Music

Friday, December 6, 2013

MADIBA MADIBA MADIBA.......

Madiba, Madiba, Madiba, moyo wangu umekufa ganzi....
Walimwengu na ulimwengu wote umeelekea Sauzi......
Makaburu na Wazungu wote wanakuzunguka kama nzi.....
Wazungu na weusi wote wanakuhusudu.........
Dhahiri umedhirisha ulikuwa chaguo la Mungu..........
Kuwasamehe, kwako haikuwa ngumu........
Miaka 27 ulinyea ndoo.....
Kweli walikukalia koo.....
Walitamani kuzika hadi ukoo.......
Kwa ushujaa ulikuwa kama Yesu......
Ulipigana kubaguliwa kwetu.....
Na kuibiwa kwa rasilimali zetu......
Waliungana kukutia selo.......
Kwani kwa uovu wao ulikuwa kero....
Ulipotoka uliwasamehe na wala hukuwatenga.........
Kama Yesu, ulisema hawajui wanalotenda........
Dah! Machozi yanazidi kunitoka......
Hivi kweli Mandela umetutoka?.......
Mungu akulaze mahala pema peponi.....
Amen

0 comments:

Post a Comment