Music

Sunday, November 16, 2014

Nasaha zangu kwa wakazi wa kata yangu ya Terat.....

Asalam aleikum/Bwana Yesu asifiwe/Endasupai engaji e maa/ Airoroki ndai laisho pookin/habari za muda na wakati huu wadau wote wa maendeleo Terat.

Ni takribani muda kidogo sasa nimekuwa kimya kutoa mawazo yangu juu ya shughuli mbalimbali za kujenga na kukuza uchumi wa jamii na jamaa zetu wa Terat. Hii inatokana na kutingwa kwa majukumu ya kulitumikia taifa langu kwa faida ya vizazi vijavyo....


Leo nitapenda nigusie kwenye hili gereza ambalo tunatarajia kuingia hivi karibuni..... Nimetumia jina geraza kwsababu maamuzi tunayoenda kufanya yatatupa taswira na mstakabali wa maendeleo ya jamii na jamaa za watu wa mitaa yetu. Maaumuzi hayo ni mara chache mno hutokea kuwa revoked kama yalivyo maamuzi ya kuswekwa lupango, labda tu kwa msamaha wa raisi.

Siku chache zijazo tunaenda kufanya uchunguzi muhimu kuliko chaguzi zingine zote ndani ya nchi hii kwani tunaenda kuwachagua viongozi ambao ndio wapo karibu zaidi na sisi na ambao ndio wa kwanza kuzijua shida, tabu na dhahama zinazotukumba......

Katika kuelekea kwny kiama hiki, mambo ya msingi ya kuzingatia ni:

1) Tambua kwamba kiongozi unayemchagua atakuwakilisha kwa takribani miaka mitano. Kwa maana hiyo tanguliza hasa uzalendo na mustakabli wa nchi yako kuliko ushabiki na mrengo/msimamo wa kikundi fulani

2)Ubora wa safu ya uongozi wa serikali ya mitaa utazaa ufanisi na utendaji kazi murua wa serikali kuu. Hivyo Serikali za mitaa ni nguzo kuu kwa serikali kuu.

3) Usichague chama ama dini ama jinsia ama rika ama kabila ama ukoo, bali mchague mtu ambaye anatambua matatizo yanayotukumba na atakuwa mstari wa mbele kusimamia kidete utatuzi wa kero hizo.

4) Weka kando ushabiki, mrengo wa dini ama chama cha siasa ili uweze kufanya maamuzi makini na ya busara. Hili namaanisha tusiache kuhudhuria kwenye mikutano ya kampeni yatakayokuwa yakifanywa na wagombea hata kama si wa chama chako kwani kupitia sera zao ndipo utakapoweza kuchagua nazi na kuacha koroma......

5) Usisite kuuliza maswali kwa mgombea kama utaona kwamba sera anazosimama nazo ni nje ya majukumu yake ama sera mfu ambazo hazitekelezeki.....

6) Usimpe kura mgombea ambaye dhima yake kuu ni kueleza madhaifu ya uongozi unaotoka madarakani badala ya kujikita kwenye sababu zinazomfanya atake kupewa nafasi anayoomba na namna atakavyotekeleza sera zake....

Kwa leo niishie hapo ila nawaomba sana sekretarieti ya vyama vya siasa mjaribu kumtafuta mtu ambaye anayajua kwa kina na anashiri kwenye matatizo yanawakumba wakazi wa maeneo husika na sio kumleta mtu ambaye si mkaazi wa mtaa husika kwa kisingizio tu kwamba anakubalika na wananchi......

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Terat

0 comments:

Post a Comment