Music

Wednesday, November 19, 2014

TAFAKURI PART 3

TAFAKURI YANGU.......

Ni jukumu la mtanzania mmoja mmoja kuanzia ngazi ya familia kuanza kujenga jamii mpya yenye uadilifu, kwa hatua taifa lilipofikia hakuna muujiza utakaoweza badili maadili mabovu ambayo kwa sasa yanamulikwa kwa urahisi kupitia kwa viongozi wa serikali ambao ni rahisi kujua maovu yao kutokana na uchungu tulionao kutokana na kodi zetu.Lakini tukiamua kujichunguza kila mmoja wetu utagundua udhaifu uliona au matendo kadhaa ambayo ungekuwa kiongozi ungeyafanya na na kuligharmu taifa kama wafanyavyo wengine.


Wakati umefika wa kila mmoja wetu kuchukia rushwa na ubadhilifu toka moyoni, kemeadhuruma kuanzia ngazi ya familia, ukoo, marafiki na jamaa wa karibu, onyesha kuwachukia wazi marafiki wenye mienendo mibaya ambayo wakiendelea kukua nayo ni hatari kwa taifa.

AMINI NAKWAMBIA SI RAHISI KUMBADILI MTU TABIA BAADA YA KUPEWA NAFASI ATUMIKIE UMA MAANA NI SAWA NA KUNYOOSHA UKUNI MKAVU. Mimi binafsi naamini kuwa taifa lina hali mbaya na naonesha chuki kwa maovu kuanzia kwangu na ukoo, najitahidi pia kuwajibika kazini kwa haki ya mwajiri, waajiriwa wenzangu na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, kutumikia serikali si lazima ikuajiri, hata kuwajibika vema kwa mambo yahusuyo serikali ukiwa katika sekta binafsi ni uadilifu,tafadhali vijana wenzangu, hasira tulizonnazo tuendelee kuwaonesha wazee lakini pia tushiriki vilivyo kuwalea watoto wetu na wadogo zetu katika maadili huku sisi tukiendelea kubadilika kitabia.

TUSIFANYE KOSA LA WAZEE WETU AMBAO SASA WANASHUHUDIA WENZAO WALIOWAZIDI UJANJA NA KUJIBINAFSISHIA VIWANDA WAKINEEMEKA NA WAO WANAPIGA KELELE AMBAZO HAZIWAZUII JAMAA KULA BATA.
Naipenda Tanzania, nawachukia mafisadi

0 comments:

Post a Comment