Music

Friday, August 2, 2013

MABADILIKO YANAWEZEKANA...

Serikali yeyote duniani hutengeneza nchi na raia wanaofanana na asili ya serikali yenyewe. Serikali isiyo na nidhamu itatengeneza raia wasio na nidhamu. Na kinyume chake ni sahihi. 
Kwahiyo tabia ya nchi inategemea sana tabia za viongozi wake. Ni ukweli usiopingika huwezi kutoa usichokuwa nacho..Serikali isiyo kuwa na nidhamu haiwezi kuleta utaratibu katika nchi...

Baadae ya taifa hili itategemea sana busara ya watu wake kuchagua viongozi wenye nidhamu na busara ya kutosha ya kulitoa taifa hili hapa lilipo. Kwakuweka akilini kwamba watu wanaowachagua watajenga taswira ya nchi kulingana na tabia zilizo ndani yao..Kiongozi asiyetenda haki hawezi kuleta haki katika nchi ni ujinga kutegemea haki kutoka katika kiongozi asiyezingatia misingi ya haki.

Kama tukikumbatia uongo na kuwachukua viongozi tunaowajua kabisa sio waadilifu kwasababu ya kuhongwa au sababu ya kutokuwa makini kwetu kuchagua watu wenye maadili mazuri ubaya hautaweza kutoka mlangoni kwetu. 

Kwahiyo matatizo tuliyonayo ni mengi na tunahitaji kubadili taswira ya nchi yetu pamoja na mwelekeo wa siasa zetu , mwelekeo tulionao kwa sasa si sahihi na wala sio wenye kuzaa matunda kwa taifa letu. Siasa zetu mbovu ndizo zimetufikisha hapo tulipo na hali inaonyesha kuwa tunaelekea pabaya zaidi kama hatutabadili mwelekeo wetu wa fikra. Sitachoka kuelezea kuhusu ubinafsi ambao ni tatizo tulilonalo kwa sasa; linalo tuzuia kusonga mbele kama taifa. 

Watu wanaingia kwenye siasa sio kwa manufaa ya taifa hili, sababu ya ubinafsi wao. Na taifa kwa sasa limegawanyika kila mtu anajiangalia yeye hatuwezi kwenda na fikra za namna hii tukalinyanyua taifa hili. Ni lazima tubadilike, katika mtazamo huu wa ubinafsi hatutaweza kupendana, hatutaweza kuwa na wajibu wa pamoja katika ujenzi wa taifa hili. 

Vijana lazima watambue ya kwamba katika siasa sio sehemu ya kutokea, tusichezee uongozi una madhara makubwa kwa jamii kama hatutakuwa na watu makini kwenye siasa, baadae yetu kama taifa itakuwa gizani. Tusipokuwa na viongozi wazuri haki haitokuwepo na kama haki haitopatikana, taifa litakuwa na mgawanyiko. Ni lazima tuwe na viongozi wanaowajibika kwa watu. 

My dear brothers:Human beings need guidance: those who have knowledge and understanding must lead others. The prudent Must be presidents and rulers and nation will get direction and great prosperity.

Kwenye uongozi sio sehemu ya kutafutia sifa bali ni sehemu ya kuongoza watu na kufanya maamuzi sahihi yatakayosaidia watu. '' Wote sisi ni lazima tuwe msaada kwa taifa hili na sio kulibomoa'' Ni lazima tuzae matunda kwa taifa hili na tulijaze taifa hili kwa mema, tubadili mtazamo wetu na tutabadili taifa hili. We must do good...and our nation will be healed..

Wote mlio katika siasa katika vyama vyote tuache ubinafsi, Tuelekeze akili zetu katika kujenga taifa hili na sio kubomoana na kubomoa taifa hili. Ni lazima tukumbuke sisi ni wamoja na mwisho wetu ni mmoja. Ni lazima tuwe wamoja na tuache huu mgawanyiko hautusaidii, kama unatafuta uongozi kwasababu ya faida za kibinafsi hufai. 

Tunahitaji watu watakaoleta matunda katika taifa letu na bunge litakalo reflect ''Nobility and courage'' Kujitolea huku kwa taifa pasipo ubinafsi ili kuona taifa hili likiendelea pamoja na watu wake is the most noblest job for any great man. Let us embrace this truth'' Nguvu ya kubadilisha taifa hili iko mikononi mwetu, iko kwenye viganja vyetu tuna hii nguvu. Kitu tunachohitajika tu ni kubadilika, kubadili fikra zetu. Nina matumaini haya ndani kabisa ya moyo wangu; tunaweza kulinyanyua taifa hili, tuna uwezo huo, tuna uwezo wa kulinyanyua taifa hili likapendeza zaidi ya mataifa mengi na likatuletea heshima yetu na watoto wetu wakafurahia kuitwa watanzania, badala ya kufurahia mataifa mengine.

Sisi sio taifa la kugeza mataifa mengine, tuna uwezo wa kujenga taifa letu wenyewe na watu wetu wakawa na mtazamo na sura ya kipekee kwa mataifa. Tunahitaji kuweka program mpya katika fikra na mioyo ya watu wetu ili kuleta mtazamo mpya na chanya kwa watu wetu juu ya utaifa. Bila hivyo hatutaweza kulipeleka taifa hili mbele. Tunahitaji kujenga kuridhika kwa watu wetu kwa taifa lao ili kurudisha amani katika taifa na mwelekeo wa pamoja wa kujenga taifa hili. Utaifa hujengwa katika akili na mioyo ya watu na huimarishwa na haki na ubomolewa katika akili na mioyo ya watu watu wasipozingatia kutendeana haki. This Bond of unity and love among our citizens we must build. As the nation we are in great confusion: We need light and we need direction. Trust disapear. we are no longer binded by Nationhood but by our selfishness. There is no Hope anymore! No future!

Tumetawanyika na hatuna nguvu ya pamoja ya kujenga taifa. Ni lazima turudishe imani kwa taifa hili; Taifa hili ni kama mtoto asiye na baba, ni kama mtoto wa mtaani asiye na mwelekeo; ni lazima sasa tujenge nidhamu na mweleko wa taifa hili na watu wake. Hisia hii ya upendo miongoni mwetu na kwa taifa letu ni lazima ijengwe. Wote wanaoleta mgawanyiko kwaajili ya faida binafsi ni lazima tupambane nao ili kulinda taifa hili lisigawanywe. 

Baadae ya taifa hili na kizazi kijacho iko mikononi mwetu, tunawajibu wa kujenga nidhamu ya watoto na vijana wetu ili wawe wenye kuwajibika na kulipenda taifa lao. Kwasababu bila nidhamu hii ambayo ni muhimu sana taifa hili haliwezi kusonga mbele. Ni lazima tuondoe ubinafsi wetu na wote tujielekeze kwa pamoja kujenga taifa hili. Tuna matatizo mengi ambayo yanahitaji nguvu ya pamoja na busara kuyatatua.

Katika mtazamo huu; ambao tutaacha ubinafsi tutaendelea kwa haraka zaidi. Ni lazima tuwe na kiu ya kutaka kuendelea kwa pamoja kama taifa. Kama tukiendelea kwa pamoja kama taifa tutakuwa na furaha ya pamoja na kila mtu atalithamani taifa hili. Hatuwezi kujenga taifa la matajiri wachache na maskini wengi. Hatuwezi kuendelea kuwasahau maskini wa taifa hili khalafu tukajenga taifa bora. Ni lazima tujenge uzalendo na wajibu kuanzia kizazi hili. Wote ni lazima tujue tunawajibika kwa taifa hili. Kuanguka au kunyanyuka kwa taifa hili kuko katika mikono ya kila mmoja wetu. 

Kwahiyo Chadema na Ccm na vyama vingine ni lazima wabadilishe fikra zao na wajue umoja wa nchi hii ni muhimu kuliko ubinafsi. Nawaomba wote wabadilishe mwelekeo wa mawazo yao. Fikra zetu iwe kujenga jamii bora sio kuleta mgawanyiko katika taifa ambao hauna faida kwetu. Ili kujenga taifa hili ni lazima tulijenge katika fikra sahihi na katika ukweli na uwajibikaji. Ni lazima tuwe na dhamira ya dhati ya kulijenga taifa hili. Kutaka sifa binafsi hakutasaidia taifa hili. Lakini pili wapime watu wanaowapa nafasi ya kugombea uongozi katika vyama vyao kama watakuwa ni wenye manufaa kwa taifa. Taswira ya taifa letu itategemea sana viongozi tulionao. Viongozi ndio wanao mould taifa according to their virtues. Taifa lenye viongozi waovu litatengeneza jamii na taifa lenye maovu. Kwahiyo ni lazima tubadilike tuache kuingia kwenye siasa ili tujijenge kibiashara. ''Administration of justice must be our primary aim as the nation without it we can not prosper'' 


Kwahiyo tunahitaji mwelekeo kutoka katika confusion iliyopo, tunahitaji dira. Ili kizazi chetu kijacho kisikose dira. Sisi vijana tuliopo tulitegemea kupata dira hii kutoka kwa wazee wetu lakini haina budi kuitafuta sasa na kuilazimisha kuwepo ili kuokoa taifa hili na vizazi vingi vijavyo, ni lazima tufikiri zaidi ya uwepo wetu. Ni muhimu kutofikiri kwa kizazi hiki tu bali tutengeneze future ya kizazi chetu kijacho ni lazima tuitayarishe sasa. Naamini watu wa taifa hili wako tayari kutayarisha baadae ya watoto wao wenyewe waliozaliwa na watakaokuja vizazi vingine vijavyo. Naamini kila mmoja wetu yuko tayari kufanya kazi kuona taifa hili likiendelea. Naamini nyinyi nyote mnalipenda taifa hili. Naamini nyinyi nyote mnanhitaji mabadiliko. Mabadiliko sio kuondoa serikali moja na kuingiza nyingine kisha mazoea na taratibu kuwa zile zile, ni lazima tuvunje gamba la yai. All we need is total transformation of our hearts and minds. Kutoka katika kiza mwangaza lazima utokee. Nina matumaini makubwa na baadae ya taifa hili kama tutabadili fikra zetu. Kama tuta shape siasa zetu ili ziwe zenye tija kwa taifa letu. 

Na mambo yote haya ya msingi yanahitaji nidhamu na kujitolea ili kuona misingi imara ya taifa hili ikijengwa na heshima ya taifa hili ikirudi. Ni Lazima tubadili siasa zetu tusipo badili maendeleo kwetu itakuwa ni ndoto. Ni lazima tujenge siasa zenye kuwajibika na za watu waliokomaa wanaojua nini wanajenga. 

Ni lazima tufanye installation kwenye akili za watu wetu na kuweka new programs kwenye akili na mioyo ya watu wetu ambazo zitakuwa na manufaa kwa ujenzi wa taifa hili. Ni lazima tuondoe virusi wote na tulete fikra mpya. 

Mwelekeo wa mawazo yetu wa sasa hauna matunda. Lazima taifa hili lijiamini, lazima taifa hili liwe na busara, lazima taifa hili liji tambue. We must be most noblest people on the earth and this; is within our reach.. we can shape our behaviour. 

Ni lazima tujenge tabia ambazo zitakuwa na manufaa katika ujenzi wa taifa hili ili kizazi cha vijana wa taifa hili wafurahie utaifa wao. Ni lazima turudishe akili zetu katika utaifa. Huku ndiko kujitambua ama sivyo tutakuwa taifa la watu wasiojitambua wao ni kina nani. We must be pioneers kwa kizazi kijacho. Ili kizazi kijacho kifurahie matunda ya juhudi zetu pamoja na maarifa yetu. 

Najua wewe sasa hivi unayesoma hii makala uko tayari kuona taifa hili likiendelea, uko tayari kujitolea..UKO TAYARI kuona taifa hili likiwa moja na likiwa huru kutoka katika rushwa na ufisadi , kwa kubadili tabia yako utabadili taifa. Na wote tuseme no kwa rushwa na ufisadi ili tujenge jamii bora na watu bora katika ulimwengu. Wote tukatae viongozi waovu na wala rushwa ili tujenge taifa kwa pamoja.


CHANGE IS POSSIBE 2

0 comments:

Post a Comment