TAFAKURI
YANGU
Na mwandishi
wetu,
Asalam aleykkum,
Tumsifu Yesu kristo ndugu zako wakazi wa Terat na wanaumajimui wa jamvi hili.
Nisisahau kusalimia kulingana na umri na rika, airoroki ndai loo akwi, airoroki
ndai loo papa, endasupai lepaiyani naidipaki aajo endasupai le muran???
Wooj!!!! Esamiakaki taa noo yeiyo aamu ituarikino ndai, Endakwenye noo koko oo
noo yeiyo??? Marikino siake selengen, Endasupai indoiye????
Wanawanchi kama
nilivyo ahidi awali kwamba kila siku za Jumanne na Ijumaa nitakuwa nawaletea
mfululizo wa elimu yangu juu ya mambo mbalimbali yanayozunguka jamii kisiasa,
kijamii na kiuchumi. Leo nafungua ukurasa kwa kuanza na makala hii ambayo
naamini itatoa darasa la kutosha kwa wanajamvi wenzangu. Makala hii itakwenda
kwa jina la TAFAKURI YANGU, ikiwa na manna ya mawazo yangu (my thought, meditation).
Tafakuri la leo linatanabaisha juu ya MAPATO YA SERIKALI ZA MITAA/VIJIJI.
Ungana na mwanatafakuri wetu ili uweze kupata elimu hii ya bure ambayo haitozwi
ada wala hela ya dawati.
1. Mapato yanayotokana na shughuli za kibiashara na
viwanda zinazomilikiwa na na au huduma zinazotolewa na mtaa/kijiji.
2. Fedha zinazotokana na leseni, vibali, ada na
ushuru ulioainishwa katika sheria ndogo zinazotungwa na halmashauri ya
kijiji/mtaa.
3. Fedha zinazotokana na upangishaji wa majengo ya
halmashauri ya kijiji/mtaa.
4. Fedha itokanayo na mikopo ambayo halmashauri ya
kijiji/mtaa imepata kutoka taasisi zinazokopesha fedha au kutoka mahali
pengine.
5. Mapato ya halmashauri ya kijiji/mtaa kutoka kwa
mtu au taasisi ya umma au serikali au halmashauri ya wilaya au ya mji kama
mchango, ruzuku, fidia au namna nyingine yoyote.
6. Fedha inayotokana na sheria ya kodi ya burudani
inayokusanywa ndani ya eneo la kijiji/mtaa (sheria Na.21 ya 1970)
7. Kodi inayolipwa na kukusanywa ndani ya eneo la
kijiji/mtaa kutokana na wenye nyuma za wageni.
8. Ushuru unaotozwa kutokana na sheria ndogo ya
kijiji/mtaa kwa biashara za rejareja, usagaji na ukoboaji wa nafaka, uuzaji wa
mkaa, mbao na bucha zilizo ndani ya eneo la kijiji/mtaa na katika miji midogo
ya biashara:
a)
Biashara
ya rejareja Tsh 15,000
kwa mwaka
b) Mashine za kusaga unga Tsh 20,000 kwa mwaka
c)
Mashine za
kukoboa Tsh 15,000 kwa
mwaka
d) Biashara ya mkaa Tsh 15,000 kwa mwaka
e)
Biashara
ya kuuza mbao Tsh 20,000 kwa
mwaka
f)
Bucha Tsh 10,000 kwa mwaka
9. Mapato mengine yoyote halali yanayopatikana kwa
njia nyingine.
10.
Fedha
atakayotozwa mtu yeyote kama faini ya kuvunja sheria ndogo ya kijiji/mtaa.
11.
Kwa mujibu
wa sheria ya ardhi ya vijiji (Na.5 ya 1999 kifungu cha 18(1)(f) Halmashauri ya
kijiji/mtaa kinaweza kutoza wanakijiji ada ya mwaka ya hakimiliki za kimila za
ardhi yao.
12.
Chanzo
kingine cha mapato ya serikali za vijiji/mitaa kinatokana na kanuni za serikali
za mitaa za taratibu za ukusanyaji wa kodi (GN No. 346/87). Kanuni hizi
zinateua serikali za vijiji kuwa wakala wa halmashauri ya wilaya/miji na
kuagiza halmashauri ya wilaya/miji kulipa halmashauri ya kijiji/mtaa asilimia
17 au zaidi ya fedha zilizo kusanywa na serikali ya kijiji/mtaa na kumlipa
mwenyekiti wa kitongoji 3% ya fedha alizokusanya.
Je, Kati ya vyanzo vyote hivi ni vipi vipo kwenye kata yetu ya terat na
vinanufaishaje kata yetu???
Asanteni na tukutane tena jumanne ijayo..
Cont: 0712 814 285
Mosi ya yote heko kwa kuvua tuone nyeti zilizofichika,pengine kujua ni limbuko la kuchukua hatua.Utapyamlo kifikra kwa viongozi ni janga kubwa mno kwa jamii inayothubutu au kumakinika kuendelea. si miundo mbinu tu yapo matatizo utitili pengine bila hata wahisani kwa malighafi tulizonazo tungeyasikia tu kwa wenzetu. Ila pia kuoza kwa viongozi si kuoza kwa jamii yote, mida imefika ya tambuka na wanajamii, ndani ya jamii ndiko viongozi watokako. Hesebu hii ndogo kuitanzua ni rahisi kwaani kuchelewa vijusi vya rushwa, udhalimu, ugabachori,ubwenyenye, nk vyazidi kukomaa. mida ya kutoka kwenye nadharia imefika kwaani zaidi ya kuitukuza nadharia bado naamini nadharia bila kutenda ni uhayawani,ninataka nadharia inayorandana na matendo, matendo ya kuuzika utapyamlo wa kifikra na kutungamisha tafakuri za mwelekeo wa umajimuini, kule kusiko na tabaka za kishenzi,kidharimu,kihafidhina wala kinyongaji. Pongezi tena kwa wistle blow,bt hii jamii ya giningi inatuchelewesha kwenye uwanja wa kuutafuta utakatifu yaani mapambano ya haki.Kwa kilitimba zilizopo bila bloodshed hakuna utakatifu,hata tukaandika kwa nakshi na lumbi lukuki,magazeti na mabango yakatapakaa salamu za kimhanga bado tutatoka patupu,NINATAKA BUNDUKI, USINIPE KALAMU NI MWAKA WA KUMI NA TANO NAISHIKA, Prof wangu kazeeka hajaacha kuishika bt haijampa matumaini, ana vitabu maelfu,journal kibao,methali na nahau kajaza bt hakika hakuna dalili ya ushindi coz amepuuza bloodshed sadaka isiyo na doa bt ya haki,NINATAKA MAPINDUZI ya kuuzika unyonge wangu,kunipa amani ya fkra isiyo batili,kuuzika unyonyaji,kumfisha mvuna jasho langu,NINATAKA MAPINDUZI ya kuutetea UTU wangu, kuipata haki yangu,hakika mapinduzi ya kuuleta usawa kwa kiumbe tashi kama mimi,kwayohayo ya kuuondoa ushetani na kunifanya mtakatifu mpenda haki, usheteni uliojijenga ndani ya mfumo dhalimu ya KIBEBERU wenye historia ya damu za mama zangu na uzalilishaji wa baba angu. NITAWAJIBIKA kuushika mtutu hakika kumshinda shetani.Mshikamano imara ushindi daimaa!!!!!!!!!!! Alfayo-0654207885
ReplyDelete