MWANANCHI WANGU, KAMA NILIVYOKUELEZENI AWALI KUHUSU DHAMIRA YANGU YA DHATI YA KUIFUNZA JAMII NA KULETA UKOMBOZI CHANYA KWA KUTETEA RASILIMALI ZA NCHI YANGU NA WATU WA JAMII YANGU, LEO NDIO TOLEO LA KWANZA LA JARIDA LETU MARIDHAWA LINALOTOKA KILA IJUMAA LIMEINGIA MTAANI........ JITAHIDI KUSOMA KILA NUKTA UPATE UKOMBOZI WA KWELI...
FUKUNUNUNYUMA
YA PAZIA
|
Toleo. Na
0001/2013 Ijumaa 03/05/2013
- 09/05/2013
|
Na
mwandishi wetu;
Ndugu mwanaterat hakika tumeonewa kiasi cha kutosha,
tumenyonywa kiasi cha kutosha na tumenyanyaswa kiasi cha kutosha bila kuwa na
wa kusikiliza vilio vyetu. Nadhibitisha ukatili huo uliofanywa na unaofanywa na
serikali yangu chini ya uongozi wetu wa kata kwa haya yafuatayo:
- Wananchi
kutoshirikishwa kikamilifu katika upangangaji na utekelezaji wa shughuli
mbalimbali za maendeleo na kuendeleza na kutumia rasilimali zilizopo ili
kupambana na ujinga, umasikini na maradhi kama ilivyoainishwa kwenye
Sheria Na. 7/1982 kifungu III(2)(e), Na TS Na.451/1995 aya 8.1
Limekuwa ni jambo la
kawaida sana kwa viongozi wa Terat kutowashirikisha wananchi katika kupanga ama
kutekeleza mambo mbalimbali ya kimaendeleo, na hii inasababishwa hasa na
kutokuwepo kwa vikao vya kata na hata mitaa. Shughuli zote zinatekelezwa (kama
zipo) na viongozi pasipo kuwashirikisha wananchi wao kwani kama kuna mradi
wowote unaoendelea Terat, hakika hakuna mwananchi mwenye taarifa ya lini mpango
huo umepangwa, kupitishwa ama kiasi gani kimetengwa kwa ajili ya utekelezaji
wake na ni kiasi gani kimekwisha kutumika na kiasi gani kimebaki.
- Wanachi
kutoshirikishwa kwenye mikataba yoyote ya kiuwekezaji inayofanywa ndani ya
kata ama mitaa yao kinyume na Sheria Na. 7/1987 kifungu 26(2)(c); kifungu
142(2)(e)
Mfano mzuri sana wa
jambo hili ni kwa kampuni iliyoingia mkataba kujenga hostel za sekondari ya
Kinana ambapo hakuna mwananchi aliyehusishwa ama anayejua yaliyomo kwenye
mkataba huo. Hadi sasa kiasi chote kinacholipwa na wanafunzi wanaotumia hostel
hiyo inachukuliwa na kampuni iliyowekeza (jina tunalihifadhi) na hakuna
mwananchi yeyote anayejua hilo zaidi ya viongozi na familia zao. Pia kuna
uwekezaji uliofanywa na meya wa jiji la Arusha kwa kufungua kampuni ya kusaga
kokoto maeneo ya En’donyo Kumur na hakuna mwananchi anayejua uwekezaji huo
unamnufaishaje mzawa ama ni kiasi gani kinachobaki kwenye mfuko wa kata.
- Mahesabu
ya mwaka kutotayarishwa, kuwasilishwa na kukaguliwa na wananchi na zaidi
wananchi kutosomewa taarifa hiyo ya mapato na matumizi kinyume na Sheria
Na.7/1982 kifungu 49 na TS Na.451/1995 aya 8.2
Kauli hii pia
ilithibitishwa na mwakilishi wa mkurugenzi wa jiji la Arusha pale alipoulizwa
na Vijana kama huwa anapokea taarifa ya vikao vya kata kutoka kwa viongozi wa
Terat, na alihamaki kwa kusema miongoni mwa kata zenye taarifa yenye madudu ni
kata ya Terat na mbaya zaidi taarifa zinazowasilishwa hazina taarifa ya Mapato
na matumizi.
- Kutokuwepo
kwa uwazi kwenye shuguli za udhibiti na usimamizi wa fedha za kata. Hii
inachochewa zaidi na kutokuwepo kwa mashaidi wa fedha (Account
signatories) ambao watahakikisha kwamba vitabu vinaandaliwa, kuandikwa na
kutunzwa ili kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi ya fedha na mambo
mengine yahusuyo fedha, mali na madeni ya kata kinyume na Sheria Na.9/1982
kifungu 39(1).
Shughuli zinazohusu
miamala ya fedha katika kata husimamiwa na kikundi/genge Fulani la watu
(mafisadi) na wala hakuna ushirikishwa wa wananchi katika hilo.
- Kutoandaliwa
kwa vikao vya kata kila baada ya miezi mitatu na kusomwa kwa taarifa ya
fedha ya mkaguzi wa nje (Independent auditor) kwenye vikao vya kata na
mtaa kinyume na Sheria Na.7/1982 kifungu 45(4)
Ni jambo la
kuhuzunisha kwamba taarifa za mkaguzi wa nje yahusuyo mahesabu ya kata ya Terat
hayajawahi kusomwa kwa wananchi kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10 sasa.
- Kutokuwepo
kwa UWAZI, UFANISI na UADILIFU kwenye utekelezaji wa shughuli za kata na
hata mitaa kinyume na Sheria Na.7/1982 kifungu IIIA (1) (c).
Mfano kwenye kata yetu
kuna shule ya msingi iliyopo En’donyo Kumur ambayo toka mradi huo umeanza
kutekelezwa sasa ni zaidi ya miaka 10 yamepita na kila mwaka mwananchi amekuwa
akitozwa fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi huo lakini cha kushangaza hakuna
hatua zozote za umaliziaji zinazoendelea hivyo watoto kuendelea kusafiri zaidi
ya Kilomita 14 kufuata shule ya msingi.
Vilevile ujenzi wa
zahanati ya Nadosoito ambayo imegeuka nyumba ya kuhifadhia vifaa vya ujenzi na
mpaka sasa hakuna mwananchi mwenye taarifa kuhusu kiasi kilichotumika hadi sasa
na kwanini ufunguzi wa zahanati hiyo haufanyiki na kupelekea watu kusafiri zaidi
ya kilomita 20 kufuata huduma ya hosipitali.
- Wananchi
kutoshirikishwa katika kujadili taarifa na maendeleo ya shule kama
ilivyoainishwa kwenye waraka wa elimu Na.14 wa 7.6 2002.
Taarifa kuhusu
maendeleo ya shule hasa shule pekee ya sekondari iliyopo kwenye kata haijawahi
kuwasilishwa na kujadiliwa na wananchi zaidi ya kutakiwa kulipa malipo mengi
yasiyo ya msingi. Mfano kila mwanafunzi analazimishwa kulipa kiasi cha Tsh
20,000 kama hela ya taaluma kwa ajili ya kuwalipa waalimu wa ziada
wanaofundisha shuleni hapo ambao hawajaajiriwa na serikali, lakini cha
kushangaza hadi leo hii kuna mwalimu mmoja tu na kuna baadhi ya masomo ambao
wanafunzi hawafundishwi kutokana na kutokuwepo kwa walimu na hakuna taarifa
kwamba kiasi hicho kinachotolewa na wanafunzi kinatumikaje kwani shule ina
wanafunzi zaidi ya 700, kwa mahesabu ya haraka tu kiasi kinachokusanywa ni
zaidi ya 1,400,000.
- Halmashauri
ilitenga kiasi cha kutosha kwenye bajeti ya ili kufanikisha uchimabaji na
ujenzi wa visima 12 sehemu kame na visima hivyo vilitolewa kwa kata ya
terat, lakini cha kushangaza hakuna ujenzi wowote uliofanyka mpaka sasa na
katika bajeti ya mwaka huu halmashauri ilitenga kiasi Fulani ili kumalizia
ujenzi huo kitu ambacho tunakiona kama kutenga kiasi kwa ajili ya kuliwa
na genge la mafisadi waliojificha Terat. Nasema hivyo kwasababu ujenzi wa
kisima kinachojengwa eneo la kisimani mkabala na shule ya Intel ni ujenzi
unaofanywa kwa msaada wa Benki ya dunia na TASAF na wala hauhusiani na
fedha zilizotengwa na halmashauri. Hali hii inasababisha kinamama kusafiri
zaidi ya Kilomita 20 kutafuta maji na muda mwingine kunywa na kutumia maji
ya mabwawa na mito.
- Kutengwa
kwa kiasi cha kutosha na halmashauri ya jiji kwa ajili ya ujenzi wa
barabara ya Terat kwa kiwango cha moram, lakini cha ajabu hakuna shughuli
zozote zilizofanyika na hali imezidi kuwa mbaya zaidi kwani barabara ile
haipitiki tena na ndio barabara kuu inayounganisha wananchi hao na mji wa
Arusha. Hali hii inapelekea wananchi hawa kukosa huduma zao muhimu za
kijamii. Hali hii iliwafanya Vijana waamue kuandamana na kufunga barabara
hiyo hali iliyomfanya mkurugenzi wa jiji kuingilia kati na kuamuru
viongozi wa kata waitishe mkutano wa kata haraka ndani ya siku 10.
- Gari
la hosipitali (Ambulance) kutumiwa na viongozi kwa shughuli zao binafsi na
muda ukihitajiwa na mwananchi hutakiwa kuweka mafuta ndio utumike
kumpeleka mgonjwa hosipitali wakati kila wiki kuna kiasi kinawekwa na
halmashauri ili kufanikisha shughuli za kuwahudumia wananchi. (Kwa taarifa
zaidi juu ya sheli wanayotumia kuweka mafuta na kiasi kinachowekwa na
halmashauri kwa wiki na kiasi kinachowekwa na wahusika (Baada ya
kuchakachua kile kiasi halali kinachowekwa na halmashauri) na namna mafuta
yanavyotumika, Ushahidi wa kimaandishi na simulizi upo)
- Chakula
kilicholetwa kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya KINANA kuuzwa
kinyemela na kinyume na sheria na wahusika wakishirikiana na viongozi wa
kata na kukusanywa zaidi ya Tsh. 10,000,000 ambazo ziligawanywa na
wahusika. Hali hii imepelekea wanafunzi kukosa chakula kwa baadhi ya siku
na kurudisha kwa kiasi kikubwa maendeleo ya shule. ( Ushahidi kwa taarifa
hii upo na hata wahusika wanao)
Nihitimishe kwa
kuwakumbusha wanaterat kwamba hakuna maendeleo yoyote yanaweza kufikiwa terat
kwa sasa bila mapinduzi. Mapinduzi tunayohitaji ni ya kisera, kimfumo na
kiuongozi. Kwani hata waliotutangulia waliwahi kusema ili kuendelea tunahitaji SIASA SAFI na UONGOZI BORA……
Cont: 0712 814 285
0 comments:
Post a Comment