Kwa maoni yangu, kuna kesi kuu nne ambazo naamini kama zingeshughulikiwa vizuri pasipo kuoneana aibu, basi mustakabali wa Taifa letu ungebadilika. Wananchi wengeweza kuwa na imani zaidi na Serikali yao. Kesi hizo ni zifuatazo:
1. WIZI WA FEDHA ZA MADENI YA NJE (EPA): Kosa la kwanza katika hii kesi ni kuwapa wezi (majambazi) wa fedha za umma muda wa kurudisha walichokiaba bila adhabu yoyote; bila hata riba!!
2. KUTEKWA NA KUUMIZWA VIBAYA KWA MWENYEKITI WA MADKTARI (DR. ULIMBOKA): Hadi leo sijui nini kinaendelea. Hata Dr. Ulimboka mwenyewe simuelewi kabisaaa! Hivi hii kitu ndio imeisha kimyakimya hivyo. Katika tamko lake Dr. Ulimboka aliwataja kabisa na wahusika lakini sijui nini kinaendelea.
3. KIFO CHA MWANDISHI WA HABARI MKOANI IRINGA AKIWA MIKONONI MWA POLISI: Laiti kama tukio hili lingetokea katika nchi za wenzetu wanaojali usalama wa raia na uwajibikaji panapotokea kosa, basi Afisa wa Polisi aliyehusika angetakiwa kuwajibishwa mara moja. Lakini hadi leo sijui nini kinaendelea.
4. SHUTUMA ALIZOZITOA DR. REGINALD MENGI KUHUSU MKUU WA KITENGO CHA KUZUIA MADAWA YA KULEVYA: Hii nayo inanishangaza. Ndugu Mengi alitoa shutuma mbele ya vyombo vya habari lakini sijui ni hatua gani zilichukuliwa kwa aliyeshutumu na kwa aliye-shutumiwa. Tunaweza sema labda walimalizia shida zao ofisini kwa siri; lakini ikumbukwe kwamba Dr. Mengi alitoa shutuma mbele ya umma wa Watanzania na tuna haki ya kujua nini kiliendelea.
0 comments:
Post a Comment