Kama ilivyo ada kila tunafikia kuhitimu mwaka, mara nyingi kila mmoja hupenda kumshukuru Mungu, ndugu, jamaa na marafiki kwa kujuimka naye katika kukabiliana na changamoto za takribani siku 365.
Shukrani zangu za dhati ninapoelekea kumaliza mwaka huu wa 2014 nazielekeza kwa kipenzi cha moyo wangu MAMA. Kila ninapojaribu kukumbuka nilipotoka, nilipopitia na hadi hapa nilipo kwa sasa, nabaki na bubujiko la machozi ya furaha kwa jinsi MAMA yangu alivyonitunza na kunilea.
Nilifanya makazi ya kuishi tumbo lake kwa takribani miezi tisa, na kamwe hakunichoka. Nilifanya kiti na kitanda mapaja yake kwa kukaa na kulala kwa zaidi ya miaka mitatu, pia hakunikinai. Nilifanya mgongo wake lifti na usafiri kwa zaidi ya miaka mitano, vile vile hakunitua. Nilifanya damu yake (maziwa) chakula kwa muda wa zaidi ya miaka miwili, nayo pia hakunibania.
Kwa UPENDO
wake huo MAMA yangu, sina cha kumlipa zaidi ya kumpenda na kumheshimu
sasa na hata milele. Elimu niliyoipata kwake, ni kubwa na ni nzuri
kuliko aina yoyote ya elimu niliyoipata katika ngazi zote za elimu
nilizofika.
Nihitimishe kwa maneno haya, "......MAMA yangu kipenzi, mimi Ismail mwanao na uzao wa kwanza wa tumbo lako, daima nitakuombea kwa Mungu, akulinde, akubariki, akuzidishie hekima na upendo zaidi, akupe maisha marefu zaidi hapa duniani na baraka tele....."
NAKUPENDA SANA MAMA
Kheri ya krismasi na mwaka mpya watu wote

0 comments:
Post a Comment