Music

Friday, November 21, 2014

ILANI YA COMRADE.....



ILANI YA COMRADE
Asubuhi na mapema, Usingizini nakurupuka….
Lahaja tamu natema, moyoni nafunguka………
Tena bila kuhema, wala machoni kuyumba……
Comrade nanena, huyu mwana anankuna.


Nawavuta hadhira, kwa diwani ya mwanagenzi….
Vitendo na nadharia, nawafunda kwa hizi tenzi….
Moyoni nimedhamiria, kukunanga mpenzi….
Comrade nanena, huyu mwana anankuna.

Kimahaba wanifuma, tafasiri ndotoni…..
Huna tabia ya kuchuna, pia kutajwa ugoni….
Wasubiri kuvuna, kwa comrade morani….
Comrade nanena, huyu mwana anankuna.

Unyago hukwenda, tohara pia shakani….
Nyanya kakufunda, kitandani upo makini…..
Wakware wakuponda, usiwasikize mwandani…
Comrade nanena, huyu mwana anankuna.

Mwanadada si mrefu, wala si mfupi wa kimo….
Wa ubani si kifutu, wala si mnene wa tumbo….
Yeye sio sistadu, napenda wake msimamo…..
Comrade nanena, huyu mwana anankuna.
Mweupe si mweusi, hana haja ya mikorogo…..
Shingo kama tausi, madaha kama korongo…..
Macho ya mdalasini, mwana wa matombolo…
Comrade nanena, huyu mwana anankuna.

Jina lako tamu, kutamka ulimini….
Hakuna chachu, kote tamu ndimini…
Deile najiwa hamu, nikiona chako kimini….
Comrade nanena, huyu mwana anankuna.

Mwandani mvumilivu, hang’oki kwa tindo….
Kitabia mstahimilivu, huyu mwanamitindo….
Shani si mvivu, mkarimu kwa vitendo…..
Comrade nanena, huyu mwana anankuna.

Mtoto mashalah, kimawazo unaninanga….
Dah! Inshalah, kwako natia nanga……
Nakushuru Allah, kwa kunipa huyu mwana….
Comrade nanena, huyu mwana anankuna.

Wahuba jina lake kapuni, kuepusha misururu…
Nikimweka wazi hani, nitaanzisha vurugu…
Si kwamba nina wengi, na wala sifanyi kufuru…
Comrade nanena, huyu mwana anankuna.

Naliacha jina hewani, hadhira mtanipendekeza….
Nisiwafunge fanani, wengine kutoendeleza….
Tumieni ukweni, mahari ijapotosheleza….
Comrade nanena, huyu mwana anankuna.

Nihitimu hizi beti, mahususi kwa wangu mwandani….
Ado huniita mwanagenzi, haamini mimi morani….
Masai mtunga tenzi, sasa kabila shakani….
Comrade nanena, huyu mwana anankuna.

Hii ndio elimu, liotapakaa kila fani….
Sijaacha uhasibu, naipenda bila kifani….
Ila isiwe hukumu, kuziacha zingine fani…
Comrade nanena, huyu mwana anankuna.
@Comrade Ole, mahususi kwa mwandani wangu.

0 comments:

Post a Comment