MBINU ZA KUSOMA KWA MAFANIKIO
Asallam
Allaeikum wenzangu waislamu na tumsifu Yesu kristo kwa wenzangu wenye imani ya
kikristo. Vile vile msidhani nimewatenga wale msioamini upande wowote kati ya
hizo mbili nilizotaja, la hasha, ila kwa kuwa hakuna salamu moja
inayowaunganisha wote basi kila mmoja achukue nafasi yake ajisikie ndani ya
moyo wake kwamba nimemsalimu kwa aina ya salamu wanayoitumia kwa imani yao.
Naam!
Baada ya salamu hizo nikiwa na imani kwamba kila mmoja amefarijika kwa kutaja
imani yake na ameitikia kutoka ndani ya nafsi na moyo wake, nami ni mzima
bukheri wa afya tele. Nisileta hoja nyingi sana kwenye utangulizi wa mada ili
nisichoshe medulla yako msomaji kabla ya kupata kupakua kile nilichokiandaa.
Katika
mada yangu iliyopita, nilijaribu kutoa ulumbi wangu juu ya nini cha kufanya ili
mwanafunzi apate matokeo yatakayopendeza machoni kwa yeyeto atakayepata muda wa
kukodolea. Katika mada ile ambayo ililenga kumpa ushauri kuntu mwanafunzi na
mzazi wake juu ya kanuni muhimu za kufuata ili hatimaye awe na matokeo mazuri
mwishoni, nililenga wanafunzi wote hasa kuanzia ngazi ya awali kabisa ya elimu
ya sekondari. Mada ya leo nalenga hasa wale wanaojiandaa na mitihani ya taifa
juu ya mbinu madhubuti za kutumia kwa muda mdogo waliobaki nao katika kujiandaa
kukabiliana na mitihani yao.
Kama
ni jambo linapaswa lizungumzwe na lipewe kipaumbele ni mbinu zipi mwanafunzi
hasa yule anayejiandaa na mitihani ya taifa azitumie ili afanikishe safari yake
kwa mafanikio. Hili linapaswa hasa lizingatiwe na mwanafunzi kwani yeye ndiye
mhusika mkuu katika tukio hilo. Sasa ungana nami katika kujadili baadhi ya
mbinu ambazo mwanafunzi akizifuata na kuzingatia atapata mafanikio katika
mitihani yake. Mbinu hizi za kusoma kwa mafanikio zitafanya kazi tu pale na kwa
yule mwanafunzi ambaye anazifuata kanuni zile nilizozitaja katika mada
iliyopita kwa kuziita principles of a
good and successful student.
Mbinu
za kusoma kwa mafanikio
i.
Tanguliza nidhamu katika kusoma
Kama nitaambiwa nitaje mbinu moja iliyo kuu katika
mafanikio ya mwanafunzi basi sitochelea kutaja NIDHAMU. Mwanafunzi mwenye
nidhamu ni yule anayeheshimu sheria za shule pamoja na kanuni na taratibu
zilizowekwa. Sizungumzii nidhamu kama kuwaogopa waalimu, la hasha, bali
nalitaja neno nidhamu katika tasnia ya elimu kama, kufuata na kuheshimu ratiba
zilizowekwa, kuhudhuria kwenye vipindi vyote kadiri ratiba inavyosema, kufuata
kanuni, taratibu na sheria za shule, kujidhamini na kudhamini mali ya shule na
kuwa mkweli na muwazi kwa wanaumajimui wote.
ii.
Fanya kusoma ni sehemu ya shughuli zako za kila siku
Kama utaambiwa utengeneza ratiba yako ya siku, basi
kusoma uwe umeipa kipaumbele. Kwa kuwa hiyo ndiyo shughuli yao kuu, hapana budi
kuhakikisha kwamba unatumia muda mwingi katika kufanikisha. Kusoma kwako kuwe
ni muda wowote ujisikiapo kufanya vile na hata ule muda ambao mwalimu hayupo
hakikisha unautumia vizuri katika kufanya maswali yanayohusiana na soma husika.
iii.
Tambua fani yako na elekeza nguvu ya ziada huko
Natumaini kila mwanafunzi amalizapo kidato cha pili
hutakiwa kuchagua fani atakayoendelea nayo. Aitha ni sayansi au biashara au
sanaa. Kabla ya kufanya machaguo hayo huna budi kuwashirikisha wadau mbalimbali
wa elimu wanaokuzunguza wakiwepo walimu wako, wazazi, ndugu, jamaa na rafiki
zako. Usifanye machaguo kwa kufuata mkumbo, ama kwasababu wataka kuonekana
kwamba upo juu…. Fanya seleksheni kwa kuangalia pale unapomudu zaidi pia kwa
kufuata ushauri kutoka kwa walimu na wazazi wako na pia kwa kulinganisha na
matokeo yako toka ulipojiunga na elimu ya sekondari.
iv.
Tengeneza ratiba yako ya kujisomea
Mbali na kwamba shule inakuwa na ratiba yake ambayo
hutumika katika kufundishia, kila mwanafunzi mwenye kutaka kufanikiwa hana budi
kujitengenezea ratiba yake binafsi. Hii ni kwasababu muda ambao mwanafunzi
anakuwa darasani akifundishwa ni mchache ukilinganisha na muda anaokuwa peke
yake akijishughulisha na shughuli zingine.
Masaa ambayo mwanafunzi anakuepo darasani kwa siku ni
masaa 6 tu. Hivyo kwa mwezi anakaa darasani kwa jumla ya masaa 132 sawa na siku 5.5. Kwa mwaka mwanafunzi hukaa
darasani kwa muda wa miezi isiyozidi 9. Kama kila mwezi anasoma siku 5.5 basi
kwa mwaka ataingia darasani kwa siku zisizozidi 50 kati ya siku 365. Kwa maana
hiyo kwa jumla ya miaka minne atakaa darasani kwa siku si zaidi ya 200 kati ya
siku 1460 ambayo ni sawa na asilimia 13.7 ya muda wake wote wa kusoma ordinary
level. Hivyo asilimia 86.3 zilizobaki mwanafunzi anakuwa free kufanya shughuli
zake. Hivyo kuna haja ya kujitengenezea ratiba yako ya kujisomea ili kufanya “effective utilization of that ample time”
v.
Soma kwa kushirikiana (Group discussion)
Kusoma kwa kutumia Group discussion, kutamsaidia
mwanafunzi kuelewa zaidi pale ambapo yawezekana hakuelewa vizuri mwalimu
alipokuwa anafundisha. Natambua kasi na uwezo wa uelewa ni tofauti kwa kila
mtu, hivyo kama wanafunzi watasoma kwa group watasawazisha yale ambayo
hayakueleweka ipasavyo kwa upande wao. Vile vile kusoma kwa makundi kunamfanya
mwanafunzi atambue uwezo wake akilinganisha na wengine, na vile vile kuongeza
ushindani miongoni mwao.
vi.
Kuwa karibu na walimu
Mwalimu ana mchango wa 25% katika mafanikio ya
mwanafunzi. Kwa maana hiyo mwanafunzi anayehudhuria darasani na kuwa karibu na
mwalimu wa somo, hata pasipo kusoma ana 25% za kufaulu kwa somo hilo. Hivyo
kama mwanafunzi atakuwa karibu na mwalimu wa somo, kutamsaidia kulipenda somo
husika na vile vile kulazimika kuongeza jitihada zaidi ili kufaulu somo hilo.
Kama atafanya hivyo atakuwa amepata zile 25% za mwalimu na sehemu ya 75% za
yeye mwenyewe kujitafutia.
Idadi
ya mbinu hizi nilizozitoa haimaanishi kwamba ndizo mbinu pekee zilizopo, hasha,
kuna zingine zaidi ambazo msomaji anaweza akazipata kutokana na kusoma makala
hii. Hivyo si vibaya ukaongezea kwani wote tuna lengo la kuboresha elimu yetu.
Nihitimishe
kwa kuwataka wanafunzi wote, walimu na wazazi wajaribu kuzitumia ili tupunguze
ombwe na kadhia hii ya wanafunzi wengi kufeli kwani kuongezeka kwa idadi ya
wanafunzi wanaofeli kunasababisha kuongezeka kwa idadi ya vijana wasio na ajira
na wasio na utaalamu wowote. Hili linapelekea kuongezeka kwa vitendo viovu
katika jamii na uvunjifu wa amani.
Imeandaliwa
na kuandikwa na:
Jina:
Ismail Mesaya
Mob:
+255 756 688 090
Vile
vile utapata kwenye: http:/fukununu.blogspot.com
Asante sana Mungu kwa huu utashi!!!
ReplyDelete