Chagua mke kipofu, Kitembea hatazami
Mbonize sio potofu, Aonacho halalami
Kiwa nje huna hofu, Haulizi hasimami
Mke alo na kasoro, Kioa ni mke bora
Chagua mke kiziwi, Alokufa masikio
Vijineno haambiwi, Udaku na matukio
Kwa soga haingiliwi, Lughaye maashirio
Mke alo na kasoro, Kioa ni mke bora
Chagua mke lo’ bubu, Ulimi alofungiwa
Matamshi yake tabu, Hasemi akajibiwa
Majungu ya taarabu, Asije akatungiwa
Mke alo na kasoro, Kioa ni mke bora
Chagua mke kiwete, Siwe kiguu na njia
Hatembei enda tete, Mwendo ni wakuguchia
Misafara asifwate, Adiriki kutulia
Mke alo na kasoro, Kioa ni mke bora
Chagua mke kikono, Ukisema hangurumi
Mkianza mabishano, Asikukunjie ngumi
Si bondia wa pambano, Ukorofi hauvumi
Mke alo na kasoro, Kioa ni mke bora
Chagua mke mshamba, Asojuwa vipodozi
Asipende kujipamba, Midume haitongozi
Siringe na kujigamba, Akazidisha mapozi
Mke alo na kasoro, Kioa ni mke bora
@Comrade Mesaya
0 comments:
Post a Comment