TAFAKURI YA LEO HAKIKA NI FUNZO TOSHA KWA JAMII YOTE YA WATANZANIA HATA WALE WASIOVUTIWA NA SIASA KWANI TAFAKURI YA LEO HAINA HATA CHEMBE YA SIASA ZAIDI YA ELIMU......................
TAFAKURI
YANGU
Na mwandishi
wetu,
Alhamdulilahi ashukuriwe mwenyezi
Mungu subhana whuataala, pia Amen ashukuriwe Bwana wetu Yesu Kristo kwa
kutujualia siku nyinge yenye kheri na iliyojawa na hashki ya kutaka kujua
tafakuri ya leo inakuja na jambo gani muhimu la kutunyetisha sisi wanajamvi wa
ulingo huu.
Ni matumaini yangu kwamba
tafakuri ya wiki iliyopita ilikwaruza kwenye nafsi ya kila mmoja na kumfanya
azijue vyanzo vya mapato yaliyopo kwenye ukumbi wetu huu mtamu wa Terat.
Tafakuri yangu wiki hii ni juu ya
WAJIBU, HAKI NA MAJUKUMU YA WANANCHI katika ngazi za serikali za
mitaa.
WAJIBU wa wananchi;
1. Kuandaa
mikutano katika vitongoji, vijiji na kitaa na kuhakikisha kuwa mikutano
inafanywa kwa muda uliopangwa (Mara moja kila baada ya miezi mitatu)
2. Kulinda mali
ya umma kama ardhi, kupambana na ubadhilifu wa aina yoyote pamoja na kutotumia
mali ya serikali kwa manufaa ya mtu binafsi.
3. Wananchi
wana wajibu wa kumwajibisha kiongozi asiyewajibika ikiwepo kumpigia kura ya
hapana.
4. Kujenga
na kuimarisha mshikamano uliopo ili kulinda sifa ya nchi.
5. Kushiriki
katika kupanga, kusimamia, kutathmini kuhoji matokeo ya miradi yoyote katika
kitongoji, kijiji au mtaa kushiriki katika kupiga au kupigiwa kura kwa
kuzingatia masharti yaliyotolewa.
HAKI
ya Mwananchi;
1. Kujua
mapato na matumizi ya fedha katika kitongoji, kijiji au mtaa pamoja na kupata
fursa ya kukagua na kuuliza kuhusu mwenendo wa mapato na matumizi.
2. Kuchagua
na kuchaguliwa ikiwa mwananchi atatimiza masharti ya kupiga au kupigiwa kura
3. Kushiriki
katika shughuli zote za kisiasa katika kijiji, mtaa au kitongoji chake
4. Kushirikishwa
na kiongozi katika shughuli mbalimbali za maendeleo
5. Kujua
mipango ya maendeleo mbalimbali inayotekelezwa
MAJUKUMU
ya Mwananchi;
1. Kuhakikisha
kwamba kiongozi aliyechaguliwa anatimiza wajibu wake ipasavyo
2. Kumwondoa
kiongozi madarakani kwa kufuata sheria na kwa kupiga kura ya hapana
3. Kudai
haki za msingi kwa viongozi wanaosimamia kutoa maamuzi
4. Kuelewa
sheria zote zilizopo na kuishi kufuatana na sheria hiyo
5. Kutambua
uwezo mwananchi alionao ili aweze kushiriki katika shughuli mbalimbali za
maendeleo
Haya sasa kazi kwako kupata elimu
hiyo isiyotozwa ada wala isiyokuwa na mtihani lakini uitumie kama ngao ya
kukombolea jamii yako……
Asanteni sana na tukutane wiki
ijayo
0 comments:
Post a Comment