Music

Friday, December 5, 2014

NASAHA ZA COMRADE MUSA K MOLLEL

UMUHIMU WA SERIKALI ZA MITAA KWA UFUPI.
Serikali yeyote yenye kuwajali wananchi huandaa budget yake kwa kuangalia vipao mbele vya mikoa (hapa ili mkoa, halmashauri, iweze kutoa mapendekezo ya priorities, council lazima itoe maoni ambayo wameyapata kwa 
wdc ya kata. Na ili wdc ikae lazima kila mwenyekiti alete maoni ya mkutano mkuu wa mtaa/kitongoji.) hivyo ndo kusema asili ya budget ni serrikali ya mtaa, lakini pia ili serikali iweze kutekeleza budget lazma serikali ya mtaa ndo mtekelezaji wa mwisho. Hakuna mradi utakaotekelezwa bila kugusa mtaa flani, sasa ndo kusema watekelezaji muhimu wa budget ni viongozi waserkali za mitaa.


Viongozi wa mitaa/vitongoji wanafanya kazi kwa karibu na wananchi zaidi kuliko taasisi nyingine yeyote. Hivyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kuheshimu uchaguzi uliombele yetu wa kuwapata wagombea wazuri watakao tusaidia kusimamia miradi yote au kuibua miradi ya kutusaidia kuleta maendeleo.

UMUHIMU WA KUMPATA KIONGOZI BORA ANAETOKANA NA MFUMO WENYE TABIA WAJIBISHI
Kwanza wananchi wanatakiwa wampate kiongozi ambaye wanaweza kumwajibisha au chama kilichomweka kinaudhubutu wa kumwajibisha. Hii itafsiriwe kuwa kuwa na viongozi wa aina hii sio tu kwamba watafanya kazi kwa uadilifu bali watakua karibu san na wananchi na pia kufanya/ kutekeleza ilani ya vyama vyao(tukifika hapa maendeleo ni lazma na sio hiari).

Hapo juu nimezungumzia mfumo, nijikite kulumba juu ya kiongozi bora. Kiongozi bora kwa sehemu kubwa anatakiwa awe na sifa sifuatazo determined, couragous, honest, participative, humility, faith,proactive & reactive, adaptable, respectful, confidence, enthusiastic, open-minded, rewarding, good communicator,consistent, delegator, organized... sasa kwa kata zetu nyingi ya sifa zinamiss, wananotakiwa kuleta heshima ya uongozi ni vijana wasomi tena wenye ueledi wa taaluma zao. Kata zetu zinahitaji wasomi hasa tena wasomi wazawa. Hata tukiwapa viongozi wasio jua maana ya uongozi lakini akajua kuwa kuna wasomi nyuma yangu atafanya mambo makubwa hujapata ona. Kata yetu sasa ina Ombwe na kiuongozi na wa kuondoa hilo ombwe ni mimi na wewe.

UMUHIMU WA WASOMI KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
Hapa nieleweke nazungumzia umuhimu wa wasomi toka kata yetu kushiriki katika uchaguzi unaoendelea. Wananchi wanahitaji kuelimishwa na wataweza kutoa elimu sahihi ni watoto wao waliosoma kwa kodi na jasho lao. Tumesoma kwa hela za mkaa, hela zinazopatikana kwa jasho lisilo la kawaida kwani muda mwingine wengine walikosa chakula kisa mazao yameuzwa kulipa ada, pia wengine tumesoma kwa kodi za wananchi hasa kwa kulipiwa ada na halmashauri(20,000/=@year kwa miaka minne).Cha ajabu waliotusomesha hatuwajali, tunasahau wajibu wetu na hii imepelekea wananchi wengi kukata tamaa na kitu kinaitwa elimu kwani waliotangulia kusoma hawaoneshi mwanga kwao. Ni kipindi cha kurudisha tumaini lililopota kwao. Sasa niwaase kuwa mchango wako mdogo wa kimawazo una matokeo makubwa sana kwao(hamjui tu heshima ya mawazo yenu kwao).

Wasomi wakinshiriki kwenye hizi chaguzi hata viongozi watakao patikana watakuwa ni viongozi watakao weza kusikiliza pande zote za coin. Viongozi walioko sasa hawawezi kwani muda wote wanajihami kuwa ukikaa karibu na msomi atajua kona zako mapema hivyo atakuumbua. Ili kukata huu mzizi lazma tushiriki katika mchakato hivyo kuwasaidia namna gani ya kuweza kusaidiana katika gurudumu la kutafuta maendeleo.

Sasa nitaanza kufanya spinning program ya campaign
 

0 comments:

Post a Comment