Friday, November 28, 2014
Ndugu
vijana wenzangu na watanzania wote, mustakabali wa taifa letu upo
mikononi mwetu, mustakabali wa vizazi vijavyo ndani ya taifa letu upo
kwenye maamuzi yetu ya leo, mustakabali wa rasilimali zetu upo kwenye
sheria, kanuni na taratibu tunazoziweka kwa sasa, mustakabali wa
kuendelea kuwepo kwa nchi yetu upo kwenye tafasiri tunazozifanya
kwasasa.
Monday, November 24, 2014
IFAHAMU UDSM PART 2
Ndugu mfuatiliaji wa kisa hiki, karibu ungana
nami kwenye sehemu ya pili ya “unaifahamu
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam?” Kabla sijakudokeza wapi tuliishia wiki
iliyopita, nisiwe mchoyo wa fadhila kukupeperushia zangu salamu zikukumbe
popote ulipo. Bila hiyana nikupongeze pia kwa kunipa muda wako tena bure kabisa
kwa kusoma mtiririko wa makala zangu kupitia kitovu cha fikra endelevu cha “Fukununu.blogspot.com”. Hii inanipa
moyo wa kuzidi kuandika, kuanika na kuchimbua na kuibua mengi ambayo yapo nyuma
ya pazia ama yanasikika kwa nadra sana kutokana na mfumo beberu na kandamizi
ulioota mzizi ndani ya jamii yetu hii ya “adabu
na utii kwa bwana mkuu” (Amani)
Friday, November 21, 2014
ILANI YA COMRADE.....
ILANI YA
COMRADE
Asubuhi na mapema, Usingizini nakurupuka….
Lahaja tamu natema, moyoni nafunguka………
Tena bila kuhema, wala machoni kuyumba……
Comrade nanena, huyu mwana anankuna.
Thursday, November 20, 2014
UNAIFAHAMU CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM?
UNAIFAHAMU
CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM?
Uuuuuwiiiiiiii!!!!!!!!!!!! Yarabiiiiii!!!!
Mwaka 2009 nilipatwa na furaha isiyokuwa na kifani baada ya kuchaguliwa
kujiunga na masomo ya juu katika ngazi ya uhasibu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Nilimshukuru maulana kwani ndoto yangu imetimia kwani sio tu kwamba
nimefanikiwa kujiunga na masomo ya juu bali ni kwa kufanikisha ndoto zangu za
kusoma Chuo Kikuu barani Afrika na duniani kwa ujumla. Toka utotoni nalikua na
fikara za kuitwa mwanazuoni wa “Mlimani”…..
NCHI YA KUZIMU
NCHI YA KUZIMU......
Kumi na mbili Aprili, karne ya ishirini....
Wa kwanza si wa pili, Kwa familia mwarobaini......
Nalizaliwa kwenye ukili, Hosipitali hawakuibaini.....
Tanzania Ole nakupenda, ila megeuka nchi jinamizi.
Kumi na mbili Aprili, karne ya ishirini....
Wa kwanza si wa pili, Kwa familia mwarobaini......
Nalizaliwa kwenye ukili, Hosipitali hawakuibaini.....
Tanzania Ole nakupenda, ila megeuka nchi jinamizi.
Wednesday, November 19, 2014
TAFAKURI PART 3
TAFAKURI YANGU.......
Ni jukumu la mtanzania mmoja mmoja kuanzia ngazi ya familia kuanza kujenga jamii mpya yenye uadilifu, kwa hatua taifa lilipofikia hakuna muujiza utakaoweza badili maadili mabovu ambayo kwa sasa yanamulikwa kwa urahisi kupitia kwa viongozi wa serikali ambao ni rahisi kujua maovu yao kutokana na uchungu tulionao kutokana na kodi zetu.Lakini tukiamua kujichunguza kila mmoja wetu utagundua udhaifu uliona au matendo kadhaa ambayo ungekuwa kiongozi ungeyafanya na na kuligharmu taifa kama wafanyavyo wengine.

Sunday, November 16, 2014
Nasaha zangu kwa wakazi wa kata yangu ya Terat.....
Asalam aleikum/Bwana Yesu asifiwe/Endasupai engaji e maa/ Airoroki ndai laisho pookin/habari za muda na wakati huu wadau wote wa maendeleo Terat.
Ni takribani muda kidogo sasa nimekuwa kimya kutoa mawazo yangu juu ya shughuli mbalimbali za kujenga na kukuza uchumi wa jamii na jamaa zetu wa Terat. Hii inatokana na kutingwa kwa majukumu ya kulitumikia taifa langu kwa faida ya vizazi vijavyo....