Kumi na mbili Aprili, karne ya ishirini....
Wa kwanza si wa pili, Kwa familia mwarobaini......
Nalizaliwa kwenye ukili, Hosipitali hawakuibaini.....
Tanzania Ole nakupenda, ila megeuka nchi jinamizi.
Kwa tabu nilisoma, praimari hadi chuo....
Kwenda shule sikukoma, pamoja na changamoto hizo.....
Kwetu elimu noma, machungani ndio kituo....
Tanzania Ole nakupenda, ila megeuka nchi jinamizi.
Mbili na saba mwaka, EPA likutomasa.....
Lowasa akakwama, Uwaziri akautosa.....
Richmond iliwaka, ujamaa wako ukaukosa....

Rada haikuacha kukukira, Dowans nayo likupakata......
Hawakujali mazingira, walimu madaktari tabu walipata.....
Wahusika walirushiana mpira, maswaiba yoyote hawakupata....

Tatizo wewe Kikwete, mafisadi mekumbatia....
Wanataka kukomba vyote, Watuache wananchi tunalia.....
Wamejikusanyia kama Dangote, wengine njaa tunaumia....

Umekua raisi kiziwi, husikii wala huoni......
Kwanini nawe tusikuite mwivi, Kama washirikiana nao chooni....
Safari kenda kwa wiki, ughaibuni umekukaa kooni....

Ukiulizwa wajifanya hujui, kwanini watu wako masikini....
Mheshimiwa hujitambui, na wala hauko makini......
Masai nalia uuuwi, Nchi umeacha na bikini....
Tanzania Ole nakupenda, Ila megeuka nchi jinamizi.
Katiba wamechakachua, Escrow wamekwapua....
Arusha kila siku wanaua, kucha na meno wanatung'oa....
Na hakuna yoyote hatua, mechukuliwa kwa hawa majuha...

Namalizia kwa hili, Mwanagenzi nakulumba....
Mafisadi hapa nchini, Wamekaba hadi kwa mitumba....
Dawa ni kuwafilisi, acha macho kufumba.....

Anza na wauza unga, Malizia na wauza nyara...
Situdanganye majina hauna, na wala usipige mkwara....
Kwa maana vifua watuna, na kukimbilia Mtwara....

0 comments:
Post a Comment