Music

Saturday, December 14, 2013

TUTAFAKARI MUDA WA KUFANYA KAZI

Kwa mwaka 2013, Tanzania ina siku 23 za mapumziko (Public Holidays), jirani zetu Kenya wana siku 9 tu za mapumziko.

Kwa Tanzania, Ofisi zote za umma na chache za binafsi hazifanyi kazi jumamosi wala jumapili. Kwa mwaka kuna jumamosi na jumapili 105.

Hivyo ukichukua siku 105 za weekend ambazo Watanzania hawafanyi kazi, ukijumlisha na siku 23 za public holiday unapata jumla ya siku 128, ambazo Watanzania hatufanyi kazi kabisa, yani tumerelax, tunaspend, kile tulichokitafuta siku 5 za wiki.

Siku 128 ambazo hatufanyi kazi ni sawa na miezi minne na siku 8.

Hii ina maana kuwa kwa mwaka, Watanzania tunafanya kazi miezi 7 na siku 22, kisha tunapumzika miezi minne na siku 8.

Hii ni nchi inayoendelea na tuna ndoto za kuwa taifa lenye nguvu kiuchumi.
Tafakari chukua hatua.!

0 comments:

Post a Comment