Ndugu
vijana wenzangu na watanzania wote, mustakabali wa taifa letu upo
mikononi mwetu, mustakabali wa vizazi vijavyo ndani ya taifa letu upo
kwenye maamuzi yetu ya leo, mustakabali wa rasilimali zetu upo kwenye
sheria, kanuni na taratibu tunazoziweka kwa sasa, mustakabali wa
kuendelea kuwepo kwa nchi yetu upo kwenye tafasiri tunazozifanya
kwasasa.
Hapa tulipofika tunahitaji hatua ya mwisho kiutawala ili kunusuru existence and furtherance of our nation and natural resources for our sons and daughters as well as the coming generation.
Hatua ya kwanza katika kufikia maamuzi kiutawala ni kwa kufanya MAJADILIANO miongoni mwa makundi mbalimbali yanayokinzana(Table negotiation). Majadiliano haya katika ngazi ya taifa hufanywa na kuratibiwa na hasasi mbalimbali za kijamii, kiraia na serikali. Njia hii ndani ya taifa letu la Tanzania zimefanyika mara nyingi sana na zilionekana kuzaa matunda tu enzi za uhai wa baba wa taifa Hayati Mwl. J.K Nyerere. Vilevile njia hii imeonekana kutoheshimiwa kabisa na kupuuzwa hasa kwenye awamu ya nne ya uongozi wa taifa hili.
Hatua ya pili kwa kawaida hufuata baada ya hatua ya kwanza kuonekana kukwama na mara nyingi hutumiwa ili kuhuisha na kufufua njia ya kwanza ya maamuzi ya kiutawala. Njia hii tunaita SHINIKIZO/VITISHO (Gumboot). Njia hii hufanywa ili kuitahadharisha kundi la utawala juu ya maamuzi yao kulipuuza jambo lililoko kwenye hatua ya kwanza ya maamuzi. Hili nalo limekuwa likifanywa sana na hasasi za kiraia, wanaharakati na vyama vya siasa ndani ya nchi yetu lakini wahusika waliishia kung'olewa meno na kufanyiwa vitendo vya kikatili ikiwa ni pamoja na kuuwawa. Hivyo kwa mara nyingine hatua hii imeshindwa ndani ya taifa letu.
Hatua ya tatu ni KUCHUKUA HATUA (TAKING ACTION). Hatua hii ni kuyatekeleza yale ya hatua ya pili kama kundi la utawala litagoma kurudi hatua ya kwanza ya maamuzi. Hatua hii ni pamoja na kuandamana nchi nzima pasipo kujali itikadi za vyama vyetu na mrengo wetu wa kisiasa bali tu maslahi ya taifa, kulipinga jambo ambalo linaonekana kuwa na madhara hasi kwa taifa letu ama linaonekana kuliumiza jamii.
Ndugu zangu vijana na watanzania wote, ukombozi wa kweli siku zote una gharama na sacrifice kubwa ila udumu milele na kuheshimiwa daima. Katika ukombozi wa mwanadamu, manabii na wafalme wote walijaribu kadri wawezavyo ila hawakufanikiwa kwasababu hawakukubali gharama za maisha yao ili ukombozi huo udumu daima. Nabii Issah/Bwana Yesu alileta ukombozi kwa mwanadamu na ambao ulikuwa ni ukombozi wa kudumu kwa kukubali yeye bila hatia yoyote kutoa maisha yake kama gharama ya kumkomboa mwanadamu. Ukombozi huo hadi leo umedumu na utaendelea kudumu daima.
Nchi za South Rhodesia (Zimbabwe), South Africa, Kenya, France, USA na zingine nyingi sana zilipata ukombozi wao kwa gharama ya watu baadhi kukubali kutoa maisha yao kwa ajili ya vizazi vijavyo. Hadi sasa ndani ya nchi hizi kuna heshima kwa utawala katika kufikia maamuzi kwani aina ile ya ukombozi ulijenga na kuotesha mzizi kwa vizazi na vizazi.
Hoja yangu kwa Tanzania, Ili tuweze kulinda na kuhifadhi rasilimali zetu kwa ajili ya maslahi ya nchi yetu na vizazi vijavyo, hatuna budi sasa kuchukua hatua ngumu ya tatu ya maamuzi. Vyombo vyote vya usalama nawaomba wawe mstari wa mbele katika hili kwa kuwalinda watanzania kwani nasisitiza kama alivyowahi kutamka Wilstone Churchil kwenye hotuba yake kwa wanajeshi kwamba, wao sio mashine kuamuriwa na mtu yeyete ili kulinda maslahi yake hata kwa kudhulumu umma. They have to think and act upon their thinking because they are not machines to be controlled by some people and worse enough is failing to have a free mind for the furtherance of their nation.
Hayo yaliyotokea Misri, Tunisia, Libya, Syria, Ukraine na Cote de avoire ni lazima yatokee kwetu ili maamuzi ya wananchi yaheshimiwe, ili rasilimali za nchi ziheshimiwe, na ili uongozi wa nchi uwaheshimu wananchi na sio kulindana katika masuala nyeti yanayohusu uhujumu uchumi.
Najua waliowengi watanipinga kwa hili kwasababu ya kuogopa gharama hii ya ukombozi lakini niwaonye tu kwamba kuna dalili ya nyota hiyo nyekundu kuanza kuchomoza hapa Tanzania na kama haitaangaza leo basi siku sio nyingi mwangaza wake utaonekana. Hii inatokana na vitendo vya kidhalimu na kiudhalilishaji yanayofanywa na serikali yetu kwa kujisahau kwamba wameajiriwa na watanzania wawaongoze ila wao wana-act like wao ndio wamewaajiri watanzania.
Mungu Ibariki Tanzania.

0 comments:
Post a Comment