Barua ya kwanza kwa Mh
Rais John Magufuli
Kwako Mh Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amiri Jeshi mkuu na mkuu wa vikosi vyote vya
usalama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Rais, salamu
sana, ama baada ya salamu ni matumaini yangu kwamba unaendelea vyema na
shughuli za kulijenga taifa letu liwe imara katika Nyanja za kiuchumi, kiafya
na kijamii.
Mheshimiwa Rais, nakala
hii ikufikie kama ilivyo na hata kama utapokea kutoka kwa vyombo vyako vya
usalama, natamani kama watakupa usome mwenyewe badala ya kupokea kutoka kwao
kama stori au mrejesho wa kilichoandikwa kwenye mitandao ya kijamii.
Mheshimiwa Rais, niweke
wazi tu mrengo na msimamo wangu kwamba, mimi ni miongoni mwa watanzania
wachache wanao “koshwa” na kuvutiwa na utendaji wako wa kazi. Naweke msimamo
wangu huu wazi ijapokuwa mimi ni wa itikadi tofauti kisiasa na wewe.
Mheshimiwa Rais, awali
tulikuwa tunalalamika na kulia kilio kimoja kama taifa kwamba tunahitaji Rais
mwenye “meno”, Rais mwenye uwezo wa kusema na kusikika, Rais mwenye uwezo wa
kutamka na kusimamia tamko lake, Rais mwenye “long run vision” kwa taifa hili.
Bila kupepesa macho wala kung’ata ulimi, wewe ni aina ya Rais ambaye nilikuwa
nikiota siku zote.
Mheshimiwa Rais, ni
ukweli usiofichika kwamba, too much
democracy is harmful for development of developing nations as it has
bureaucracy decision even on sensitive deals. Leo hii bara la Afrika na
vyama vingi vya saisa vinamtumia na kumuona Kanali Muamar Gadafi kuwa nguli na
kiongozi shupavu na imara kwa Afirca na waafrika kwababu alitetea na kusimamia
kile alichokiamini (long run vision) ijapokuwa kilifasiriwa na hawa hawa
wanaotuimbia na kutuhubiria demokrasia kuwa alikuwa dictator.
Mheshimiwa Rais, Ili
taifa hili lisonge mbele na tufike mbali kiuchumi, ni lazima awepo mtu mmoja
mwenye uwezo wa kukemea na akasikika, mwenye uwezo wa kuonya, mwenye uwezo wa
kutoa, kusimamia na kutetea msimamo wake ambao una long run development vision
kwa nchi yetu.
Mheshimiwa Rais, kusudi
langu kubwa la kuandika nakala ya barua hii, ni kukupa mawazo yangu kama kijana
wa kitanzania mwenye ndoto ya kuona Tanzania ikiwa taifa kubwa kiuchumi Afrika
na duniani.
Mheshimiwa Rais, nianze
kukunanga kwa wateule wako wa nafasi mbalimbali, mfano Mawaziri, Makatibu wa
wizara, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri na miji.
Hawa ndio watendaji wa shughuli za kila siku. Hawa wanapaswa kuwa na:
a)
Work Plan and KPI zinaonyesha target zao
(drawn from national target) na namna ya kuzifikia. Mfano, ni aibu sana kwa
halmashauri kulalamika hawana mapato ya kutosha kutekeleza shughuli za
kimaendeleo wakati wana uwezo wa kuongeza pato la halmashauri kwa kupanua wigo
wa mapato like, kurasimisha biashara zote ndogondogo ili kukusanya kodi
kiurahisi, kusajili nyumba zote ili kurahisisha kukusanya kodi zitokanazo na
majengo
b)
Ubunifu wa namna ya kuongeza ufanisi kwa
chombo wanachokiongoza. Mfano, ni aibu sana kwa taifa kama hili kulalamika
upungufu wa chakula wakati kuna mikoa ambayo ina uwezo wa kuzalisha chakula kwa
wingi kama Mbeya, Katavi, Iringa, Rukwa etc. Mikoa ya Dodoma na Singida ndio
mikoa ambayo water table ipo karibu sana, kiasi kwamba hawa wanaweza kutarget
kwenye kilimo cha umwagiliaji kwa kuchimba mabwawa makubwa kila wilaya na kuwa
na mashamba ambayo yataendeshwa na kusimamiwa na wizara ya chakula. Mavuno ya
mazao yote haya yanakusanywa na kupelekwa kwenye maghala ya taifa badala ya kumilikisha
watu binafsi.
Mheshimiwa Rais, Suala lingine
ambalo ningependa kulizungumzia kwa leo ni kuhusu wafungwa wa nchi hii.
Nashauri, wafungwa watumike katika shughuli za ujenzi wa miundombinu zetu.
Mfano, tunaweza kuwatumia katika ujenzi wa majengo ya serikali (nyumba za
walimu na askari), ujenzi wa barabara nk. Hii itawapa elimu ya ufundi ili hata
watakaporudi mtaani wawe na uwezo wa kujiajiri kuliko kuwa tegemezi. Lakini pia
inashindikana nini kuwa na mashamba makubwa ya serikali ambayo watakaokuwa
wanafanya kazi ni wafungwa kama sehemu ya kuwapa mafunzo na pia kuzalisha
chakula kuliko kupelekewa chakula bure bila kufanya kazi?
Mheshimiwa Rais, suala
la pili kwa siku ya leo ni kuhusu ELIMU yetu. Kulingana na mwelekeo wa dunia ya
leo, hatuna budi kuweka mfumo wa elimu ambao utatuwezesha kuendana na kasi ya
dunia hii. Mapendekezo yangu, tuwe na mfumo wa elimu ambao kuanzia ngazi za
msingi kabisa unawaandaa wanafunzi kuwa wataalamu wa fani Fulani.
Mheshimiwa Rais, kuna
umuhimu wa kuwa na masomo ya Sanaa na Ufundi kuanzia ngazi ya msingi. Masomo
haya yatawajenga vijana wetu kuwa imara kwenye soko la ajira ili kuwa na uwezo
wa kujiajiri pindi wanapohimtimu elimu ya msingi kama watakuwa hawajafanikiwa
kujiendeleza na elimu ya sekondari.
Mheshimiwa Rais, Kuliko
na shule ya sekondari kila kata, tuwe na shule za mafunzo ya Ufundi, Sanaa,
Michezo au/na Teknolojia kila wilaya. Kwa mfano, tuwe na shule kwa ajili ya
mafunzo ya sayansi ya madini, sayansi ya gesi, elimu ya uvuvi, ufugaji na
kilimo cha kisasa nk. Elimu hii ianze kutolewa kuanzia ngazi za chini na
itolewe kwa nadharia na vitendo. Iandaliwe miundombinu sanifu na shule hizi
zianzishwe mahali ambazo kuna rasilimali husika. Kwa wale ambao watakuwa
wame-opt kufanya elimu kama sheria, uhasibu, ugavi, engineering, waunganishwe
moja kwa moja na bodi husika ili pindi wanafunzi wanapohitimu wawe tayari
wameshasajiliwa na bodi husika. Hii itawawezesha wanafunzi kuwa imara na
kujihusisha na taaluma zao mara wanapohitimu tofauti na ilivyo sasa ambapo wakihitimu
wanapaswa kufanya mitihani tena za kusajiliwa na bodi. I see this like jipu na
njia iliyobuniwa na wachache kuwaibia watanzania. Wenzetu wa nchi ya India,
kama mwanafunzi anachukua uhasibu, ataanza kuandaliwa kuanzia ngazi za awali kwa
kujiunga na Chartered Accountant Collage/Institutes. Pindi anapohitimu anakuwa
tayari ni recognized and registered accountant. Vivyo hivyo kwa watu wa fani
zingine.
Mheshimiwa Rais, Nisikushoshe
sana na barua hii kwani najua una majukumu mengine mengi ya kulijenga taifa
letu. Nikutakie afya njema na Mungu aendelee kukulinda na kukupa moyo hasa
katika kipindi hiki ambapo unafanya mapinduzi ya kimfumo katika Nchi yetu kwani
walio wengi watakupinga kutokana na kuguswa moja kwa moja.
Ni wako katika ujenzi
wa taifa, Ismail Mesaya (Mob: 0756688090)
0 comments:
Post a Comment