kuelekea kwa viongozi kufikisha madai yao huambulia vilungu mikong’oto, mabomu ya machozi, Risasi za moto, maji ya kuwasha na utumiaji wa nguvu kubwa kupita kiasi kuthibiti maandamano ya wanafunzi. Bali msafara wa maandamano huo kipindi cha Julius Nyerere kuelekea Ikulu waliruhusiwa kuja na hoja zao na kuzungumza kwa uhuru wote kueleza Manun’g’uniko yao. Rais Nyerere hakuwatisha wala kufanya lolote baya zaidi ya kuwasikiliza kwa kina.
Kiongozi wa Msafara huo alihitimisha hoja yake kwa kumwambia Rais Nyerere kuwa wao hawa kuwa tayari kwenda JKT na kama Serikali itawalazimisha basi “miili yetu itaweza kwenda, lakini roho zetu hazita kwenda na mapambano kati ya wanyonge na walionacho yatadumu”.
KIINI CHA MIGOMO VYUO VIKUU NCHINI NI HIVI:
- Bodi ya mikopo Elimu ya juu [HESLB]
- Mfumo mpya wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi 2011/2012. vikiwemo vipaumbele vya serikali
- Serikali kuingilia Jumuiya na Serikali za wanafunzi.
- Uhaba na uchache wa hostel vyuo vikuu nchini
- Tatizo la ada kupandishwa mara kwa mara vyuo binafsi nchini
- Ubovu wa miundombinu vyuoni nchini
Kuifuta au kuitafutia ufumbuzi wa kudumu sera ya cost sharing, bodi ya mikopo na mchujo ni wakati muafaka kuelekea uundwaji wa katiba mpya ili kutafuta suluhu
sahihi, ila kwa sasa nashauri serikari ibadilishe utaratibu wake wa mchujo (means testing). Utaratibu huu ndio unoleta mgogoro sasa kwani wanafunzi wahitaji hawapewi mkopo ipasavyo na wale wasiopaswa kupata ndio wanapewa mkopo. Makosa ya wanafunzi wengine kupewa mkopo mara mbili au zaidi yanajitokeza mara kwa mara. Wajiulize juu ya hiyo means testing isiwe ya kienyeji (kilocal local)
kwani kuna ripoti za waliotumwa kufanya utafiti juu ya nchi jirani zinavyofanya means testing, kwa nini ripoti hizo zisitolewe wazi ili zijadiliwe kama kuna uwezekano tuanze kuzitumia hata kama ni gharama sana, ni heri kuliko kuendelea kusahaulisha uzalendo kwa vijana…Si busara kwa chuo kutoa ushirikiano kwa wanafunzi na kufunga chuo tena kwa muda usiojulikana kwani hii ni aibu na ninachelea kusema sijui itakuwaje.
Hivi serikali inajua shida/adha/kero n.k. Vinavyowapata wanafunzi wa vyuo hasa baada ya chuo kufungwa, hasa wale wa nje ya nchi na wasio na ndugu hapa mjini…..
Yanipasa kutoa kisa cha binti aliyeutunza ubinti wake sanaa ila chuo kikuu cha UDSM kilipofungwa mwaka 2008 kwa kuwa hakuwa na ndugu DSM aliangulia mikononi mwa jibaba lililokuwa likimfuata fuata kwa muda mrefu hadi aliponaswa wakati huo {boom} limeisha, kwao ni mkoani mbali, hayo na mengine mengi yakamfanya ajipatie hifadhi kwa hili jibaba lililomgeuza mkewe na kumwambukiza VVU!
- Ni mabinti wangapi wanageuka machangudoa……
- Laiti jamii inayothubutu kuwalaumu wanafunzi ingeelewa matatizo yawapatayo wanafunzi hawa hivi vyombo vya habari viko wapi kuelezea na kuchambua kidedea na kiini cha matatizo. Wakowapi hao development partner kufuatilia chanzo cha matatizo [grass root] badala ya kiridhika na ripoti za viongozi wetu,wako wapi kutoa technical assistance na capacity building badala ya kutoa fedha tu.
- Pia Serikali inapata hasara kubwa chuo kinapofungwa kwa sababu ya mgomo au vurugu za madai ya wanafunzi kwani tayari bajeti ya chuo inakuwa ishapangwa ya mwaka mzima wa masomo. Kumbuka hizo pesa ni za walipa kodi wa nchi hii ambazo zingepelekwa kwenye shughuli nyingine za maendeleo. Hivyo ni muhimu kwa Serikali kubadili sera zinazopelekea migomo na vurugu vyuoni.
[IMG]file:///C:\DOCUME~1\ADMINI~1\LOCALS~1\ Temp\msohtmlclip1\01\clip_imag e002.jpg[/IMG]Hawa niwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Kampasi ya Mlimani wakiwa nje namizigo hawajui waelekee wapi baada ya chuo hicho kufungwa gafla mwaka 2008
MIGOMO VYUO VIKUU NCHINI.Serikaliisikilize hoja badala ya kupinga na kutumia nguvu za polisi
[IMG]file:///C:\DOCUME~1\ADMINI~1\LOCALS~1\ Temp\msohtmlclip1\01\clip_imag e002.jpg[/IMG]Polisiikitumianguvu kuwatawanya wanafunzi Chuo kikuu cha Muhimbili baada ya kuitishamgomo wa kushinikiza utawala kurudisha serikali yao.(MUHASO)
Chuokikuu cha Dodoma- UDOM walipogoma kushinikiza hoja zilizo wazi kabisa za kuwekokwa mafunzo kwa vitendo walipikwa mabomu. Mtoto wa mkulima waziri mkuu MizengoPinda alikwena huko na kukiri kuwa wanafunzi walikuwa na hoja za msingi,akaagiza ishughulikiwe. Wanafunzi wa UDSM tuliandamana kudai nyongeza zakujikimu,kwa siku,tukapikwa mabomu. Mawaziri Mh shukuru kawambwa wa elimu na Mh.Shamsi Vuai Nahodha,jumaosi wakakutana na menejimenti ya chuo na wawakilishi wawanafunzi na kukiri kuwa madai ya wanafunzi ni ya msingi. Hata tukajiuliza je? serikali ni lazima ipige watu wake mabomundipo itambue uzito wa madai yao ya msingi?
kutoa maoni yao na matatizo yanayowasibu kuhusu Mfumo wautoaji wa mikopo ya Elimu ya juu. III. Vigenzo vilivyowekwa na bodi ya mikopo katikakuwatambua wahitaji sahihi wa mikopo vimeshindwa kuweka wazi au kumtambuamhitaji halisia wa kupewa mkopoTOFAUTI ZA GREDI. [MEANS TESTING] Hili limekuwa tatizo lamuda Mrefu tangu kuanzishwa kwa utaratibu mpya Mwaka 2005 wa kuwakopeshawanafunzi mikopo kwa ajiri ya masomo yao ya elimu ya juu kupitia bodi ya mikopoTanzania (HESLB) katika Mfumo wa (tes Means).Tunaomba ifahamike kwamba mfumo huuumekuwa hauna uhalisia katika kugawamikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu hasa katika kigezo cha uwezo wa kiuchumiwa familia Mwanafunzi hivyo kutoa mkopo kwa kuangalia uwezo wa kiuchumi kwakuangalia mambo yafuatayo. I. Shule nilizosoma za sekondali kwa kuangalia kiasi chaada (fees) ya shule ilikuwa kiasi gani Madhaifu ya Kigezo hiki. II. Naomba ifahamike kwamba kutokana na uchache wa shule zasekondari za serikali wazazi hulazimika kuwapeleka watoto wao shule binafsibaada ya serikali kuchagua idadi chache ya wanafunzi hasa wa kujiunga na kidatocha tano. Kutokana na uchache wa high school hivyo wazazi hulazimika kuwapelekashule binafsi hata kama hawana uwezo. III. Tunaomba ifahamike kwa serikali kwamba baada ya matokeoya kadato cha nne kutoka kila Mwaka. Huwa wanafunzi wanafaulu kwa viwangoTofauti kuanzia daraja la kwanza, daraja la pili, daraja la tatu na daraja lanne. Mara nyingi serikali huwa inachaguawale waliofaulu kwa daraja la kwanza, na la pili na
IV. daraja la tatu. Hivyo huwa kuna wale daraja la tatu nala nne na ambao halazimika kurudia mtihani kutafuta (credit) kama hazikufikahawa wote hulazimika kwenda shule za binafsi sio kwa sababu wana uwezo wakifedha bali hawakupata nafasi serikali hivyo familia nzima, ndugu na jamaahulazimika kutoa mchango ili hawa wanao au watoto wao waweze kupata elimu. Hivyo Serikali hapa ikichukuwa kigezo cha adaya shule aliyosomea mwanafunzi huyu itakuwa haijamtendea haki kwani alilazimikakwenda pale baada ya kutokuwepo uwezekano wa kupata nafasi kutokana na sababuhizo. V. Kigezo au utaratibu wa kusainisha fomu za bodi yamikopo kwa wanafunzi wanaenda kuanza mwaka wa kwanza elimu ya juu. Naombaserikali ifahamu kuwa taarifa zinazoandikwa kwenye fomu hizo hazina uharisia naukweli wa hali halisi ya maisha,ya mwanafuzi hili naomba niwe Mzalendo wa nchiyangu Tanzania na kuhurumia kodi za walala hoi. Kwa wanaohusu kuhakiki taarifazilizoandikwa kwenye fomu ya kuomba mkopo ni katibu kata, na Afisa mtendaji wakijiji na kata pamoja na wajumbe watatu (3). Lakini nimeshuhudia wanapopelekewa fomu hizo huomba kuonyeshwa eneo lao lakusaini bila kusoma taarifazilizoandikwa. Na baadae taarifa hizo hutumwa bodi ya mikopo elimu ya juu.nahizo ndizo taarifa zinazotumiwa kupanga magurupu ya mikopo wakati taarifa hizohazina uharisia wa maisha ya manafunzi fumilia yake. VI. VIPAUMBELEVYA SERIKALI KWA BAADHI YA KOZI. MfanoElimu na Sayansi vinaacha Matabaka na Athari kwa jamii ya watanzania maskinihivyo tunapinga mfumo wa vipaumbele vya Serikali kwa hoja kuntu zifuatozo:- a) Nchi yetu bado inahitaji wataalamu wa fani mbali mbaliili kukuza uchumi wa nchi yetu na mendeleo ya familia zao kwa jumla.b) Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zipo kwenyemchakato wa uanachama wa shirikisho la Afrika Mashariki. Ambapo nchi yetuhaiwezi kunufaika katika shirikisho hili kama haina Rasilimali watu hususanikatika soko la Ajira. Hivyo tunaitajiwataalamu wa fani mbali mbali ili tuweze kunufaika na shirikisho hili kama wanauchumi, wanasheria, wataalamu wamambo ya kijamii (Sociology, Psychology,HumanResources,poli tician,naBiashara,Wahasibu,(AC COUNTANT).Lakini kama serikali itaendelea na msimamo wa vipaumbele vyake vya Elimu naSayansi tu. Wataalamu hawa wa fani hizi ngingine tutawakosa kwa asilimia kubwa. c) Serikali kuweka vipaumbele vya Elimu na sayansi tu nakwenda kozi nyingine kuna athari kubwa ya kuathiri vipaji vya wanafunziwanaotoka familia maskini. Kutokana na hali ngumu ya maisha wanafunzi wanotokakatika familia Maskini watalazimika kuchukua kozi ambazo serikali Imezipakipaumbele Elimu na Sayansi na sio kuchagua kozi kulingana na vipaji vyao(Talent and Ambition) na kuharibu (future) zao. Hivyo Taifa linaweza kujikutalinazalisha wataalam ambao wamesomea kozi au fani ambazo sio vipaji vyaokutokana na umaskini wao. Kitu ambacho kinaweza kuwa hasara kwa Taifa kwaniwatashindwa kufanya kazi kwa ufanisi. d) Wanafunzi watakao chaguliwa kozi tafauti na vipaumbelevya serikali Elimu na Sayansi na wanaotoka katika familia Maskini watashidwakuimudu gharama ya Elimu ya juu ili hali wana sifa zote za kusoma Elimu ya juu(chuo kikuu) na hili ni hatari kwa Taifa ambalo wananchi wake bado ni Maskini e) Serikali kuweka vipaumbele kwa baadhi ya fani na kuachanyingine katika Elimu ni kukiuka katiba ya jamhuri ya muungano wa TanzaniaIbara ya 11 sehemu ndogo ya 2 na 3 kama inavyosema kwenye katiba. 11. (2) “kilamtu anayo haki ya kujielimisha, na kila raia atakuwa huru kutafuta elimu katikafani anayopenda hadi kufikia upeo wowote kulingana na stahili na uwezo wake.”Ibara ya 11. (3) inasema “Serikaliitafanya jitihada kuhakikisha kwamba watu wote wanapata fulsa sawa na zakutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote zashule na vyuo vinginevyo vya mafunzo.” Vi. Pesa za kujikimu (BOOM) kutolewa vyuonibadala ya bodi ya mikopo (HELSB) Sisikama kamati ya wanafunzi pamoja na wadaumbalimbali Wanaona mapendekezo hayo na utekelezaji wake ni mgumusana na unaitaji kufanyiwa marekebisho mara moja kwa sababu zifuatazo:- i. Utaratibu huu utasumbua Mwanafunzi na kumpotezea mudawa kuondoa hali ya utulivu wa masomo kwa mwanafunzi asiyekopeshwa na bodi.Kwani uwezekano wa chuoni kugeuka sehemu ya kudai pesa na sio kusoma ni mkubwakama tulivyoona baadhi ya vyuo kwa sasa (UDSM, MT. JOHN).
MAPENDEKEZO YETU KWASERIKALI1) Tunakuomba sana mheshimiwa Rais pamoja na waziri wa Elimukwa mamlaka uliyonayo mh. Rais ya kikatiba ibara ya 45 kipengele kidogo Cha 1, a,b,c na d utoe msamaha kwa wanafunziwote zaidi ya 900 waliosimamishwa masomo, waliofukuzwa vyuo na walewaliofunguliwa Kesi mahakani ili kuepusha migogoro inayiweza kujitokezakwa wanafunzi kushinikiza utawala vyuo na serikali kuwarudisha wenzetuVyuoni kwani wao pia wanahaki ya kupata elimu kamawatanzania Wengine. 2) utaratibu wa utoaji fedha (boom) za wanafunzi urejeshwebodi ya mikopo [HESLB]ili kuondoa na kuepusha vurugu zilizoanza kujitokeza katiya wanafunzi na utawala wa vyuo vikuu .pili itasaidia kuondoa wizi [ufisadi]ulipoanza kujitokeza kutokana na pesa kupelekwa vyuoni kwa kuingiza majina hewaya wanafunzi .mfano .kamati ya bunge ya hesabu za mashirika ya umma[poac]imebaini wizi wa sh.miliomi 66 katika chuo kikuu cha mkwawa baada ya kubaini majinahewa ya wanafunzi 32. ambayo yalikuwa yanafanana mwanzo na kufautiana mwishoyakiwa na saini halali za wanafunzi yakionyesha kupewa mikopo 3) bodi ya mikopo ifanyiwe mabadiliko ya uongozi ikiwa nipamoja na kufanywa marakebisho ya sheria zinazoipa nguvu bodi ya mikopo [HESLB]ya kubadili na kufanya mabadiliko ya sera mara ya kwa mara kwa wanafunzi waelimu ya juu nchini 4) Uanzishwe utaratibu mpya na bodi ya mikopo kuajirimaofisa mikopo kila chuo kikuu ili wawe kiunganishi kati ya bodi mikopo na chuohusika na kupereka taarifa muhimu Bodi ya mikopo kwa wakati. 5) ofisa mikopo chuoni atakuwa na jukumu la kuakikishamajina ya wanafunzi halisi ambae amesajiriwa na chuo na anatakiwa kupewa mkopona kubaini wale waliopoteza sifa za kuendelea kupewa mikopo katika muda muafakamfano mwanafunzi akifukuwza chuo mwanafunzi akisimamishwa masomo kwa mudafurani mwafunzi akifeli masomo [discotinuty] na mwanafunzi akifariki afisamikopo atatakiwa kutuma taarifa bodi ya mikopo ili akaunti ya benki ifungwemara moja. 6) Ofisa mikopo chuoni atatakiwa kusainisha majina yawanafunzi na kuyatuma bodi ya mikopo kwa muda muafaka ili kuondoa tatizo laucheieshwaji wa pesa wanafunzi kutoka bodi ya mikopo kwa kusingizia Eti chuokichelewesha majina bodi ya mikopo saopo kwa kushirikiana n utawara wa chuohusika watamsaidia kumpatia taarifa muhimu kuhusu wanafunzi kwa muda muafaka 7) Ofisa Mikopochuoni atawajibika iwapo mgomo au vurugu zitatokea chuoni kwake napofanyia kazikwa sababu ya uzembe wake hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake ikiwa nipamoja na kusimamishwa kazi mara moja. 8) Kwa kuwaimezoeleka kila inapotakiwa kuongezwa pesa ya kujikimu na malazi kwa wanafunzi wa elimu ya juu iliziendane na hali halisi ya maisha ni lazima wanafunzi wagome na kuandamana ndiopesa hiyo iongezwe kama turivyoonyesha mwaka 2008 kutoka sh3500 hadi5000mwaka 2011 kutoka sh 5000 hadi7500/= Tunashauri na kupendekeza serikalinikiundwe chombo Maalum ndani ya wizara ya elimu kitakacho kuwa na jukumu kutathiminina kufanya tafiti ya hali halisi yagharama ya maisha na pesa wanayokopwa mwanafrunzi elimu juu ili kufanyamaboresho kwa kushauriana na wizara fedha na hazina ya Taifa na sio kusubiriwanafunzi wagome na kuandmana ndio pesa iongeze wakati wanafunzi wanafukuzwavyuo na kusimamishwa masomo kwa madai eti walikua vinara wa migomo hiyo na niaibu kwa nchi yetu inayo hubiri sera ya utawala bora kusubili migomo namaandamano ndiyo inatekeleza madai hayo itakua haina maana.9) Tunaombautaratibu wa kujaza fomu ya bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu juu urejeshwengazi ya wilaya kila wilaya kupitamkurugenzi wake au afisa elimu wilaya utaratibu huu utakuwa na faidazifuatazo:- i. Utaratiku huu utasaidia selikali kutambua uwezo wamwafunzi kiuchumi na kumpa asilimia na gredi zinazostairi kwa mwafunzi nakuondoa vigezo vinavyo tumiwa na bodi ya mikopo ambayo havina ukweli ndani yakekama kigezo cha shule aliyosoma mwanafunzi kwani wanafinzi wanaoludia mitihani na ambayohawachaguliwi na selikali kidato chakwanza na kidato cha tano hulazimika kwenda shule binafsi. ii. Utaratibu huu mpya utasaidia selikali kufuatiliaurejeshwaji wa mikopo kwa wanafunzi wanapoanza kazi baada ya kuhitimu masomoyao. Zoezi ambalo litakuawa jepesi kwa wilaya kufika kwenye familia ya mdaiwawa mkopo au kufanya mawasiliano na familia yake. iii. Utaratibu huu utasaidia serikali kupitia wilaya kuwa narekodi [DATA BASE] ya wanafunzi walioko vyuoni kila wilaya na kuandaa utaratibuwa kuwatumia [ajira] watakapohitimu masomo yao chuoni. iv. utaratibu huu wakutumia wilaya utasaidia kuondoa upendeleo, kujuana, rushwa, wizi na ufisadiuliomo ndani ya bodi mikopo [HESLB] nchini kwa kuingiza majina hewa yawanafunzi kwa kujuana na kupokea rushwa kwa kuwapa mkopo na asilimia kubwawatoto wa vigogo (matajiri) huku wanafunzi wanaotaoka familia maskini wakikosamkopo (No loan) au kupewa asilimia ambazo hawastahiki. Tumeshuhudia ofisa waBodi ya mikopo Esther Budili akifikishwa mbele ya Hakimu mkazi kisutu jijiniDar es salaam kwa tuhuma za wizi wa sh.Millioni 90 baada ya kughushi majina ya wanafunzi na watumishi katika vyuo tisanchini. v. Utaratibu huu utasaidia wanafunzi kutoa na kupeleka malalamiko yao ngazi yawilaya kama itatokea kupewa asilimia ndogo ya mkopo (%) ambayo haiendani nauhalisia wa familia ya mwanafunzi kiuchumi ili afanyiwe marekebisho ngazi zawilaya na kutumwa Bodi ya mikopo. Maana mara nyingi inatokea ndugu wa familiamoja waliosoma shule moja na wamefaulu madaraja sawa. cha ajabu na kushanghaza wanapata asilimia tofauti za mikopo (%)haingii akilini. 10) Mkataba(fomu) uwe wazi kwa mkopoji: mkataba kati ya Bodi ya Mikopo na mwanafunzi waElimu ya juu uwe wazi ili ajue vizuri masharti ya mkopo anaokopa Mfano: ni mudagani atatakiwa kurejesha mkopo baada ya kuhitimu masomo yake ya chuo kikuu naatarejesha kwa nani kupitia njia gani ni muhimu viwekwe kwenye fomu ya kujazakwa ajiri ya mkopo. 11) Serikaliingie mkataba na Benki hapa nchini ili zitoe mikopo kwa wanafunzi wenye ajira tiari (inservice) chiniya udhamini wa serikali na utaratibu wa mkataba wa Benki na Mwanafunzi utumike mkataba wa Bodi ya mikopo(HESLB) ili kuepuka Riba na usumbufu unaoweza kujitokeza baada ya serikali kujana sera ya kutowapatia mikopo kupitia Bodi ya mikopo (HESLB) 12) Serikaliifungue akaunti Maalum ya Bodi ya mikopo kwa ajiri ya wanafunzi wa elimu ya juukuondoa ukiritimba wa ucheleweshaji wa pesa kutoka Hazina kwenda Bodi yamikopo. Pia Bodi ya mikopo iingie mkataba na Benki nyingine kama NBC, NMBkuliko kutegemea kupitisha pesa kwenye Benki moja ya (CRDB) pekee na CRDBkusambaza taratibu kwenye Benki nyingine kitendo ambacho hufanya wanafunziwenye akauti tofauti na CRDB kuchelewa zaidi ya siku 5 hadi 7. kupata pesa zaohuku wa CRDB washapata tiari na kuleta vurugu. 13). Tunaiomba serikali kupitia wizara ya Elimu iundechombo maalum au kupitia (TCU) chakulatibu ada ya Elimu ya juu vyuo binafsi na shule binafsi ili kuondoaukilitimba wa kibiashara katika elimu na kutoa fursa kwa jamii maskini nao wapateElimu. Hivyo tunaiomba serikali iliangalie suala hili kwa jicho la huruma naumakini sana. Kama Serikali iliona umuhimu wa kuundwa vyombo kama Ewura,Sumatra kwenye mafuta,maji gesi, na usafiri ni wakati mwafaka kuundwa chombokitakachosimamia Elimu na Ada (fees) shuleni hadi vyuo vikuu ndani ya Wizara yaElimu na Mafunzo ya ufundi 14).Tunaiomba Serikali isiingilie Jumuiya na Serikali zawanafunzi pamoja na vyama vya siasakupandikiza vibaraka wao kupitia uchaguzi wa serikali na jumuiya hizo piatunaiomba Serikali iziache serikali za wanafunzi zijiendeshe zenyewe kwa mujibuwa katiba zao na sio za Magembe (GN) Serikali iwape itupe uhuru wa kujiongozawenyewe kwani hakuna Taasisi au Jumuiya za watu ambazo Serikali ilizitungiakatiba za kujiongoza. Huu ni unyanyasaji uliovuka mipaka ya haki za binadamu. 15). Kuhusu uhaba na uchache wa hosteli vyuo vikuu hapanchini. Tunaiomba Serikali iandae mpangomkakati wa ujenzi wa hosteli za kutosha vyuo vyote vya umma na kushinikiza vyuoBinafsi navyo kufanya hivyo katika Bajeti ijayo mwezi wa saba 2012/2013 kupitiawizara ya Elimu na Mafunzo ya ufundi. Pia tunaishauri Serikali ili mpango huuwa ujenzi wa hosteli vyuo vikuu ukamilike kwa haraka na kwa ufanisi ni muhimuSerikali iingie mkataba na Taasisi za hifadhi ya kijamii kama NSSF, PPF, LAPF,GEPF, PSPF. Au Wakala wa nyumba (TBA) na Benki hapa nchini. 16. Tunaiomba Serikali iandae utaratibu wa harakawa kuboresha na kujenga Miundombinu mpyaitakayoendana na ongezeko la wanafunziwa elimu ya juu kama madarasa, kumbi za mihadhara n.k.OUR ADVICE TO THE ADMINISTRATORSOF DODOMA AND DAR ES SALAAM UNIVERSITY Constructive administrativedecisions should be applied beyondreasonable doubts by administrators in University when dealing with studentsdemands in their learning process.Itsan embarrassing situation seeing Vice Chancellors and their administrative associates failing to givehelpful decisions in settling problems facing students. In most cases, theirdecisions effect students and the country as whole. Since 2008, the University of Dar esSalaam (UDSM AND UDOM) faced riotsalmost in very year, a situation compelling the public to question what iswrong with the oldest University in theCountry.Atthe end of 2011, students at Mwalimu Nyerere Campus were at demonstration demanding for their right toaccess loans tuition fees, meals and accommodation allowances.Unfortunately,the UDSM and UDOM administration underthe leadership of the vice Chancellors, Prof. Rwekaza Mukandala and prof IdrisKikula targeted only 48 students in udsmand 670 in udom who were reveled that the administration had no proof tosubstantiate that the expelled students were the real instigators of thestrike.Outof the total number of expelled students, some submitted their appeals to be reinstatedwithout fruitful results.Toget a true picture of the problem has become difficult since the relevant man to do anassessment is the Vice Chancellors themself, Prof. RwekazaMukandala and prof Idris Kikula who hasbecome elusive to give more light to the predicament. Itonly reffects his negative attitude on people and failure to be accountable to the public members whohe sworn to defend and promote. If the VC is such a busy man then he doesn’t qualify tolead such an important institution. No wonder he doesn’t care about studentsproblems thinking that they are a nuisance while in reality are the ones whohave made him occupy such a position.TheAfrican reporter submitted enquiries to the Vice Chancellor about students matters but the didn’t neither answer thequestions nor delegate the responsibility to his assistants!Leadersshould learn to delegate power and notmoving with office keys in their pockets. Increase team working spiritparticularly in educational institutions. Frequent meeting are instrumental tools inrunning any institution educationinstitutions included. The meetings aim at reviewing and analyzing what theinstitution have accomplished to be ac-completed and developing plans and strategies for future.Itwas wonderful as professors sat-down to solve the issue of students loans but they finally came out withthe recommendations to expel the students for good.Ithink they are confused since the decision is arbitrary, excessive and parochial in nature lackingdemocratic elements and void of compassion.InApril 17- 24-2008, UDSM there was a tag of war between the students and the administrationfollowing the suspension of some students. The suspension caused students toboycott classes pressing the administration to reinstate the suspendedstudents.Atthat time DARUSO President Deogratias Daudi said “We held the meeting with theadministration to iron out the problem but the administration remained stiff and uncompromising.”Analystsquarry on what is the probem behind UDSM and UDOM students strikes failing to knowwhether Prof. Mkundala’s administration and Prof Idris Kikula’sadministration has failed to run theUniversities or is the problem of the students themselves as since 2008students have not stopped boycotting udsm. And which start udom.Moreover,the field Force Unit (FFU) Kinondoni was deployed under regional Police Commander Jamal Rwambowesaid, “we had received the names of 16suspended students as ring leadrs whostared rioting since February 2008 due to water short age”.The2008 demostration caused the death of one student named Dominic Deogratus due to chaos at theUniversity.UDSMand UDOM leadership needs to learn from other Universities with in and outsidethe country regarding that Professors are the main advisors of the state. Thereis a belief that their decisions are above the bar.Itcould be wise for them if they cant handle students to put down the tools and pave the way forothers to take over. It is not good to rule the institution by using your ironhand and out od political dichotomy. In 2008, further demonstrations took placeat the some University during theelection for DARUSO leaders. One of the contestants for the presidential postOdong Odwar was stoped from contesting by the administration. He was givenstiff conditions to prove his legality being at the campus. But how a student’s legality resurfacesduring the election. Further in vestigations revealed that it was a politicalinfluence.DrKenneth Blanchard, Ph.D. and Spencer Johnson, in their book gave tips on management once toseek for advice how to manage the institution. The young man found “a one minutemanager” in the office. In thediscussion, the manager took the young man to stand at the window lookingoutside.Theyoung man was asked how many foreign cars were along the road. The young man said “I see more of themevery day” The managers asked him why people buy foreign cars. Is it becauseour country did not make enough cars? Or because the did not make the qualitycar the public really wanted?Theyoung man said it was a question of quality and quantity. The manager added quality is simplygiving people the product or service they really want and need.Productivityis about both quantity and quality. And frankly,the best way to achieve both of theseresults is through people. The young mans face showed surprise. He had neverheard of a One Minute Manager”.Therefore,from this parable, one can imagine, what kind of students do Universities in Tanzaniaproduce. Do universities produce bothquality and quantity graduates? What kind of leadership do the learninginstitutions needs?Howcould they produce both, if the management, administration and leaders do not clearly showthe commitment to give quality and quantity education in the country?Ofcourse we have profession, well respected but we don’t see tangible managementexamples geared to improve education in the country.Platoadvocated about education by insisting that children suitably gifted are to be trainedby the state so that they may be qualified to assume the role of a rulingclass. The idea or theprinciple of Plato goes almost differently or against some of the Professors inthe Higher learning Institution like UDSM and UDOM that want them to be puppiesand men!Butobviously the students who were, sent home are the losers since they don’t learn anymorewhile the Professors are working and getting more salaries. Will the countryproduce quality and quantified graduate?Whatdo the University of Dar es Salaam and University of Dodoma, the Ministry of education and thestate of Tanzania think about this to wards the common tendency of expellingstudents?Forexample, it was revealed that studentsfrom UDOM this year submitted appealcases before the dean of the students to be presented to the vice Chancellorfor review same to UDSM.Unfortunately, they were kecked out.JeanPiaget the Philosopher placed great value of education in children. He declared in 1934that, “ only education is able to save our societies from possible collapse,whether violent, or gradual. He described children as little scientists seeingthem active. Professors must learn from them from these living examples.Thesegreat Philosophers differ in opinion with current Professors at the University of Dar es Salaamand University of Dodoma and other Higher learning Institutions as they fail tocapitalize on students potentials buy handling problems hampering smoothlearning environment. Professors have read a lot about psychological,administrative, leadership, philosophical books and done researchers how theycould discipline the old and the young people in different. So we expect themto be capable of accommodating the situation.Despitehaving all the required knowledge, they resorted into dismissing students with limitedevidences showing their participation in instigating riots. They just “believedthat the expelled students were involved in the strike with limited proof.Although they could be found with some mistakes or errors, the Professors hadto give alternative punishments including being enrolled in other Universities.Ibelieve that UDSM and UDOM administrators have read about Mason, a British educator who invested her life in improving the quality ofchildren’s education. The problems with most ofacademicians in Tanzania is that they engage themselves more in politicalmatters, to prepare themselves to feature in to politics after retiring fromthe public services. In this way, they keep their commitments open and thusruining the education sector unnoticing.Masonsphilosophy of education was probably the best. He said “Education is anatmosphere, a discipline, a life” and “Education is the science of relations”.Professors could not teach students educational relationships. That failureindicates that Professors decisions bear some shortfalls.SheMason) believed that children were born persons and should be respected as such; theyshould also be taught the way of the will and the way of Reason. “I ought, Iwill”. Therefore, professors should embrace such charisma. Students by laws donot allow expelling any student without watertight evidence. How did they comewith the sloppy decision?Locke(1632-1704) had some thoughts concerning education. He expressed the beliefthat education makes the man. He said “I think I may say that of all the menmeet with, nine parts of ten are what they are, good or evil, useful or not, bytheir education”.It is interesting to note that University Professors are atthe forefront to prove to the world the administrative principle lapses and howto run companies, national economy as consultants and advisors of thePresident! But they miserably fail to solve loan problems for 14,000 studentsin the country.Thisis the reason why Locke said “I think a may say that of all the men we meet with, nine parts of ten are what theyare, good or evil, usefully or not, by their education”. There is a saying inthe philosophy of education which states that Perenialists believe that one should teach the things that onedeems to be of everlasting importance to all people everywhere.Theybelieve that the most important topics develop a person. This is what thestudents need to get from professors. Instead our professors chase the studentsfrom colleges. Are the developing the country or destroying it?Thesame students receiving incomplete education at UDSM and UDOM are the ones whowould work at Bank of Tanzania to produce fake and substandard bank notes thatare significantly ruining our economy.Thegovernment under President Kikwete pledged to provide free education to allprimary school pupils and after loans to Higher Education students. Butstudents every year go on rampage demanding their loans while they qualified tojoin Higher Education institutions.Itwas received about 14,000 students did not receive loans a reason thattriggered for a massive demo.Amongthe priorities declared by president Jakaya Kikwete after he was elected tobecome a president was strengthening the education sector. He said “ we willstrengthen the higher education students loans Board so that it can offer itsservices to more people.Some students were quoted as saying “we went on rampageafter the Minister for Education and Vocational Training, Dr, ShukuruKawambwa told us that to loan board hadreached its maximum limit of offering loans while majority students were notallocated.TheRetired Secretary General of the UnitedNations Kofi Annan once said “todays real borders are not between nations, butbetween powerful and powerless, free and the fettered, privileged and thehumiliated”. The conflicts that students in particular and the public at largefacing right now, is because they are powerless.Theyare powerless because they are poor, they are poor because they are noteducated, and most of them are not educated because they share certainpolitical views. The powerful people in Tanzania are the ones with education,money , or have some connection with an eminent political figure.Thisis were the border is created between the rich and the poor, educated and uneducated.Poverty isone of the major reasons for the rising crimes rate in may developing countriesTanzania included. There fore the expelled students from UDSM and UDOM willfollow track to become rebels if not handled with care because of in-conclusiveand not constructive decisions made by the Universities administrators incollaboration with some politicians.It is our hope that the president awareabout the expelled students because of demanding loans as per his statement. Inthat regard we are waiting for his statement on this important matterthat would reflect what he said when hewas first elected to lead Tanzanians. USHAURI WETU KWA MWESHIMIWA RAIS WAJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIASisikama wasomi (intellectual) tumeona ni vizuri kutumia nafasi hii kukushauri Raiswetu katika harakati za kuongeza kasi ya Maendeleo ya uchumi ili kupunguzaumasikini kwa Watanzia. Mheshimiwa Rais Mojawapo ya mambo makubwakatika Awamu ya nne ni msukumo mpya wa kuendeleza kilimo. Tumeshuhudia bajeti ya sektaya kilimo ikipanda kutoka asilimia 3 ya bajeti kwa mwaka 2001/2002 hadi kufikiaasilimia 7.8 mwaka 2010/2011. Pia ruzuku imepanuliwa kutoka kwenye mbolea pekeyake hadi kwenye pembejeo zingine kama mbegu na zana za kilimo.Kwamatokeo yake fedha zinazokwenda kwenye ruzuku zimeongezeka kutoka shilingi billion 2 mwaka2003/04 (sawa na asilimia 1.3 ya bajeti ya kilimo.MheshimiwaRais chapisho la mpango huu linaonesha kwamba lengo kuu katika sekta ya kilimoni kufanya kilimo kuwa cha kisasa, cha biashara na chenye tija kubwa.Katika andishila kilimo kwanza imeonyeshwa waziwazi nini kifanyike lini na nani. Wasiwasiuliopo ni kwamba chapisho la kilimo kwanza ni chapisho kama yalivyo machapishomeni hapa nchini yenye lengo la kuendeleza sekta ya kilimo mfano: Dira la Taifa ya Maendeleo 2025, MKUKUTA,Mini – Tiges Plan, ASDP, AMSDP, MKURABITA, na sera mbalimbali. Kama sio Mwenyeji wa Tanzaniaukisoma ahadi zilizomo katika machapisho haya hasa kuhusu kilimo cha wakulimawadogo utadhani nchi itaendelea kesho.Lakinimtu mwenye akili husu akipitia mpango huu kwa makiniharaka sana atagundua kwamba hakuna kitu ambacho unaweza kukiita “ubunifu”katika mchakato mzima wa utkelezaji wake ili kuweza kutoafautisha mpango huu namipango mingi iliyotangulia na kushindwa-maneno, ahadi na mbinu ni zile zile.Kunamashaka sana kwamba mpango huu utafanikiwa kwa sababu unadai utatekeleza mamboyote kwa miaka mitano ambayo tumeshindwa kuyatekeleza katika kipindi cha miaka50! Mpango hauelezi tumekuwa tukikosea wapi na umewekwa mkakati gani kukwepamakosa hayo katika kutekeleza mpango huu. Kwa ufupi hakuna ubunifu katikautekelezaji wa mpango huu. Ila ubunifu kidogo unajitokeza katika kutafuta fedhaza kugharimia mpango wenyewe.MheshimiwaRais ikumbukwe kwamba si kweli kwamba Tanzania haiendelei kwa kukosa mipangomizuri, fedha, wataalam. La hasha. Nchi ina ugonjwa sugu wa kushindwakutekeleza mipango yake ya dhati kwa sababu mbalimbali kama ubadhilifu nakutowajibika kwa watendaji. Machapishoyanaonyesha kwamba mpango huu utagharimu shilingi trilioni 37.3, kati ya hizoshilingi trilioni 3.8 sawa na karibu asilimia 10.3 ya bajeti yote zitatumikakwenye sekta ya kilimo.Hiini fedha nyingi sana na ni mfano mzuri wa kulenga mbali tulikoongelea mwanzonimwa mada hii, na hatuna shaka kwamba fedha hii inaweza kupatikana lakini kwa vilembinu za utekelezaji zitakuwa zilezile zilizozoeleka na watu ni walewalenatabiri (hypothesize).Fedhayote hii itaisha na sekta ya kilimo itakuwa na matatizo yale ya miaka yote,ambayo ni pamoja na : kutegemea huruama za mbingu kuleta mvua; ukosefu wamiundombinu ya kusaidia uzalishaji na usambazaji; mfumo dhaifu wa utafiti nauhgani; matumizi hafifu ya pembejeo na zana za kisasa; kukosa mfumo madhubutiwa mikopo kwa wakulima wadogo wadogo; mfumo duni wa usambazaji wa pembejeo;matumizi ya mbegu duni za mazao na wanyama; kiwango kidogo cha usindikaji wamazao ya kilimo; kukosekana kwa mfumo madhubuti wa matumizi ya ardhi;kuathiriwa na hali ya hewa pamoja na soko la uhakika la mazao yao.MheshimiwaRais haya ni mapendekezo yetu kuhusu sekta ya kilimo ili kurekebisha makosaambayo tumekuwa tukiyafanya ili kuhakikisha Mapinduzi ya kijani Tanzania:- Kwa kuzingatia changamoto na matatizoyanayokwamisha ya serikali yako ya nne ya kilimo kwanza. Tunapendekeza liundweBaraza la ushauri la kilimo (National Agricultural Advisory council) (NAAC)wajumbe wa baraza hilo wateuliwe bila kujali mwelekeo wao wa kisiasa au kazizao. Wajumbe wa baraza hilo wawe ni wataalam waliobobea kwenye kilimo ambaohistoria ya matendo yao (track record) inaonyesha mapenzi na uwezo mkubwa wakuchambua changamoto zinazokabili sekta ya kilimo.Kuwana cheo kikubwa serikalini au msomi wa masuala ya kilimo kisiwe kigezo cha kuwamjumbe wa NAAC. Mjumbe anaweza kuwa mfanyabiashara, mkulima, mfanyakazi waserikali, mwanasiasa, au mtu binafsi ili mradi awe na uelewa wa kutosha narekodi inayoweza kuthibitishwa ya uwezo wake wa kuchambua vikwazo vya sekta yakilimo.Usalamawa Taifa unaweza kusaidia upatikanaji wa wajumbe hao kwa mtindo ule ule ambaowa Mwl. Nyerere alikuwa akitumia kuwapata viongozi. Baraza hilo lipewe jukumula kufikiria kwa kina, kwa niaba ya watanzania wote, changamoto mbalimbalizinazokabili kilimo na kupendekeza mipango ya kukabailiana nazo. Ikiwezekanawapewe uhuru zaidi ya kuwa visima vya fikra (think tank) za maendeleo ya sektaya kilimo.Hapahatupendekezi kitu kama mabaraza ya ushauri ya mikoa au wilaya (Regional andDistrict consultative councils – RCC and DCC) ambazo ujumbe wa mtu hutegemeacheo cha mtu pale mkoani au wilayani. Kuwana cheo hakuna uhusiano wa moja kwa moja na uwezo wa kufikiri kwa kina wamhusika; mara nyingi hutemea uhusiano wa mteuliwa na mteuaji. Bila ya kuwa nachombo kama hiki, maamuzi magumu kuhusu mwelekeo wa sekta ya kilimo yanaachwamikononi mwa wanasiasa wakiongozwa na mapenzi yao, ambayo mengine yanaweza kuwayameathiriwa na Rushwa, kujuana, kutowajibika n.k.Mapendekezoya NAAC yawe yanawekwa hadharani kwa wadau mbalimbali (kwa nkia itakayo kuwainapendekezwa) ili kujadiliwa na kuwa na umiliki wa mpango wowoteutakaotekelezwa. Kwa njia hiyo Tanzania ianweza kuwa na mipango yake mwenyewekuliko hii ya sasa ya kukata na kubandika kutoka kwa wengine. Kuanzishwa kwa(NAAC) kwende sambamba na kuanzishwa kwa baraza dogo la Mawaziri (Mini Cabinet)ndani ya baraza kubwa la Mawaziri. Mawaziri wa Mini Cabinet wawe ni walewanaoongoza wizara zinazohusiana na uzalishaji na kukua kwa uchumi.Kwamuundo wa bara la mawaziri la ssa wanaweza kuwa Waziri Mkuu, Waziri waTAMISEMI, Waziri wa kilimo usalama wa chakula na ushirika, Waziri wa Maendeleoya mifugo na uvuvi, Waziri wa fedha na uchumi, Waziri wa ujenzi, Waziri waviwanda na Biashara, Waziri wa uchukuzi, Waziri wa maji na umwagiliaji, Waziriwa uwezeshaji na uwekezaji na Waziri wa kazi vijana na Ajira. Hawa wanawezakuwa wanakutana kupokea mapendekezo ya (NAAC) kupanga utekelezaji wa mipangoilipendekezwa na NAAC.Lakiniyatosha tu kusema pendekezo la kuundwa kwa Baraza la ushauri la kilimo linawezakuzaa matunda iwapo kutakuwepo na utashi wa kisiasa wa kweli na mawazo yakimapinduzi ya kijamii.MheshimiwaRais wananchi wako wanateseka na mfumuko wa bei za bidhaa uliofikia asilimia 20sasa. Watanzania wengi wameshindwa kumudu gharama za maisha huku tukiambiwauchumi wetu unaendelea kukua. Hivi huku kukua kwa asilimia za uchumi wakatiwananchi wengi wanakabiliwa na ugumu wa maisha kuna maana gani. Hivi kipi ni sahihi; kasindogo ya kukua kwa uchumi inasababisha walio wengi kuwa masikini au umsikini wawalio wengi kuwa masikini unasababisha uchumi kukua kwa kasi ndogo? Ingawajeswali hili linaonekana kuwa jepesi, lakini ni la msingi mno katika kutafutasuluhisho la kasi ndogo ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu. Kwa mtu ambaye haelewi maana ya kukua kwauchumi anaweza kuwa na shida ya kupata jibu la swali hilo.MheshimiwaRais tuanze kwa kueleza maana kukua kwa uchumi. Kukua kwa uchumi kunapimwa kwaongezeko la pato la Taifa, Kiingereza Maarufu kama Gross Domestic Product (GDP)kwa nchi zinazoendelea. Pato la Taifa ni thamani ya bidhaa na huduma mpyazilizozalishwa au kutolewa katika uchumi wan chi kwa kipindi husika. Kipindi hiki kinaweza kuwamwezi, miezi, miezi mitatu au mwaka. Kwa maana hiyo, iwapo zitazalishwa bidhaapamoja na huduma nyingi zaidi basi pato la taifa huongezeka. Hivyo hivyo iwapozitazalishwa bidhaa au huduma ndogo pato la taifa hupungua.Kupunguaau kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa au huduma, kwa kiwango kikubwa hutegemeamahitaji ya bidhaa au huduma husika. Iwapo mahitaji yatakuwa makubwazitazalishwa bidhaa nyingi zaidi, na kama mahitaji yatakuwa madogo bidhaazitazalishwa kidogo. Mahitaji haya ambayo kwa kingereza yanajulikana kamaaggregate demand, kwa mantiki hii ni matumizi ya pesa kununua vitu au huduma.Kwahiyo uaweza kuona kwamba kumbe kukua au kudorora kwa uchumi kuna uhusiano wakaribu zaidi na ununuzi wa jumla yaani aggregate spending. Hii ina maana matumizi yakiongezeka na patola taifa huongezeka na kinyume chake ni hivyo hivho pindi matumizi yakipungua. Kamaununuzi ndicho kigezo kikubwa cha kuongezeka au kupungua kwa pato la Taifa nivizuri tukaangalia ni vitu gani husababisha ununuzi kuongezeka au kupungua.Kitaalamu,vitu hivyo vinawekwa katika makundi manne (4) ambavyo ni Kaya ambapo mtubinafsi au familia inanunua vitu au huduma mbalimbali kama chakula, kodi yapango, matibabu na vinginevyo.Kundi lapili ni wazalishaji likiwakilisha matumizi ya wazalishaji wanaponunua malighafiza kutengenezea bidhaa nyingine. Kuna serikali kundi la tatu ambayo hununuabidhaa mbalimbali wa ajiri ya kuhudumia jamii kama vile shule, barabara nahospitali.Kundila mwisho ni la wanunuzi wa nje ambao hununua bidhaa za nchi husika. Lakini kwahili la mwisho kinachoangaliwa ni tofauti kati ya thamani ya bidhaazilizonunuliwa na wageni na zile ambazo wageni waliiuzia nchi husika. Iwapo thamaniya bidhaa au huduma iliyonunuliwa kutoka nje itazidi ile ya bidhaa au hudumailiyonunuliwa kutoka nje itazidi ile ya bdihaa au huduma zilizouzwa nje, pato la Taifa litapungua, nalitapanda itakapokuwa kinyume chake. Katika pato la Taifa kundi la ununuzi wakaya ndilo huwa kundi kubwa zaidi na kukua kwa uchumi ambako kunanufaishasehemu kubwa ya jamii, kunatakiwa kutokane na ongezeko la ununuzi wa kaya.Hiiina maana kwamba kama nchi itakuwa na kaya nyingi ambazo zina uwezo mkubwa wakununua, basi hata uchumi wake utakuwa mkubwa zaidi kwa vile bidhaa na hudumahuhitajika kwa vile bidhaa na huduma huhitajika kwa wingi. Kayazitahitaji chakula kingi na kizuri zaidi, matibabu bora zaidi, usafiri mzuri,starehe, elimu na mengineyo.Hivyo hivyo, kama nchi ina kaya nyingi zenye uwezomdogo wa kununua, uchumi wake utakuwa mdogo na utashuka kwa vile kayazinahitaji bidhaa chache na huduma kidogo tu. Hata hivyo, hii haina maanakwamba kaya hizi hazina haja na bidhaa au huduma husika, bali kulazimikakuzikosa kwa sababu ya uhaba wa kipato. Lakini fursa ikuruhusu kwa maana yakipato kuongezeka, mara moja hununua bidhaa hizo kama vile kujitibia vizurizaidi, kupeleka watoto shule nzuri zaidi, kununua vyombo vya usafiri namengineyo.Nikwa sababu hiyo, binafsi tunatilia mashaka mikakati inayoitwa ya kukuza uchumina kuondoda umasikini katika nchi masikini kama Tanzania. Nafikiri dhana sahihiingekuwa mikakati ya kuondoa umasikini na kukuza uchumi.Tukishapunguzaumasikini wa kipato kwa wananchi walio wengi, hata viwanda vitachangamka kwavile vitakuwa na soko.Ukifanyautafiti katika viwanda vyetu vingi utagundua kwamba mauzo ya bidhaa zaoyamefungamana na shughuli za wakulima. Kiwanda cha urafiki kwa mfano, mauzo yanguo zake huendana na msimu wa mavuno wakulima wanapovuna na kupata fedha ndipohunnuua nguo nyingi.Msimuukiisha tu msimu wa mavuno nguo zinakuwa hazina soko tena. Hivyo hivyo kwaviwanda vya pipi, mafuta ya kula, pombe, sukari, mchele, ujenzi wa nyumba(sementi, mabati, nondo, rangi, misumari,mbao) Tv, Redio, na vinginevyo. Lakinikwa kujua au kutojua viongozi wan chi masikini kama yetu wanaweza kuwa namikakati ya kukuza pato la Taifa kwa kuongeza ununuzi wa moja ya yale makundimengine kama vile wazalishaji (ongezeko la wawekezaji) na wageni (ongezeko lamauzo nje ya nchi).Wanawezakufanikiwa kama ambavyo Tanzania imefanikiwa kupata wawekezaji katika migodi,viwanda, majengo makubwa na mashamba makubwa. Na kutokana na uwekezaji huowanaweza kufanikiwa kuongeza mauzo nje ya nchi, na kweli pato la Taifalitaongezeka kama ambavyo limekuwa likiongezeka kwa asilimia 6 hadi 7 kwa miakamitatu iliyopita.Lakinikukua huko kwa uchumi hakutakuwa na manufaa kwa wananchi masikikni walio wengikwa maana ya kupungua kwa umasikini kwa sababu hata hizo fedha zinapoingiazinaishia mikononi mwa wachache. Kwa kutojua hilo ndio maana viongoziwanashindwa kuelewa kinatokea nini; mbona uchumi unakua vizuri tena kwa kasilakini watu wanazidi kulalama tu kila kukicha.Kukuauchumi kwa mbinu tunayokwenda nayo kwa sasa Mweshimiwa Rais kutaifanya Tanzaniaifanane na nchi kama Kenya na Afrika ya Kusini tunazozipigia mfano na kuzisifukila mara kwa kupiga hatua kubwa kimaendeleo. Katika nchi hizi kuna viwandavingi na uchumi wao ni mkubwa, lakini wananchi walio wengi wamebaki kuwawashangiliaji, huku wakiongelea katika madimbwi ya ufukara.Pamojana tofauti kubwa baina ya masikini na matajiri, bado Kenya au Afrika Kusiniwatu wanaishi pamoja hata kama wanamanung’uniko ya chini chini. Mipango yakueneleza nchi ikiifanya Tanzania ifanane na Kenya au Afrika ksini amanitunayojivunia itatoweka kabisa.Hiini kwa sababu ya historia tofauti za nchi hizi Kenya na Afrika kusinizimejengwa katika misingi ya kibepari tangu zipate uhuru. Wananchi wameshazoeahali hiyo na wanavumilia. Leo hii Tanzania ina watu wanaokadiriwa kuwamillion 42 huku vijana wakiwa asilimia 60 hadi asilimia 70. Lakini wanakabiliwana tatizo la ajira. Wengi wao hawana Elimu ya kuwawezesha kupata Ajira Rasmi nahata wale wanaohitimu vyuo vikuu wakirudi mtaani wanakumbana na tatizo la AjiraSerikalini wakitaka kijiajiri hawana mitaji (Capita) na mifumo ya ukopeshaji wakibenki haiangalii mkopaji ana kiwango gani cha Elimu kitakachomuwezesha kukopana kuzalisha ili arudishe bali benki zinaangalia unamiliki nini (nyumba, Ardhi)ili ukishindwa kurudisha zichukuliwe hizo mali Je,! Hawa vijana wa familiamasikini waliobahatika kupata elimu angalau ya vyuo vikuu hawana Ardhi walanyumba kama mdhamini ili wapate mkopo benki watafanyeje Mweshimiwa Rais wetu?MheshimiwaRais ili serikali iweze kutoa huduma za kijamii kwa wananchi kama Elimu, Afya, Maji,umeme, bwawa, mawasiliano ulinzi na usalama wa mali zao inapaswa kukusanya kodiya kutosha ili kuboresha huduma hizo lakini cha ajabu na kusikitisha sualaambalo ni ugonjwa sugu wa “Rushwa” unaoendelea na kulitafuna Taifa letu nakusababisha kukosa mapato ya kutosha.Mheshimiwatuna kumbuka “RUSHWA” ni miongoni mwamambo uliyoahidi kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu kwa kuboresha na kuipa mamlakataasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) lakini Mweshimiwa msaada wachombo hiki umekuwa ni mdogo au hauonekani kabisa kwa kushindwa kubaini“RUSHWA” inayofanyika mikataba mikubwa ya nchi (Ten percent) mfano Richmond,ununuzi wa Rada, Migodi ya madini na sehemu nyingi za mikataba mikubwa. Nchiyetu Mweshimiwa Rais itaishia mikononi mwa wachache wenye nafasi za uongozi nafamilia zao huku sisi tukiendelea kuumia na ugumu wa maisha maana huduma zakijamii zote ni ghari kwetu kama Afya, Elimu, Umeme, Maji na mfumuko wa bei ya bidhaa.Kituambacho kama serikali ingekuwa inakusanya kodi kama inavyopaswa ingewezakuzioboresha huduma hizi kwa kuzitengea “RUZUKU” Mfano: TANESCO ili kupunguzana kuondoa taabu wanayopata wananchi pale TANESCO inapopandisha bei za umemeili shirika hilo liweze kujiendesha lenyewe baada ya kukosa RUZUKU kutokaserikali na kupelekea bidhaa zote zinazotokana na viwanda kupanda mara dufu.MheshimiwaRais tunakumbu mwaka 2009 wakati unazindua Jengo la Taasisi ya Kuzuia nakupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika jiji la Dar es Salaam. Ulielezamasikitiko yako wa kusema alilimia 30 ya bajeti ya serikali kila ikipangwainaishia mifukoni mwa watendaji ukimaanisha TAKUKURU wafanye kazi haswa lakiniwapi. Lakini kwa nini Rais wetu ulalamike wewe na sisi wananchi itakuwaje. Raiswawajibishe viongozi wote wenye tuhuma za Rushwa.Mheshimiwarais ushahidi uko wazi, ripoti za kila mwaka za Mkaguzi Mkuu wa fedha zaserikali (CAG) zinaonesha matumizi mengi yenye kutilia shaka kwa mtindo wamatumizi yasiyoidhinishwa, matumizi yasiyo kwenye vitabu vya mahesabu, malipoyasiyo ya kawaida, malipo yasiyo na viambatanisho, na Halmashauri kupata hatichafu kila mwaka. Kwa mfano:kati ya mwaka 2001 na 2006, fedha kiasi cha shilingi billion 14.5 zilitumiwavibaya. Pia ripoti ya (CAG) ya Juni 2008 inaonesha kwamba kulikuwepo na mashakasana juu ya matumizi ya shilingi billion 2.3 katika program ya mbolea yaRuzuku.MheshimiwaRais suala la rushwa, mikataba mibovu (Ten percent), kutowajibika kwa viongozi,ubinafsi vimeendelea kulitafuna taifa na kuwa chanzo cha uchumi wetukulegalega. Mfano; utafiti uliofanywa na shirika la (Faceit) mwaka 2009 chiniya ufadhili wa serikali ya Denmark ambao uliangali hali ya Rushwa na utawalabora nchini.Taasisizilizoshika kinara kwa rushwa ni Polisi 76%, Mahakama 71%, Ardhi 64.3%, TRA54.8%.MheshimiwaRais utaona ni namna gani Taifa linakosa mapato ya kutosha ili litoe huduma kwawananchi kama Elimu, Afya, Umeme, Maji na Barabara kutokana na pato la Taifakuwa dogo kitu ambacho kinatufanya kuwa tegemezi katika bajeti. Tunaombaserikali imulike, iangaze kwa jicho la kizalendo Rushwa inayofanywa ndani yajeshi la polisi na namna Taifa linavyokosa mapato, Tunaomba Rais uangalie kwamakini muhimili wa Mahakama kama unatuhumiwa kwa 71% kwa rushwa ni hatari kwanchi inayojitangaza kuwa na utawala boroa wa kisheria. Ndiyo maana Mafisadiwakipelekwa Mahakamani mwisho wanashinda kesi. Tunaombakama Rais wetu uangalie kwa makini Sekta ya Ardhi iliyoshika 64.3% kwa rushwa.Tumeshuhudia migogoro vijijini na mijini chanzo cha migogoro hiyo ni Rushwachonde chonde Rais wetu ingilia kati.TunaombaRais wetu kwa Roho ya huruma na moyo wa kizalendo uingalie Mamlaka ya mapatoTanzania iliyoshika 54.8% kwa rushwa hii ni hatari chombo kilichopewa mamlakaya kukusanya kodi ili Serikali iweze kuwahudumia wananchi wake kinapatikana nahatia ya Rushwa kwa asilimia kubwa namna hii 54.8%. Je? Mheshimiwa nchi yetukuendelea kuwa tegemezi katika mataifa ya kibeberu kila bajeti yake ya kilamwaka. na serikali kushindwa kuendesha mashirika ya umma kwa kuyapa ruzuku kama(Tanesco), Dawasco ili kupunguza ukali wa maisha na mfumuko wa bidhaa. hayayote na adha hii tutakuwa hatujakosea kama tutatwisha mzigo huu TRA na kubebamzigo wa dhambi hizo.1/17/2012.Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ilitangaza kwamba Desemba mwaka jana (2011) ilifanya“kufuru” pale waliposema kukusanya kodi kwa kiwango ambacho hakijawahi kufikiwatangu kuundwa kwake, zaidi ya miaka 15 iliyopita.Vyombovya habari vilimnukuu kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi wa TRAAllan Kiula akisema Desemba, Mamlaka hiyo ilikusanya Sh. 682.5 billioni nakuvuka lengo la Sh. 645 bilioni ambazo hazijawahi kukusanywa kabla.MheshimiwaRais kama mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) inashika nafasi ya nne kwa Rushwa54.8% na bado inashangilia eti wamevuka lengo la kukusanya Sh. 645 billioni nawakusanya 682.5 billioni ni dhahiri Rais wetu Serikali yako ikiweka lengo lakukusanya 800 -1000 billioni kwa mwezi inawezekana. Iwapo Rushwa itakomeshwandani ya chombo hiki muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.MheshimiwaRais ili uweze kutimiza ahadi yao uliowahidi watanzania mwaka 2005 wakatiunaomba ridhaa ya kuingia madarakani ya “Maisha Bora kwa kila Mtanzania”. Nimuhimu yafuatayo ushauri wetu ukazingatiwa kwa maslahi ya Taifa letu sote.1) Serikaliyako ipunguze matumizi (ijibane).2) Mikatabayote (uwekezaji, ubinafsishaji) ipitiwe upya ili ile mikataba iliyofungwa chiniya ushawishi wa Rushwa (Ten percent) ivunjwe kwa maslahi ya Taifa ili lipatemapato stahiki.3) Serikaliiangalie upya Taasisi hizi muhimu hapa nchini TRA na TAKUKURU ili ziisaidieSerikali kukusanya kodi na kusimamia usalama wa kodi za wananchi. MweshimiwaRais tunakuwa na mashaka kama Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa(TAKUKURU). Usalama wa Taifa kama vijambo hivi vimeshindwa kuisaidia serikalikubaini udanganyifu unaofanywa katika mikataba mbalimbali kama (RICHMOND,UNUNUZI WA RADA) n.k. udanganyifu unaofanywa katika Wizara mbalimbali katikamatumizi mabaya ushahidi huu uko wazi ukipitia ripoti zinazowasilishwa namdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG).4) MweshimiwaRais wakati muafaka serikali yako kubadilisha sera ya “Kilimo kwanza” hadiwananchi watakapoelimika na kuja na sera ya “ELIMU KWANZA”. Kwa ninitunakushauri hivyo Mweshimiwa Rais:-(1) Sualala wanafunzi 9730 kufutiwa matokeo ya mtihani wa Taifa mwaka jana.(2) Kuongezekaidadi ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika. Shuleya msingi msigani ya Mbezi Kimara Dar esSalaam kushindwa kufunguliwa mwezi januari hadi mwezi machi mwaka huu kwasababu vyoo vya wanafunzi viliathiriwa na mafuriko ya mwaka jana. Matokeo yakidato cha nne kuanzia mwaka jana kuonesha zaidi ya nusu kuwa wamefeli. Migomona maandamano vyuo vikuu iliyosababisha zaidi ya wanafunzi 900 kufukuzwa vyuona wengine kusimamishwa muda usiojulikana.5) MheshimiwaRais ni wakati muafaka Serikali yako ikapunguza matumizi ili ipate uwezo wakutoa RUZUKU katika mashirika ya Umma, ili kupunguza gharama wanazozibebawananchi wa kipato cha chini mfano; Shirika la umeme Tanzania Tanesco likipewaRuzuku kutoka Serikali itaweza kujiendesha lenyewe jambo ambalo litapelekeaTanesco kupunguza bei ya umeme nchini. Na umeme ukipunguzwa bei ni dhahiri beiza bidhaa nyingi zinazozalishwa viwandani zitapungua. Jambo ambalo litakuwanafuu na auheni kwa wananchi wa kipato cha chini waweze kuhimiri athari namfumuko wa bei za bidhaa uliofikia asilimia 20 kwa sasa. Huo ndiyo ushauri wetuMweshimiwa Rais. Tunaomba kuwasilisha.
SHUKRANI
Shukrani zetu za dhati zinawendeewale wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamefanikisha ukamilifu wa warakahuu kwa michango mbalimbali kama ushauri, ushiriki wa moja kwa moja katikakuandaa waraka huu, michango ya watu mbalimbali kwa njia ya makala kupitiaFacebook, twiter, Jamii forum, Magazeti, Simu za mkononi, nakala na majaridambalimbali, michango na mapendekezo ya walimu wetu vyuoni (wahadhiri) lakinishukrani zetu ziwaendee pia wanachi wapenda elimu pamoja na wadau mbalimbali waElimu hapa nchini, pia shukrani zetu ziwafikie viongozi wa Serikali zawanafunzi vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini kwa ushirikiano wao katikakufanikisha kazi hii adhimu. Wafuatao tungependa kuwatambulisha kwa majina yaokwa namna moja ama nyingine mchango wao kwa kiasi kikubwa umesaidia ukamilifuwa kazi hii.DEBORA GABRIEL ( Rais wa chuo Kikuu cha Dodoma)MUSA NDILE (Waziri Mkuu Serikali yaWanafunzi chuo kikuu cha IFM)MBOYA JAMES (Katibu katika serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha (IFM)DANIEL NAFTAL (Waziri wa mikopo chuo kikuu Cha Dar es Salaam)MRUTA JURIUS (Waziri wa Elimu chuo Kikuu cha Dar esSalaam mwaka 2009/10) LUSAPI, YUDAH (Mwakilishi kamati ya mikopo chuo kikuu cha Arusha)MR. MAKULI (Waziri Mkuu mstaafu Serikali yawanafunzi chuo kikuu cha Dar es Salaam)RWEZAULA ROBERT .K. ( waziri mkuuserikali ya wanafunzi chuo kikuu cha st.John Tawi la DAR ESSALAAMBICHWA SAUL (Waziri serikali ya wanafunzi chuo kikuuKishiriki cha Dar es SalaamDUCE ISMAIL MVUNGI (Rais wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Ardhi)MR. SALUM ( Makamu wa Rais serikari yawanafunzi chuo kikuu Cha Tiba muhimbili)KB OMARI, (Wadau wa Elimu nchini) RANKIM RAMADHANIHUSSENI SUNGURA, (Wanafunzi kutoka Chuo kikuu cha St.August AMINI RASHIDI Mwanza MUGATA GEOFREY, RUGEMARILA FRENK, (Wanafunzi wa chuo kikuu cha kumbukumbu SELENGIA GEORGE yaNyerere) HUSSEN RASHID ( Mwanafunzi chuo kikuu cha TibaIMTU) RICHARD JOHN (Wanafunzi wa chuo kikuu cha tibaBugando) SADRU MOHAMMED OTHMAN MRISHA, (Wanafunzi chuo kikuu cha KiislamMorogoro) KURUTHUMU HULEDIPamoja na wale ambao hatukuwatajahumu ndani lakini walitoa mchango wao uliowezesha kufanikisha kazi hii tunatoashukrani zetu pia kwa walimu wetu mnaotufundisha kwa mioyo ya uzalendo, wazazina walezi wetu, viongozi wetu wa Dini pamoja na watanzania wote kwa ujumla MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI SEKTA YAELIMUMASTAWILYFAHAMI MWENYEKITIWA KAMATI CHUOKIKUU CHA DAR ES SALAA
0 comments:
Post a Comment