MAKOSA YA WAZI KWENYE
HOTUBA YA RAIS
1.
Hoja kwamba pesa zilitolewa kwa uamuzi wa
hukumu ya sept 5.2013 sio sahh kwasababu hukumu ilisema ALL AFFAIRS OF IPTL SHOULD BE HANDED TO PAP. Haikusema kama escrow monies ni party of affairs of IPTL
kwasababu zilikuwa kwenye mgororo. hoja ya kusema hukumu ilisema ilikuja baada
ya kikao cha Oct8.2013 kunduchi beach hotel ambacho kiliongeza maneno kwenye
hukumu kwa kusema ALL AFFAIRS OF IPTL INCLUDING
RECEIBLES FROM ESCROW AC SHOULD BE HANDED TO PAP. Huko ni kupotosha hukumu kwani hela za escrow zilikuwa na
mgogoro kati ya Tanesco na IPTL na PAP kununua IPTL haimanishi mgogoro kati ya
IPTL na Tanesco umekwisha bali PAP ingechukua nafasi ya IPTL kwenye mgogoro wa
pesa za escrow. hili Rais kapotoshwa.
2.
Kusema Muhongo atamtoa
bada ya uchunguzi wake ikulu kukamilika ni mbinu ya kumlinda kwani mbona
mawaziri wanne waliohusika ktk oparesheni tokomeza ripoti ya bunge ilitosha
rais kutengua uteuzi wao na kisha rais akaunda tume ya rais uchunguzi. kwann
kwa Muhongo inakuwa kinyume chake?
3.
Bunge liliazimia mamlaka
ya uteuzi ichukue hatua dhidi ya Maswi. Rais anasema suala la Maswi ameliacha kwa mamlaka ya nidhamu
ambayo ni Katibu Mkuu Kiongozi, Hapa Rais
amekwepa Jukumu lake kwani yy ndio anateua na kufukuza Makatibu wakuu. pia suala hili sio jipya kwa Katibu Mkuu Kiongozi ingetosha awe
amekwisha kuchukua hatua za kinidhamu siku nyingi kama TRA walivofanya kwa
wahusika tawi la Ilala.
4.
Hoja kwamba kutaifisha
mitambo ya IPTL kutakimbiza wawekezaji ina mapungufu kwasababu kwa mujibu wa
ripoti ya CAG, PAP alifanya utapeli wa kughushi katika umiliki wa IPTL hivyo
sio mwekezaji mwadilifu hivyo kutaifisha haiwezi kutisha wawekezaji. pia
ifahamike kwamba wawekezaji wengi wanatoka Ulaya na Amerika na nchi hizo ndio
zimezuia misaada kutaka serikali itekeleze mazimio ya Bunge na mazimio ya Bunge
ni pamoja na kutaifisha mitambo hiyo. sasa inawezekanaje nchi hizo zinazotaka
serikali itekeleze mazimio kwamba ndio zikimbie kuwekeza kwa sisi kutekeleza
mazimio husika? hapa ni namna ya kulinda matapeli wanaokuja kwa jina la
wawekezaji
5.
Hoja kwamba mikataba ikiwa
wazi itakimbiza wawekezaji ina mapungufu kwasababu tatu;
a)
Nchi nyingi sasa duniani
mikataba ipo wazi na mfano rahisi ni Ghana na bado wawekezaji hawajakimbikia
kwasababu hiyo. Ndio utekelezaji halisi wa itifaki ya OPEN GOVERNANCE ambayo Tanzania
tulisaini
b)
Kipengele cha
Usiri(Confidentiality clause) kwa mikataba yote kinasema mkataba utakuwa siri
isipokuwa kwa pande za mkataba(parties of contract) na kwa mahitaji ya dola(
statutory purpose). sasa statutory purpose maana yake ni mahitaji ya Serikali,
Bunge na Mahakama. sasa tatizo la sasa ni pale serikali inapokataa kutoa
mikataba kwa bunge kwa hoja ya kipenge cha usiri(confidentiality clause) wakati
kipengele hicho kinaruhusu Bunge kuwa na mamlaka ya kuona mikataba kama part of
state organ
c)
Pia wawekezaji hawa
wanaposaini mikataba hapa wanakwenda kutafuta mitaji kwenye masoko ya mitaji
kwao(stock markets). Kule kwenye masoko ya mitaji wanaweka wanalazimika kuweka
mikataba hiyo wazi na wanaweka. hivyo kwa dunia ya leo ni aibu kuendelea
kufanya mikataba kuwa siri.
6.
Hoja ya kodi. TRA walidai
kodi kwa barua kwenda BOT. na Werema ndio aliandika barua kukataa kodi. Kwakuwa
CAG alikiri ktk ripoti kuwa kodi ilipaswa kulipwa kiasi cha 23bn mana yake
alosema kodi isilipwe anapaswa kuchukuliwa hatua za kutaka kusababisha hasara
hiyo. ikumbukwe Basil Mramba yupo mahakamani
mpaka sasa kwa kesi ya kusababisha hasara ya 11bb. inawezekanaje hawa waishie
kujiuzulu?
7.
Mwisho kauli ya Mhe Rais
kuwa fedha zile ni za IPTL kwasababu tu ziliwekwa kwenye escrow na Tanesco
badala ya kulipwa moja kwa moja kwa IPTL kutokana na mgogoro sio sahh kwasababu
pesa ya mgogoro kati ya Tanesco na IPTL haiwezi kuwa ya IPTL mpaka mgogoro
umalizike na mwenyewe amekiri kuwa mpaka pesa hizo zinatolewa mgogoro ulikuwa
haujamalizika. ni kwa mantiki hiyo pesa hiyo haikuwa sahh kuita ya IPTL. pia
hapa niongeze kwamba Mgogoro wa IPTL kutoza zaidi Tanesco capacity charge
unamanisha ni dhuluma ya IPTL tangu mwanzo wa utekelezaji wa mkataba mwaka 2002
na sio 2006 kama Mhe Rais alivosema. Hii ni kwasababu mgogoro wa IPTL ku
overcharge Tanesco kwenye capacity charge msingi wake ni udanganyifu wa IPTL
ktk mtaji na hivyo hesabu yake inapaswa kuzingatia tangu mwanzo wa utekelezaji
wa mkataba mwaka 2002 na sio 2006 escrow ilipofunguliwa. Hii inakaziwa na
Uamuzi wa mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara (
International Centre For Setllement Of Investment Disputes-ISCID) wa Feb12.
2014.
By David Kafulila(MB)
0 comments:
Post a Comment